Posts

Showing posts from November, 2018

NISSAN SAFARI INAUSWA IPO DAR

Image
Nissan safari(BXB) Year :    1990 Cc.    4169 Fuel.  :diesel Engine:TD4 Forglights Selling price :10m Gari imetunzwa vizuri,mmiliki anaweza kubadilisha na gari nyingine kama (1) Brevis (2)Crown (3) IST (4)Mark x (5)Au gari nyingine yoyote nzuri

Kigogo wa CCM atupwa ndani saa 48

Image
Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kata ya Okaoni amejikuta akilala rumande kwa saa 48 kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya baada ya kiongozi huyo kulalamikiwa na wananchi, kuwa amemiliki shamba kwa muda mrefu bila kuliendeleza. Diwani huyo ambaye anafahamika kwa jina la Moria Makoi alituhumiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya kuwa kupitia baraza la madiwani alimilikishwa shamba la kahawa Nkwasira lenye ukubwa ekari 500. Akizungumza mbele ya Mkutano huo, Dc Sabaya amesema "sina kumbukumbu na mwekezaji, huyu ambaye pia ni diwani wa CCM, haiwezekani shamba hili alilopewa na serikali akalime maharage badala ya kulima kahawa." Hali ya kukamatwa kwa viongozi kwa upande CCM imekuwa mara chache kutokea kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho, lakini imekuwa ni tukio la mara kwa mara kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao mara kwa mara wamekuwa wakituhumiwa kuvunja sheria. Machi 2018 Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nag

TAKUKURU yaokoa mamilioni ya fedha yaliyotaka kuibiwa Manyara

Image
Na John Walter-Manyara Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa [TAKUKURU] mkoa wa Manyara kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2018, imefanikiwa kuokoa kiasi cha shilingi milioni 270,973,774.48 zilizokuwa zimefanyiwa ujanja ujanja kutoka kwenye miradi mbambali inayotekelezwa mkoani hapa na kuzirejesha serikalini na zingine kuzielekeza kwenye miradi husika. Pia Taasisi hiyo imeanzisha utaratibu wa kufuatilia fedha zote zinazotolewa na serikali pamoja na wafadhili kwa ajili ya huduma na miradi ya Maendeleo kuanzia bajeti  zinapopitishwa,zinapo pokelewa au  kukusanywa kutoka vyanzo vya ndani na kufuatilia mchakato wa matumizi au manunuzi unapofanyika na katika hatua zote za utekelezaji wa mradi husika. Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Mkuu wa TAKUKURU Fidelis Kalungura, amesema katika ufuatiliaji huo watahakikisha wanadhibiti ucheweleweshaji katika uanzishaji wa mchakato wa matumizi mara baada ya fedha kupokelewa au kukusanywa kwani mchakato wa matumizi na

BMT yaonya rushwa uchaguzi OBFT

Image
BARAZA la michezo la taifa (BMT) limewaonya wajumbe watakaojitokeza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la ngumi za wazi nchini (OBFT) kutoendekeza rushwa na badala yake wachague viongozi halali wenye uwezo wa kuinua mchezo wa ngumi. Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho hilo umepangwa kufanyika leo katika ukumbi wa Baraza la.michezo la taifa BMT. Akizungumza na gazeti hili jana Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkenyenge alisema wapiga kura wanapaswa kuangalia umuhimu wa.mchezo na si maslahi binafsi. Alisema kutokana na hilo wawakilishi wapiga kura kutoka vyama mbalimbali vya mchezo vya mkoa wanatakiwa kuwa makini katika zoezi hilo. “tunaenda kwenye tukio muhimu la uchaguzi, niwaombe wapiga kura kutumia kura zao vizuri kwa kuchagua viongozi wenye uwezo wa kuiongoza OBFT, na niwaambie tu wapiga kura na wagombea kuwa hatutafumbia macho vitendo vya rushwa,” alisema Nkenyenge. Alisema jumla ya wagombea 18 watapata nafasi yakujieleza mbele ya wapiga kura nini watalifanyia Shirikisho hil

Yondani amleta beki huyu Yanga

Image
Beki mkongwe na nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani amesema amesikia taarifa za kutua beki wa Lipuli FC, Ally Mtoni ‘Sonso’ na kutamka: “Mbona yupo freshi tu, nileteeni”. Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu ziwepo tetesi za beki huyo kuwaniwa na Yanga katika usajili huu wa dirisha dogo uliofunguliwa Novemba 15, mwaka huu. Kocha Mkuu wa Yanga Mkon­goman, Mwinyi Zahera hivi karibuni alitoa mapendekezo ya usajili kwa uongozi wa timu hiyo akiomba beki wa kati, kiungo, winga na mshambuliaji ambayo tayari yameanza kufanyiwa kazi. Kwa mujibu wa Championi Ijumaa, Yondani alisema anau­fahamu vizuri uwezo wa Sonso ni beki mwenye sifa zote za kuichezea Yanga ambao ameuo­na akiwa naye kwenye timu ya taifa, Taifa Stars. Yondani alisema kama uongozi wa Yanga ukifanikiwa kumleta Sonso, basi utaimarisha vema safu yao ulinzi ya kati kutokana uwezo mkubwa alionao uwan­jani. Aliongeza kuwa amecheza na Sonso mara kadhaa wakiwa na kikosi cha Taifa Stars na mch­ezo wa mwisho walipocheza na

Mshambuliaji huyu ashtushwa na kasi ya Makambo

Image
Baada ya kufikisha jumla ya mabao 7 mshambuliaji wa Yanga, Herieter Makambo amemshtua mfungaji namba moja kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara, Eliud Ambokile. Makambo amefikisha mabao 7 kwenye Ligi Kuu sawa na washambuliaji wawili wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi hali inayofanya kuwe na vita kubwa ya mfungaji bora msimu huu.  Ambokile amesema kuwa anajifunza mambo mengi hasa kupitia washambuliaji hao hasa namna wanavyopambana uwanjani hivyo hana wasiwasi endapo watampita. "Wanafanya kazi kubwa uwanjani hivyo wanapata kile ambacho wanastahili kupitia wao nami pia najifunza ili kuendelea kuwa bora siku zote. "Sina hesabu za kuwa mfungaji bora ila kazi yangu kubwa ni kuweza kuisadia timu kuweza kupata matokeo, nitafunga kila ninapopata nafasi nina amini kila kitu kinawezekana," alisema.  Ambokile anaitumikia timu ya Mbeya City amekuwa akihusishwa kujiunga na Yanga katika dirisha dogo baada ya kocha kuvutiwa na uwezo wake ili aongeze nguvu kwenye safu ya ushambu

Mshambuliaji wa Simba apata dawa ya kuituliza Yanga

Image
Mshambuliaji  wa kimataifa wa timu ya Simba raia wa Rwanda, Meddie Kagere anajua kwamba wapinzani wao Yanga wanaongoza ligi kwa sasa wakiwaacha nyuma kwa jumla ya pointi 8, ameibuka na kuwatuliza mashabiki wa Msimbazi. Simba wamecheza michezo 12 na kujikusanyia pointi 27 baada ya kushinda mechi 8 sare 3 na kupoteza mchezo 1 wakiwa nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi kuu.  Kagere amesema kuwa hana wasiwasi na wapinzani wao Yanga kuongoza ligi kwa sababu anajua walichokifanya mpaka wakawa hapo na wao wanatakiwa kufanya nini. "Sina wasiwasi na wanaoongoza Ligi kwa sasa kwa sababu najua kile ambacho wamekifanya na sisi tunatakiwa kufanya nini ili tuweze kufika hapo walipo hakuna cha kuhofia. "Wao wameshinda michezo yao na ndio maana wapo hapo hivyo ili nasi tuweze kufika hapo walipofika kazi yetu ni moja tu kushinda michezo yetu hicho tu hakuna kingine," alisema Kagere. Kagere ana jumla ya mabao 7 kwenye ligi kuu msimu huu pia ni mchezaji wa kwanza kuchukua tuzo ya

Bocco awafunda wachezaji wenzake

Image
NAHODHA WA SIMBA, JOHN BOCCO NAHODHA wa Simba, John Bocco, amesema hawapaswi kubweteka kwa ushindi walioupata juzi kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Simba katika mchezo huo ilifanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-1 na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri yakufuzu kwa hatua inayofuata ya michuano hiyo. Akizungumza na gazeti ili, Bocco, alisema kwa sasa ni kama wamecheza dakika 45 za kwanza na dakika 45 za pili watazicheza ugenini hivyo ni lazima wajipange kumaliza mchezo huo. “kazi bado haijaisha, tunatakiwa kujipanga na kuweka akilini kuwa bado tuna kazi nzito mbele yetu, tunaenda kucheza ugenini na wenzetu watakuwa wamejipanga kujaribu kubadilisha matokeo,” alisema Bocco. Aidha, alisema ili kusonga mbele wanapaswa kuwa na nidhamu ya mpira kwa dakika zote 90 watakazocheza ugenini. “Kikubwa tutafuata maelekezo ya makocha wetu, na tutajitahidi kupambana kwa nguvu kuweza kusonga

Mtanzania kusimamia fainali Wanawake leo

Image
ALIYEWAHI KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA SOKA CHA WANAWAKE TANZANIA, LINA KESSY ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama cha soka cha Wanawake Tanzania, Lina Kessy ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kusimamia mchezo wa Fainali ya Afrika kwa Wanawake. Lina atakuwa Kamishna wa mchezo huo utakaochezwa leo kati ya timu ya taifa ya Nigeria dhidi ya Afrika Kusini. Mchezo huo namba 16 utachezwa Accra Sports Stadium kuanzia majira ya saa 10:00 Alasiri. Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), fainali hiyo itachezeshwa na mwamuzi kutoka Zambia, Glady Lengwe, atakayesaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba moja kutoka Madagascar, Lidwine Rakotozafinoro pamoja na  mwamuzi msaidizi namba mbili kutoka Malawi, Bernadettar Kwimbira huku mwamuzi wa akiba akiwa Fatou Thioune. Katika fainali hizo zinazomalizika leo, mwamuzi wa Tanzania, Jonesia Rukyaa alikuwa miongoni mwa waamuzi walioteuliwa kuchezesha fainali hizo ambapo alichezesha mchezo wa nusu fainali kati ya Afri

BREAKING: Rais George Bush afariki Dunia

Image
George H.W. Bush Rais wa zamani wa Marekani George H.W. Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94 huko mjini Houston, msemaji wake Jim McGrath amethibitisha kifo chake. Rais huyo wa zamani wa Marekani aliongoza kwa awamu moja tu akiingia madarakani mwaka 1989 na kuondoka 1993 hivyo kubaki kama Rais pekee aliyeiongoza Marekani kwa awamu moja.

MAGAZETI YA LEO 1/12/2018

Image

Mwanamke mpenda kudumu katika mahusiano ya ndoa, anapaswa kufahamu mambo haya

Image
Wakati mwingine wanawake wanatakiwa kuwaza mambo ya msingi yatakayowasadia wao kwa namna moja ama nyingine kuhakikisha wanaume walionao wanakuwa wa kwao peke yao. Wanawake wengi hufanya kila aina ishara ya upendo kwa wanaume zao, lakini cha ajabu wanaume hao bado hutoka nje ya ndoa zao na kwenda kutafuta vimada vingine, kitu ambacho wanawake hukosea ni kwamba wanawake hao huonesha upendo kwa wanaume zao, lakini ukweli ni kwamba asilimia tisini na tisa( 99%) ya wanaume duniani kote hawahitaji upendo kutoka kwa wapenzi wao, bali mwanaume yeyote yule anahitaji kitu hiki ili mdumu katika mahusiano ya ndoa: Mwanaume anahitaji umuamini. kujenga imani na mpenzi wako ndiyo siri kubwa sana ya kudumu katika mahusiano yenu. Kutokujenga imani na mwezi wako ni mwanzo wa kubomoa mahusiano yenu, hivyo kama itakuwa ni ngumu kujenga imani hiyo unachotakiwa kufanya pale mambo yakiwa hayaendi sawa ni heri kumwambia kuliko kukaa kimya. Hayo ni mambo ya msingi ambayo unatakiwa kufanya ili kudumis

Kwanini utumie nanasi kwa wingi

Image
Kwa mara nyingine tena Muungwana blog inakuja tena mbele ya macho yako ili uweze kusoma makala haya, ambapo siku ya leo tutazungumza ni kwanini ni muhimu kula nanasi kwa wingi. Kwanza kabisa unatakiwa kuelewa ya kwamba tunda la nanasi lina wingi wa vitamin A, B, C pia lina mkusanyiko wa madini ya Chuma, calcium, copper na phosphorous pia watalamu mbalimbali wa maswala ya afya wanatusahauri tule tunda hili kwani linasaidia sana kuimarisha mifupa na misuli ya mwili. Zifuatazo ndizo sababu ya kwanini uendelee kula tunda la nanasi: Husaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza wingi wa maziwa kwa akina mama wanyonyeshao, hivyo ni muhimu kwa watu hawa kuendelea kula matunda haya ili kuongeza kiwango kingi cha maziwa. Kwa wale wenye matatizo ya upungufu wa damu mwili basi tunda hili husaidia sana katika suala kuongeza damu mwili. Pia kama unamatatizo ya kufunga kwa choo basi unashauriwa kuendelea kutumia tunda hili  la nanasi kwani linauwezo mkubwa  wa kuweza kutibu tatizo hilo kwa asilim