Kim ataka juhudi kali zaidi kuizuia Corona


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametaka juhudi madhubuti zaidi katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona, akisema kutakuwa na athari mbaya sana iwapo ugonjwa huo utaingia nchini mwake.

 Shirika rasmi la habari la Korea Kaskazini limesema hii leo kwamba Kim ameiagiza ofisi kuu ya kitaifa ya mapambano dhidi ya majanga kuimarisha uchunguzi na vipimo ili kufunga njia zote zinazoweza kutoa mwanya kwa virusi hivyo kuingia nchini humo.

Kim aliyekuwa kwenye kikao cha chama tawala, amesisitiza kwamba timu zote zinatakiwa kuheshimu mwongozo uliotolewa na ofisi hiyo kuhusu karantini ya waathirika bila ya masharti yoyote, lakini pia utekelezaji madhubuti wa hatua za kujilinda dhidi ya kile alichotaja kuwa ni virusi tete vinavyosambaa kwa kasi.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato