Posts

Showing posts from February, 2020

Iran yatoa wito wa watu kubakia majumbani kuepuka Corona

Image
Idadi ya waliokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini Iran imefikia watu 43 na kuwa taifa la pili lenye idadi kubwa ya vifo nje ya China. Msemaji wa wizara ya Afya ya Iran amearifu kuwa watu 9 wamekufa kutokana na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita na visa maambukizi vimepanda na kufikia watu 593. Serikali mjini Tehran imeamuru kufungwa kwa shule zote hadi siku ya Jumanne na kurefusha likizo ya vyuo vikuu pamoja na kupiga marufuku matamasha na shughuli za michezo kwa wiki moja. Maafisa kadhaa wa ngazi ya juu akiwamo makamu wa rais, naibu waziri wa afya na wabunge 5 wamethibitika kuambukizwa virusi hivyo na kuilazimisha serikali kulifunga bunge pamoja na kuweka marufuku ya kusafiri.

Mwakalinga amtaka Mhandisi Mshauri wa Lusitu - Mawengi kujipanga upya

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mbunifu Majengo, Elius Mwakalinga, amemtaka Mhandisi Mshauri anayesimamia barabara ya Itoni- Ludewa- Manda sehemu ya Lusitu- Mawengi (Km 50), inayojengwa kwa kiwango cha zege kujipanga upya kutokana na kutoridhishwa na kasi ya utendeji kazi ya mkandarasi wa mradi huo. Akizungumza wakati akikagua mradi huo mkoani Njombe, Mwakalinga amemuagiza Mhandisi Mshauri huyo kuhakikisha anawasilisha taarifa zote  na muhtasari wa vikao wanavyokaa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), ofisini kwake, ili aone kama anahifadhi taarifa hizo na anatekeleza yatokanayo na vikao hivyo. “Sijafurahishwa na utendaji kazi wa Mkandarasi, nimewaagiza waniletee taarifa zao zote pamoja na muhtasari wa vikao vyote wanavyokaa wakiwa na TANROADS ili nione kama anatekeleza maagizo anayopewa, na kama hatekelezi ni kwa nini yupo mpaka sasa hivi”, amesema Mwakalinga. Mwakalinga, amefafanua kuwa Mkandarasi huyo haj...

Klopp haamini kilichotokea kwenye dimba la Vicarage Road

Image
Mshambuliaji wa umri wa miaka 22 Msenegal, Ismaila Sarr (katikati) amefunga mabao mawili dakika za 54 na 60 katika ushindi wa 3-0 wa Watford dhidi ya Liverpool, bao lingine la wenyeji likifungwa na Troy Deeney dakika ya 72 Uwanja wa Vicarage Road kikosi cha Jurgen Klopp kikipoteza mechi ya kwanza ya msimu katika Ligi Kuu ya England.

MAGAZETI YA LEO 1/3/2020

Image

Rais wa Zanzibar ahakiki taarifa zake katika daftari la mpiga kura

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja , akisuburi Kitambulisho chake cha mpiga kura baada ya kuhakikiwa na Mkuu wa Kituo cha Kijiandikisha Wapiga Kura Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya Kati Unguja.Bi.Salma Abdulla Mussa.(Picha na Ikulu).29-2-2020.

Simbachawene ajitosa kumsaidia mama aliyejifungua mapacha watatu Mpwapwani

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiwaangalia watoto mapacha watatu waliozaliwa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mama Mzazi wa watoto hao, Mariam Jonas. Simbachawene ameahidi kuwahudumia mapacha hao mpaka watakapo kuwa watu wazima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akiagana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpwawa, Dkt Hamza Mkingule, baada ya kufika hospitali hapo kuwaangalia watoto mapacha watatu waliozaliwa katika Hospitali hiyo, Mjini humo Mkoani Dodoma. Simbachawene ameahidi kuwahudumia mapacha hao mpaka watakapo kuwa watu wazima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto), akizungumza na mama aliyejifungua watoto watatu mapacha, Mariam Jonas, katika hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa. Simbachawene ameahidi kuwahudumia mapacha hao mpaka watakapo kuwa watu wazima. Picha na Wizara ya Mambo ya N...

VIDEO: Taarifa za uzushi kuhusu hoteli ya rivertrees

Image
Baada ya Kuzuka taarifa za Uongo kuhusu Virusi vya Korona kwenye Hotel ya River Tree Iliyoko Arumeru Muungwana Tv Tumefika katika Hoteli hiyo na kukanusha pia kwamba hakuna mtu yeyote ambaye anaumwa hivyo wamesikitishwa na aliyezusha taarifa hiyo TAZAMA FULL HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

VIDEO: Wahamiaji haramu Mkoani Kagera wakithiri ,asilimia 95 ni wakimbizi

Image
Wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera inakabiliwa na wimbi la  wahamiaji haramu huku takribani asilimia 95 ya wakazi katika Kata ya Kakunyu wakithibitika sio raia wa Tanzania Naibu  Waziri  wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni anatembelea wilayani hapo ikiwa ni mkakati wa serikali kukabiliana na tatizo hilo linalohatarisha hali ya ulinzi na usalama  kwa  raia halali Mia Tatu Kumi na Tisa (319) huku  wasio raia wakitajwa kufikia Elfu Sita Mia Tatu Kumi na Moja(6,311) katika Kata ya Kakunyu TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

Marufuku kushikana mikono na kukumbatiana

Image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wananchi kuacha kupeana salamu ya kupeana mikono na kukumbatiana hasa kipindi hiki cha tishio la virusi vya cororna. “Katika kipindi hiki cha tishio la virusi vya corona nawataka Wananchi wajizuie kabisa kupeana mikono, kukumbatiana na kupeana mabusu, najua ni ngumu hii kwa Watanzania lakini tujitahidi ili kujiepusha na kuwaepusha wenzetu na maambukizi”- WAZIRI UMMY @ummymwalimu • “Njia kuu za kuambukizana corona zinatoka kwenye majimaji, kwahiyo unavyombusu, kumkumbatia au kumshika mkono mwenzio unamuweka kwenye hatari, na kama utampa mkono haraka kanawe maji, kwa kipindi hiki tusalimiane hata kwa ishara na usipopewa mkono usinune” -WAZIRI UMMY MWALIMU

Viwanja Vimeshuka Bei: Bunju na Mapinga

Image
Viwanja vipo Kimele/Mapinga (mpakani mwa Bunju na Mapinga. Vipo viwanja vya bei zifuatazo: Mita 10 /20 ni tsh 2.5 mil, Mita 15/20 ni tsh 4 mil, Mita 20/20 ni tsh 5 mil, Mita 20/30 ni tsh 7 mi, Mita 20/40 ni tsh 10 mil, Robo eka ni tsh 11 mil, Nusu eka ni tsh 21 mil, Eka moja ni tsh 41 mil Viwanja hivi vipo umbali wa km 2 kutoka main road (Dar to Bagamoyo Road) Na huduma zote za umeme na maji zipo. Ukipata ujumbe huu mjulishe ndugu/jamaa/rafiki. Hakuna dalali/udalali Mpigie mhusika: 0758603077, Whatsap 0757489709

Serikali yatoa tamko kwa Uhamiaji, NIDA kuhusu wahamiaji haramu Misenyi

Image
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ameitaka idara ya uhamiaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA),kuongeza nguvu kazi katika Wilaya ya Misenyi baada kugundulika uwepo wa wahamiaji haramu wengi wanaotishia hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa wa Kagera unaopakana na nchi za Uganda na Rwanda.  Ameyasema hayo baada ya kusikiliza taarifa ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya  Misenyi iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,Kanali Denis Mwila iliyoweka wazi  idadi ya asilimia 95 ya wakazi katika Kata ya Kakunyu iliyopo Wilayani Misenyi Mkoani Kagera ni wahamiaji haramu huku sababu kubwa zikitajwa za ongezeko hilo ni  kuletwa kwa wahamiaji hao kutafuta ajira na kutafuta mashamba ya maeneo ya malisho ndani ya Ranchi ya Taifa. “kuna haja ya kuleta nguvu kazi  kubwa sana kutoka idara ya uhamiaji na NIDA,lazima tuwe na takwimu halisi ya kila mtu aliyeko katika maeneo haya ambayo yana mashaka,nchi yetu inakaribia kufanya uchaguzi mku...

Kim ataka juhudi kali zaidi kuizuia Corona

Image
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametaka juhudi madhubuti zaidi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, akisema kutakuwa na athari mbaya sana iwapo ugonjwa huo utaingia nchini mwake.  Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini limesema hii leo kwamba Kim ameiagiza ofisi kuu ya kitaifa ya mapambano dhidi ya majanga kuimarisha uchunguzi na vipimo ili kufunga njia zote zinazoweza kutoa mwanya kwa virusi hivyo kuingia nchini humo. Kim aliyekuwa kwenye kikao cha chama tawala, amesisitiza kwamba timu zote zinatakiwa kuheshimu mwongozo uliotolewa na ofisi hiyo kuhusu karantini ya waathirika bila ya masharti yoyote, lakini pia utekelezaji madhubuti wa hatua za kujilinda dhidi ya kile alichotaja kuwa ni virusi tete vinavyosambaa kwa kasi.

