Waziri Kalemani atoa maagizo TANESCO

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuharakisha utekelezaji na usimamizi wa Miradi ya Umeme inayotarajiwa kuimarisha upatikanaji wa Nishati ya Umeme wa uhakika na unaotabirika Mkoani Kagera.

Dkt KALEMANI ametoa kauli hiyo Mkoani Kagera Wakati wa Ziara yake, ambapo amesema Umeme huo Utaunganisha Mkoa huo moja kwa moja na Umeme wa Gridi ya Taifa.“Katika kuunganisha Mkoa wa Kagera na Gridi ya Taifa, tayari tunajenga laini kubwa ya kusafirisha umeme toka Bulyanhulu mpaka Geita na Geita kuja mpaka Nyakanazi na Nyakanazi mpaka Rusumo ambapo Tunatekeleza mradi wa kufua umeme kupitia maporomoko ya Rusumo.

Hivyo tutakuwa tumeunganisha Wilaya zote za kagera na umeme wa Gridi ya Taifa” Alisema Waziri Kalemani.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato