Posts

Showing posts from July, 2019

Serikali yanunua magari 12 ya huduma ya dharura na uokozi

Image
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imenunua magari kumi na mbili kwa ajili ya huduma za dharura nchini. Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ukaguzi kwenye ofisi za Toyota jijini Dar es Salaam. Dkt. Ndugulile amesema magari hayo yameletwa muda muafa ikiwa zimesalia siku chache kuanza mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambapo magari hayo pamoja na mabasi mawili ya uokozi yatatumika kutoa huduma za kiafya kwenye mkutano huo na baada ya hapo yatagaiwa kwenye maeneo yaliyoanishwa kwa uokoaji wa majeruhi wa ajali.

Picha: Simba SC waliporejea nchini

Image
Mabingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL), Simba SC wamerejea nchini wakitokea Afrika Kusini alipokuwa wameweka kambi. Kikosi hicho kipo kwenye maandalizi ya mchezo wao watakaocheza kwenye tamasha la Simba Day.

Kumbilamoto achaguliwa kuwa Meya Ilala

Image
Diwani wa Vingunguti (CCM), Omary Kumbilamoto, amechaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Ilala baada ya kumshinda mpinzani wake katika Greyson Selestin aliyepata kura 14. Uchanguzi huo umefanyika Jumatano hii, katika kikao cha baraza la madiwani ambapo Kumbilamoto ameshinda kwa kura 41 kati ya kura 55 zilizopigwa ambapo hakuna kura iliyoharibika. Akizungumza na waandishi baada ya uchaguzi huo, Kumbilamoto amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopata na kila mmoja aliyempigia kura ambapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuomba ushirikiano ili waweze kufanikisha majukumu ya Manisapaa hiyo. “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu  kwa nafasi hii nilioipata na kufanikisha zoezi hili la uchanguzi kufanyika na kuisha salama, nawashukuru madiwani wote mlioweza kunipigia kura za kutosha na hata msionipigia lakini mmefanikisha haki zenu za kidemokrasia. “Kikubwa niwaombe umoja na ushirikiano katika kufanikisha majukumu ya Manispaa ya Ilala inafanya kazi na miradi yot

Makusanyo ya kodi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/19

Image
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imefanikiwa kukusanya jumla ya TZS 15.9 trilioni kati ya lengo la TZS 18 trilion kwa mwaka wa Fedha 2018/19 kuanzia tarehe 1 Julai 2018 hadi 30 Juni 2019. Aidha katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha yaani, mwezi Machi hadi Juni 2019, TRA ilikusanya TZS 1.1 trilioni, TZS 1.2 trilioni, na TZS 1.5 trilioni kwa mwezi Aprili, Mei, na Juni, mtawalia. Kwa namna ya kipekee kabisa, TRA inawashukuru walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kwa ushirikiano. Ikumbukwe kwamba, katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) ambao utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili (2). Awamu ya kwanza, ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo. Awamu hii ya kwanza iliyoanza kutekelezwa tarehe 15 Januari 2019 imeendelea vizuri na maandalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi, na CD/DVDs yamekamilika. Hivo mfumo huu wa ETS kwa awamu

Waziri Mkuu akagua maandalizi ya Terminal III

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekagua jengo la tatu la abiria kwenye kiwanja cha ndege cha Mwalimu Nyerere ili kuona maandilizi ya mapokezi kwa wajumbe wa mkutano wa SADC. Akizungumza na watendaji wa Serikali pamoja na Kamati ya maandalizi uwanjani hapo Jumatano jioni, Waziri Mkuu amesema maandalizi ni mazuri isipokuwa kwa kasoro chache zilizobakia. “Nimepita VIP hakuna shida. Pale terminal 2, sehemu ya Uhamiaji iko vizuri, uchunguzi wa afya nayo iko vizuri, lakini vyoo inabidi vibadilishwe haraka sana. Vile vyoo pale nje vimechoka, vibadilishwe mara moja, siyo tu kwa ajili ya ugeni, bali ni kwa faida yetu pia,” amesema huku akimwagiza meneja wa uwanja huo, Bw. Paul Lugasha aharakishe zoezi hilo. Katika jengo la tatu la abiria kwenye uwanja huo, Waziri Mkuu amekagua eneo ambalo viongozi wakuu wa nchi watashukia, watakagua gwaride la heshima na kuangalia vikundi vya ngoma. Pia amekagua vyumba ambavyo watapumzikia kabla ya kuelekea mjini. Amesisitiza kuwa usafi wa barabarani ba

Waziri Lukuvi atatua migogoro ya ardhi Dar

Image
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amefanya ziara katika maeneo ya Kigogo na Msimbazi Center jijini Dar es Salaami na kurejesha kiwanja cha Bwa. Ramadhan Sudi Balega  kilicho tapeliwa na mtu ajulikanaye kama Bw. Macha  katika eneo la Kigogo. Waziri Lukuvi amerejesha kiwanja hicho kutokana na mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka Kumi kutokana na kuwepo na utapeli katika eneo hilo huku akisisitiza kuendeleo kupambana na matapeli wa ardhi popote walipo kwani Wizara yake haitokubali wanyonge kudhurumiwa katika kipindi chake chote cha uongozi. Lukuvi amerejesha Hati ya jengo lake na kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa msajiri wa Hati ambaye alifanya makosa ya kubadili hati kutoka kwa Ramadhan kwenda kwa Bw. Macha huku akijua kufanya hivyo ni kunyume cha utaratibu na swala hilo linatafsiriwa kuwa ni kitendo cha utapeli. "Nataka kuwapa matumaini wananchi wote walioonewa, haki yako itachelewa tu lakini ipo siku utarudishiwa haki yako nataka kuwapa onyo

Mkandarasi aagizwa kuwasaidia usafiri wafanyakazi

Image
Na. Amiri kilagalila, Njombe Naibu waziri wa ujenzi Elias kwandikwa ametoa maelekezo kwa mkandarasi anayejenga bara bara kwa kiwango cha lami Lot2 kutoka Moronga-Makete,kuwawezesha wafanyakazi usafiri ili waweze kufika kwa wakati katika  maeneo yao ya kazi. Waziri ametoa maelekezo hayo wakati akikagua maendeleo ya mradi mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa waendashaji wa mitambo katika mradi huo kutokana na kutumia gharama kubwa ili kufika sehemu ya kazi. “Nimeelekeza hawa wakandarasi walitazame tuweke mazingira mazuri kwasababu magari yapo,waweze kuwasafirisha kwenye sehemu za kazi na mfanye kazi vizuri”alisema Kwandikwa Hata hivyo naibu waziri huyo amewataka wafanyakazi katika maeneo hayo kutengeneza uongozi ili waweze kufikisha matatizo yao badala ya kusubiri viongozi. “Tengenezeni uongozi wenu wenye busara sio nia ya kugombana ili kurahisisha mawasiliano na matajiri wenu kwasababu  kila mmoja akizungumza itakuwa ni kelele,hii itasaidia bahati nzuri viongozi wenu n

MAGAZETI YA LEO 1/8/2019

Image

VIDEO: CUF yatikisa Handeni Vijijini, mamia wachukua kadi/ Mbunge, Diwani wafunguka

Image
Wabunge saba wa CUF Jumatano hii wameendelea na ziara yao ya kukagua uhai wa chama chao katika baadhi ya vijiji vya jimbo la Handeni Vijijini ikiwemo Hoza, Ruye, Sezakofi, Kwamsisiri nk . Katika ziara hiyo mamia ya watu wamechukua kadi za CUF katika baadhi ya vijiji ambavyo wamevitembelesa ndani ya jimbo hilo. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBCRIBE

Tetesi: Golikipa Kindoki aachwa Yanga SC

Image
Inasemekana golikipa wa Yanga SC, Klaus Kindoki anaachwa ili kutoa nafasi kwa klabu hiyo kusajili mchezaji mwingine (mshambuliaji) wa kimataifa. Inaelezwa kuwa, kulikuwa na mvutano kuhusu kumtema Kindoki ambaye ni raia ya DR Congo wengine wakitaka abakizwe lakini wengine wakasema haiwezekani kukawa na magolikipa wawili wa kimataifa.

Wanaofanya shughuli kwenye hifadhi za wanyama watakiwa kuhama

Image
Wananchi wenye makazi na wanaofanya shughuli zao kwenye hifadhi za wanyama wilayani Songwe, wametakiwa kuhama kutoka maeneo hayo kwa kuwa si salama na yanahatarisha maisha yao kutokana na uwapo wa wanyama wakali. Kwa mujibu wa ofisa maliasili kata ya Kapalala, wilayani Songwe, Benard Nenje, kumekuwapo na matukio mengi ya wakazi wa maeneo yaliyo jirani na hifadhi kushambuliwa na wanyama sambamba na kuharibiwa mali zao ikiwamo mazao shambani. Akizungumza, Nenje alisema kwa mwaka jana pekee, wananchi 24 walipata madhara ya kuvamiwa na wanyama, ambapo kati yao 22 wanatokea kata ya Gua na wawili kata ya Ngwala ambao serikali ililazimika kuwalipa fidia kutokana na mazao yao kuliwa na tembo. Alisema kwa mwaka huu wananchi 30 wanatakiwa kulipwa fidia kutokana na tembo kula mazao yao na wengine kujeruhiwa na simba na fisi. Ofisa huyo alisema asilimia kubwa ya wananchi wanaovamia maeneo ya hifadhi wanakuwa hawaelewi madhara yake hivyo kujikuta wakijenga makazi na kujishughulisha na kili

TUNZA INJINI YA GARI LAKO NA KICHOCHEO CHA NANO

Image
Tunakitambulisha kichocheo madhubuti cha Nano  kilichothibitishwa ubora wake na shirika la viwango la kimataifa (ISO 9001:2015). Hii ni teknolojia ya kipekee na ya kimapinduzi kwenye tasnia ya magari na mitambo. kichocheo cha Nano kimetengenezwa na teknolojia ya kisasa duniani ya Nano (Nano technology) kwa ajili ya kuikarabati na kuipa ulinzi injini ya gari yako bila kuifungua. Kichocheo cha Nano huziba mikwaruzo yote ndani ya injini na kuirudisha nguvu ya injini kama ilivyokuwa mpya. Wasiliana nasi kupitia Namba 0715480174. Kichocheo cha Nano kinaipa injini ganda au tabaka gumu la ceramic na platinum. Tabaka hili linafanya muunganiko wa kudumu na chuma cha injini (cylinder wall) na kina uwezo madhubuti wa kuhimili uchakavu na michubuko itokanayo na msuguano. Inarudisha uwezo wa kusukuma wa injini (compression ratio) kwa kuweka ganda gumu kwenye ukuta wa cylinder. FAIDA ZA KICHOCHEO CHA NANO. Hupunguza matumizi ya mafuta kwa 8% - 21%. Huongeza nguvu ya injini hadi kufikia 10

Kocha wa Simba SC aelezea kambi ya Afrika Kusini

Image
Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amefunguka mara  baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Orlando Pirates kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1. Aussems amesema ameridhika kwa namna timu yake ilivyocheza mchezo huo na kambi waliyoweka nchini Afrika Kusini imekuwa yenye mafanikio sana. “Tumemaliza kambi na Orlando Pirates ambao wapo tayari kuliko sisi [muda walitumia kujiandaa na msimu mpya] lakini tumecheza vizuri. Napenda kuwapongeza wachezaji wangu tulikuwa na wakati mzuri sana Rustenburg, kila mmoja kafanya kazi nzuri tunaweza kusema hii kambi imekuwa nzuri sana na nimeridhishwa” amesema Kocha huyu. Huo ulikuwa mchezo wa nne wa kujipima nguvu kwa Simba SC katika kambi yake ya Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya, baada ya awali kushinda mechi mbili mfululizo na kutoa sare moja.

Pato la kampuni ya Huawei lazidi kupaa

Image
Pato la kampuni kubwa ya teknolojia ya China Huawei limeongezeka kwa asilimia 23.2 na kufikia dola bilioni 58.3 za kimarekani katika nusu ya kwanza ya mwaka huu ikilinganishwa na la mwaka jana. Kwa mujibu wa ripoti ya nusu mwaka iliyotolewa na kampuni hiyo, kiwango cha ongezeko la pato la kampuni hiyo katika kipindi kama hicho kilikuwa asilimia 8.7. Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Liang Hua amesema, uendeshaji wa kampuni ni mzuri, na hali ya kampuni hiyo ni nzuri kama zamani.

Shabiki wa Chelsea afungiwa maisha kwa kumbagua Raheem Sterling

Image
Klabu ya Chelsea ya England imefikia maamuzi mazito ya kutangaza kumfungia maisha kuingia uwanjani shabiki wao ambaye alionesha ubaguzi wa rangi kwa nyota wa Manchester City Raheem Sterling. Chelsea imemfungia maisha kuingia uwanjani shabiki huyo aliyetoa maneno ya ubaguzi wa rangi kwa Sterling wakati akienda kuokota mpira wakati wa mchezo wa Ligi Kuu kati ya Chelsea na Man City December 8,2018 kwenye uwanja wa Stamford Bridge na Chelsea kupata ushindi wa 2-0. Mashabiki wengine watano ambao walitumia lugha kali na za vitisho wamefungiwa kwa muda wa kati ya mwaka mmoja na miwili. Pamoja na kuwa uchunguzi wa jumla kuhusiana na tuhuma hizo za ubaguzi kutokamilika kutokana na madai ya kutokuwa na ushahidi wa kutosha, lakini Chelsea binafsi ilifikia maamuzi hayo baada ya kufanya uchunguzi wao binafsi.

Chile: Watu sita wafariki na wengine 40 kujeruhiwa kwenye ajali

Image
Watu wasiopungua sita wamefariki na wengine 40 kujeruhiwa siku ya jana baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika barabara kuu ya mkoa wa kati wa Chile wa O'Higgins. Basi liliondoka mji mkuu Santiago alfajiri Jumatatu na lilikuwa linaelekea mji wa kusini wa Temuco, umbali wa kilomita 680, lilipopata ajali hiyo. Miongoni mwa waliofariki kulikuwa na wanawake watano na mwanaume mmoja. Uchunguzi bado unaendelea ili kubaini kilichosababisha ajali hiyo.