Mkuu wa ujasusi wa jeshi la DRC afariki dunia

Image
Mkuu wa idara ya ujasusi wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Delphin Kahimbi amefariki jana Ijumaa baada ya kupata mshituko wa moyo, hii ikiwa ni kulingana na mke wake, kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba kumefunguliwa uchunguzi kuhusu madai kwamba alijaribu kulivuruga amani ya taifa hilo.  Kahimbi pia alikuwa akikabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya kufuatia madai ya kukiuka haki za binadamu wakati aliporuhusu operesheni za kijeshi dhidi ya waasi mashariki mwa Congo katika miaka ya 2000. Mkewe Brenda Kahimbi ameiambia Reuters kwamba, mumewe alipata mshituko wa moyo akiwa nyumbani na kufariki muda mfupi baada ya kufika hospitalini.  Vyanzo viwili vya usalama wa taifa vimesema Kahimbi hivi karibuni alisimamishwa kwa tuhuma za kujaribu kuficha silaha na kuivuruga amani ya nchi.

Trump awaomba Waafghanistani kukumbatia fursa ya amani

Image
Rais Donald Trump wa Marekani amewaomba Waafghanistan kuikumbatia fursa ya mustakabali mpya, muda mfupi kabla ya kusainiwa kwa makubaliano ya kihistoria ya amani kati ya Marekani na Taliban hii leo mjini Doha. Trump amesema atamtuma waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo kushuhudia utilianaji saini makubaliano hayo, na kando ya shughuli hiyo, waziri wa ulinzi Mark Esper atatangaza azimio la pamoja lililofikiwa pamoja na serikali ya Kabul. Trump amesema kwenye taarifa yake kwamba ahadi zitakazotolewa kwenye makubaliano hayo ya Taliban pamoja na azimio hilo ni hatua muhimu kuelekea amani ya kudumu, itakayowaweka huru Waafghanistan na kitisho cha Al Qaeda na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Makubalino hayo yatashuhudia kuondoka kwa maelfu ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan baada ya zaidi ya miezi 18.

Samatta kuiongoza Aston Villa kuikabili Man City kesho

Image
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta anatarajia kuiongoza safu ya ushambuliaji ya klabu yake ya Aston Villa itakapowavaa mabingwa watetezi wa Carabao Cup, Manchester City, Machi Mosi mwaka huu. Aston Villa ilitinga fainali ya Carabao Cup baada ya kuiondoa Leicester City, huku Machester United ikiondolewa na Manchester City. Mchezo wa fainali ya Carabao Cup utafanyika katika dimba la Wembley jijini London, uwanja wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 90,000. Timu hizo mbili zinakutaka kuwania taji hilo wakati kila moja ikipambana kwa namna yake kwenye Ligi Kuu ya England. Wakati Man City ikipambana kuhakikisha ushindi ili iwakaribie mahasimu wao Liverpool, Aston Villa inapambana kuhakikisha kuwa haishuki daraja.

Ebitoke achukua fomu kushiriki miss Tanzania

Image
Msanii wa vichekesho Ebitoke amechukua fomu ya kushiriki shindano la miss Tanzania kanda ya ziwa akiwa na ndoto ya kuvuka huko na kufika hatua ya kushinda na kuvaa taji la  miss Tanzania. Kupitia ukrasa wake wa intagramu ameandika; "Asanteni sana mashabiki wangu kwa support mnayoendelea kunipa. Napenda kuwajulisha rasmi tayari nimesha jaza form ya kushiriki miss Tanzania kanda ya ziwa 2020 nikiuwakilisha mkoa wangu wa kagera na nimeisubmit kwa wahusika. Ni imani yangu nitafika mbali, nahitaji support yenu !"

Ratiba ya leo michezo ya ligi kuu ya Vodacom

Image
Leo jumamosi february 29 michezo ya ligi kuu ya vodacom inaendelea katika viwanja mbalimbali ambapo  mbali na mechi zote mchezo unaosubiriwa kwa hamu ni kati ya Yanga na Alliance utakaochezwa katika uwanja wa Taifa saa 1:00 usiku.

VIDEO: Agizo la Rais Magufuli kuhusuhu magereza kujitosheleza kwa chakula lafanikiwa

Image
Katika kutekeleza Agizo la Rais Dkt.John Magufuli la kutaka Jeshi la Magereza kujitegemea kwa chakula katika kulisha wafungwa,Gereza la Kilimo Kitengule lililopo wilayani Karagwe mkoani Kagera limefanikiwa kuvuna jumla ya gunia Elfu Tano Mia Saba Thelathini na Mbili ndani misimu minne ya mavuno kuanzia mwaka 2015 mpaka 2019 Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Gereza hilo,Hadari Yuda TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

VIDEO: Simbachawene atoa maagizo haya kwa askari magereza

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi George Simbachawene amelitaka Jeshi la Polisi hapa nchini kuacha kukamata ovyo watu na kusababisha kujaa kwa mahabusu katika Magereza mengi na kusababisha hasara kwani Magereza hayo hawazalishi chochote. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

Yanga, Alliance hapatoshi leo

Image
HATUKUBAHATISHA! Hayo ni maneno ya Yanga kuelekea mechi yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Alliance FC kutoka Mwanza inayotarajiwa kuchezwa leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Yanga itashuka dimbani katika mechi hiyo ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare nne mfululizo katika mechi za ligi huku Alliance ikiwa na kumbukumbu ya kumchapa Mwadui FC mabao 4-1. Akizungumza na gazeti hili jana, Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa, alisema timu yake iko tayari kwa mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani na wachezaji hawana hofu ya aina yoyote. Mkwasa alisema wamejipanga kuendeleza kasi ya ushindi na wanaamini wakifanya vizuri katika mechi zao zinazofuata, wana nafasi ya kuutwaa ubingwa wa ligi ambao sasa unashikiliwa na watani zao Simba. "Maandalizi yetu ni mazuri, timu haina hofu yoyote kuelekea mechi ya kesho (leo), kama baadhi ya mashabiki wenye lengo la kuwavuruga wachezaji wao kisaikolojia wanavyodai, na kuelekea pia katika mchezo wa dhidi ya Simba tuta...

Waziri Jafo afungua kongamano la Mama Lishe Festival Kisalawe

Image
WAZIRI wa Ofisi ya Nchi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Seleman Jafo, amesema kukamilika kwa mradi wa maji  ulioigharimu Serikali kiasi cha zaidi ya Sh Bilioni 10, kutazidi  kukuza maendeleo ya wilaya hiyo ambayo kwa kipindi cha hivi karibuni imeshuhudiwa ikipiga hatua kubwa kupitia sekta za elimu pamoja na afya. Akizungumza wakati akifungua kongamano la ‘Mama lishe’ lililowakutanaisha mama lishe mbalimbali wilayani humo, Waziri Jafo  pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo Jokate Mwegelo kutokana na  juhudi  mbalimbali anazozichukua kuchagiza kasi ya maendeleo ya wilaya hiyo akisisitiza kuwa ana jisikia fahari kumpata Mkuu huyo wa wilaya ambaye ni ‘mchapakazi’ Alisema  kuanza kupatikana kwa huduma ya maji safi na salama ambayo hapo zamani ilikuwa kero kubwa kwa wananchi wa wilaya hiyo, ni jambo walilolipokea kwa furaha wananchi wa Kisarawe na kuongeza kuwa pamoja na hiyo,  huduma zingine muhimu zinazopatikana wila...

Sikuwahi kuwa na ndoto ya kutafuta mali na utajili- Dkt. Kigwangala

Image
Waziri wa maliasili na utalii Mhe. Hamis Kigwangala amesema kuwa katika maisha yake hajawai kuwa na ndoto ya kutafuta mali na utajiri. “Kabla ya Ubunge nilikuwa na kampuni yangu binafsi na sikuwahi kuajiriwa kabisa, pili ninamiliki chuo cha afya na mradi ukikamilika tutakuwa na hospitali hapo, tatu mimi ni mkulima, mfugaji, mfanyabiashara ya mazao na mmiliki wa viwanda, mabasi n.k”  Kigwangalla “Kwenye maisha yangu ndoto yangu haijawahi kuwa kutafuta mali/utajiri, maana kufikiri hivyo ni kufikiri kwa akili ndogo, mimi huwaza na kubuni namna ya kutatua changamoto kwenye maisha ya jamii yangu yote, Ubunge ni fursa ya kuijenga upya Nzega yetu,wala sio ajira” - KIGWANGALLA “Kuna mtu badala ya kumuona Kigwangalla mfano kwake na kwa wanae, anamdharau bure tu, yeye hata ubalozi tu hajafika, hata Masters hana! anaona eti siyo deal kwa Mtoto huyu kupata wasaa wa kuzungumza na Mtu kama mimi”- KIGWANGALLA

Diamond atua studio za Swizz Beatz Marekani

Image
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Diamond Platnumz, ameonekana akiwa katika studio za mtayarishaji maarufu wa muziki nchini Marekani, Swizz Beatz. Hilo linatokea ikiwa ni siku chache zimepita tangu mtayarishaji huyo, aweke wimbo wa ‘Gere’ ulioimbwa na Tanasha Donna akimshirikisha Diamond na ile ya singeli ya ‘Wanga’ iliyoimbwa na Meja Kunta akimshirikisha Lavalava wa lebo ya WCB katika ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram. Kama haitoshi siku sita zilizopita mtayarishaji huyo aliweka video katika ukurasa wake ikimuonyesha  mwanamuziki Alicia Keys ambaye ni mke wake akionekana kucheza wimbo wa Wanga. Diamond katika picha hiyo ameonekana amekaa kwenye kiti akiwa amevaa fulana ya njano wakati Swizz Beatz yeye aliyejiegesha kwenye moja ya mashine ndani ya studio hiyo akiwa amevaa tracksuit ya rangi ya chungwa na kofia yenye rangi ya kaki. Katika picha hiyo, Diamond ameandika ’Kanda! Kanda! nipo na mfalme ananifanya nijisikie kama nipo nyumbani Tanzania, naji...

Waziri Kalemani atoa maagizo TANESCO

Image
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuharakisha utekelezaji na usimamizi wa Miradi ya Umeme inayotarajiwa kuimarisha upatikanaji wa Nishati ya Umeme wa uhakika na unaotabirika Mkoani Kagera. Dkt KALEMANI ametoa kauli hiyo Mkoani Kagera Wakati wa Ziara yake, ambapo amesema Umeme huo Utaunganisha Mkoa huo moja kwa moja na Umeme wa Gridi ya Taifa.“Katika kuunganisha Mkoa wa Kagera na Gridi ya Taifa, tayari tunajenga laini kubwa ya kusafirisha umeme toka Bulyanhulu mpaka Geita na Geita kuja mpaka Nyakanazi na Nyakanazi mpaka Rusumo ambapo Tunatekeleza mradi wa kufua umeme kupitia maporomoko ya Rusumo. Hivyo tutakuwa tumeunganisha Wilaya zote za kagera na umeme wa Gridi ya Taifa” Alisema Waziri Kalemani.

Klabu ya Simba yapata ugeni kutoka Ujerumani

Image
Wageni wa klabu ya soka ya wanawake Simba Queens, timu ya St Pauli ya Ujerumani wamewasili nchini leo Februari 29, 2020 majira ya Saa 9:30 Alfajiri kwa ajili ya kuitembelea klabu hiyo. Kwa mujibu wa taarifa ya Simba, ujio huo wa St Pauli ni muendelezo wa ushirikiano baina ya timu hizo. 'St Pauli wamefika nchini wakiwa na jumla ya wachezaji 15 na watakuwa hapa kwa muda wa siku 15 ambapo pia watatembelea Zanzibar na Morogoro ikiwa ni sehemu ya wao kuufurahia sehemu za kitalii katika Miji hiyo mbali na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki', imeeleza taarifa hiyo. Mbali na kucheza mechi pia wataelimisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia, katika kufanikisha azma ya kufuta unyanyasaji wa kijinsia katika jamii kwa kutumia michezo

Baada ya kukamatwa mbowe aachiwa kwa dhamana

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa katika kituo cha Polisi Bomang'ombe Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kwa zaidi ya saa mbili. Mbunge huyo wa Hai alikamatwa leo Ijumaa Februari 28, 2020 saa 12 jioni baada ya kumaliza kuhutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Nkoromu kata ya Masama Kati wilayani Hai. Amehojiwa kuanzia saa 12:35 jioni hadi saa 3:20 usiku na alipotoka katika kituo hicho amewaeleza waandishi wa habari kuwa hawezi kuzungumza chochote. Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamdun alilieleza Mwananchi kuwa Mbowe amekamatwa baada ya kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano huo. Amebainisha kuwa maneno aliyoyatoa yanaashiria  uchochezi  na kuamsha hisia za wananchi, chuki dhidi ya Serikali ya Tanzania na polisi. "Mbowe amekamatwa baada ya kutuhumiwa kusema au kutoa maneno yanayoashiria uchochezi, kuamsha hisia na chuki dhidi ya Serikali na polisi. Anahojiwa lakini baada ya mahojiano at...

MAGAZETI YA LEO 29/2/2020

Image