Trump awaomba Waafghanistani kukumbatia fursa ya amani


Rais Donald Trump wa Marekani amewaomba Waafghanistan kuikumbatia fursa ya mustakabali mpya, muda mfupi kabla ya kusainiwa kwa makubaliano ya kihistoria ya amani kati ya Marekani na Taliban hii leo mjini Doha.

Trump amesema atamtuma waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo kushuhudia utilianaji saini makubaliano hayo, na kando ya shughuli hiyo, waziri wa ulinzi Mark Esper atatangaza azimio la pamoja lililofikiwa pamoja na serikali ya Kabul.

Trump amesema kwenye taarifa yake kwamba ahadi zitakazotolewa kwenye makubaliano hayo ya Taliban pamoja na azimio hilo ni hatua muhimu kuelekea amani ya kudumu, itakayowaweka huru Waafghanistan na kitisho cha Al Qaeda na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS.

Makubalino hayo yatashuhudia kuondoka kwa maelfu ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan baada ya zaidi ya miezi 18.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato