Posts

Showing posts from February, 2019

BREAKING: Mbowe na Matiko washida rufaa dhidi ya DPP

Image
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko wameshinda rufaa ya dhamana yao dhidi DPP katika Mahakama ya Rufani. Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana. Wawili hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika. Hata hivyo, baada ya mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo. Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi ulidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu. Rufaa ya (DPP) dhidi ya Mbowe na Matiko ilisikilizwa chini ya jopo la Majaji watatu wakiongozwa na Stella Mgasha, Mwanaisha Kwariko na Gerald Ndika.

Msanii Ariana Grande aongoza kwa wafuasi mtandao wa Instagram

Image
Mwanamuziki wa Pop Ariana Grande amekuwa staa wa kike duniani mwenye idadi kubwa zaidi ya wafuasi (followers) kwenye mtandao wa Instagram, nafasi iliyokuwa inashikiliwa mwanzoni na Selena Gomez. Ariana Grande amefikisha idadi ya wafuasi Millioni 146.3 huku SelenaGomez akiwa nyuma yake kwa wafuasi Millioni 146.2. Kwa miaka mitatu Selena alikuwa ameshikilia nafasi ya kwanza kwa mastaa wenye wafuasi wengi zaidi duniani hadi cristiano Ronaldo alivyompindua Oktoba mwaka jana. Kwasasa anayechezea klabu ya Juventus nchini Italy ndiye anaongoza akiwa na wafuasi wengi zaidi kwenye mtandao huo akiwa na wafuasi millioni 155.9.

Kukamatwa Wabunge wa Upinzani, Msajili wa Vyama atwishwa zigo

Image
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi ametakiwa kutoa tamko kuhusu kamatakamata ya wabunge wa upinzani inayoendelea nchini kwa sasa. Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Katibu Mkuu wa Chama cha Ada-Tadea, John Shibuda ambaye amesema kauli yake kuhusu suala hilo huenda ikasababisha chama husika kumgeuka, hivyo kuna haja suala hilo kutolewa tamko na Msajili wa Vyama vya Siasa kwa kuwa ndiye mlezi wa vyama nchini. "Mimi siwezi 'nika-react' au kutoa 'statement' (tamko) bila chama husika 'ku-appeal' (kukata rufani) kwa sababu naweza nikafanya hivyo, halafu chama kikanigeuka kwamba nisiingilie mambo yao, ila msajili pia anatakiwa atoe 'statement' kwa kuwa ndiye mlezi wetu," Shibuda alisema. Hivi karibuni, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee, aliitwa polisi kwa madai ya kutenda kosa la uchochezi. Wiki iliyopita, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu (Chadema), alikamatwa na kuho

Simba SC kuwafuata Stand United leo

Image
Kikosi cha Simba SC kinaondoka leo mjini Singida kuelekea Shinyanga ambako siku ya Jumapili watacheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United. Hapo jana jioni Wachezaji wa kikosi hicho  walifanya mazoezi kwenye uwanja wa Namfua ili kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo huo. Hadi sasa Simba SC wamecheza michezo 19 ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) na kujikusanyia pointi 48, wakati Yanga Sc na Azam FC waliowatangulia wekundu hao wakiwa wamecheza michezo 25 kwa kila mmoja.

Mwili wa Ruge Mutahaba kuwasili nchini leo

Image
Taarifa kwa Umma. Mwili wa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba utawasili leo saa 9:00 Alasiri kutoka South Africa. Hii ni Ramani ya njia rasmi mwili utakapopita hadi kufikishwa hadi Hospital ya Lugalo kupumzishwa. Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani wametangaziwa kujipanga  pembezoni mwa Barabara wakati mwili wa Ruge ukipita kwa heshima za mwisho. Route yake itakuwa hivi: Airport - Buguruni - Barabara ya Uhuru - Karume - Magomeni - Morocco Hotel - Sinza Kijiweni - Bamaga - ITV - Clouds - Kawe - Lugalo. Ruge Mutahaba atakwenda kuzikwa nyumbani kwao huko Bukoba siku ya Jumatatu, siku ya Jumapili mwili utasafirishwa kwenda Bukoba. Ruge Mutahaba amefariki siku ya February26 mwaka huu nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.

Hatma rufaa ya Mbowe na Matiko kujulikana leo

Image
Mahakama ya Rufani leo inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa iliyokatwa na DPP dhidi ya Wabunge Freeman Mbowe na Esther Matiko. Uamuzi huo huenda ukairuhusu Mahakama Kuu kuendelea kusikiliza rufaa iliyokatwa na washtakiwa hao baada ya kufutiwa dhamana, au ikatupilia mbali rufaa hiyo. Novemba 23, 2018 Jaji Wilbard Mashauri akiwa Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, alifuta dhamana ya Mbowe na Matiko kutokana na kukiuka masharti ya dhamana. Wawili hao walikata rufaa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga uamuzi wa Kisutu kufuta dhamana yao ambapo rufani yao ilipangwa kwa Jaji Sam Rumanyika. Hata hivyo, baada ya mahakama Kuu chini ya Jaji Sam Rumanyika kusikiliza mapingamizi ya pande zote iliamua kuanza usikilizaji wa rufaa hiyo. Upande wa serikali ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Paul Kadushi ulidai kuwa wamekata rufaa katika Mahakama ya Rufani kupinga maamuzi yaliyotolewa na Mahakama Kuu. Rufaa ya (DPP) dhidi ya Mbowe na Matiko ilisikilizwa chini ya jopo la Majaji wat

Waziri Mkuu afurahishwa na ujenzi uwanja wa ndege Julius Nyerere

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.  Waziri Mkuu amesema kuwa amefurahishwa na kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi. Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka. Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha  taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.

BASATA wasitisha usajili wa Dudu Baya

Image
Rayvanny na Dudu Baya  Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetangaza kusitisha usajili wa Msanii Godfrey Tumaini a.k.a Dudu Baya kuanzia siku ya jana November 28, 2019.

MAGAZETI YA LEO 1/3/2019

Image

Zijue sababu zinazopelekea wapenzi wengi kuchokana mapema

Image
Hivi uliwahi kujiuliza hivi ni kwanini baadhi ya mahusiano ya kimapenzi hufa mapema, kama si kufa basi kushuka kwa mahusiano hayo? Moja kati ya sababu ambayo husababaisha kufa kwa mahusiano ni ile tabia ya kuchokana mapema katika mahusiano na moja kati ya sababu kubwa ambayo hupelekea kuchokana mapema ni: 1. Mazungumzo Mazungumzo ni njia muhimu ya kujenga ndoa na kuiimarisha , aidha ni njia ya mkato ya kuchokana na kuchukiana. Mwanamke ambaye hajui wakati gani aseme nini na wakati gani asiseme, hujikuta katika wakati mgumu ndani ya ndoa yake. Kwa mfano: Mwanamke ambaye kila anapoongea na mume wake huanza mazungumzo yake na matatizo na lawama humfanya mumewe awe na woga kila anaposikia sauti yake, na kuiona nyumba chungu, kwa sababu hakuna binadamu anayependa kusikia matatizo tu wakati wote. Mwanamke wa aina hii huwa anamsubiri mumewe kwa hamu kubwa, na anapofika tu na kabla hata ya kupata rizki, anaanza kumsomea orodha ya matatizo; watoto wamerudishwa shule, karo haijalipwa, sha

VIDEO: Video ya mtandaoni yamponza Mkuu wa Soko

Image
Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Arusha, Dkt. Selemani Madeni amekasirishwa na kitendo cha mtumishi ambaye alikuwa mkuu wa soko kuu Arusha kwa kurikodi Video fupi kwa wafanyabiashara wamachinga na kuiweka mitandaoni huku ikionyesha ubishani baina yao na mfanyakazi huyo ambaye alikuwa anadai ushuru kwa machinga ambao wana vitambulisho vya Magufuli. TAZAMA FULLL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE   

Kanuni 15 za Ujasiriamali ambazo ni lazima uzifahamu

Image
Ikizingatiwa kuwa upatikanaji wa ajira umekuwa wa shida sana, watu wengi hujikuta wakiwa na chaguo la kuwa wajasiriamali pekee kwenye maisha yao. Wengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo. Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali. 1. Kuwa mtatuzi wa matatizo Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu. Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hi

Moshi wa sigara ukimpata mtoto uathiri mapafu yake akikua

Image
Utafiti uliofanyika nchini Marekani umebaini kwamba watu wazima wasiovuta sigara lakini walipokuwa watoto wazazi wao walivuta sigara mbele yao,wana hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na maradhi ya mapafu. Watafiti wanasema kati ya watu laki moja ,watu saba hufa kila mwaka kutokana na madhara ya sigara waliyoyapata wakiwa watoto. Watalamu wanasema kinga bora zaidi ya kuzuia watoto kutoathirika na sigara ni wazazi kuacha kuvutaji sigara kabisa. Aidha utafiti huo umebainisha kwamba sio watoto peke yake ndio wanaweza kuathiriwa na sigara bali hata mtu mzima ambaye havuti sigara lakini anaishi au anakuwa karibu na mtu anayevuta sigara. Moshi wa sigara wa saa 10 au zaidi kwa kila wiki unaongeza hatari ya vifo vya ugonjwa wa moyo kwa asilimia 27,kupooza kwa asilimia 23 na madhara katika mapafu kwa asilimia 42 ukilinganisha na wale ambao wanaishi na watu wasiovuta sigara. Utafitit huu ambao umechapishwa kwenye jarida la ' Preventive Medicine' uliwauliza watu kuhusu uvutaj

Zijue Teknolojia 10 zilizovumbuliwa na wanawake

Image
Mara nyingi michango ya wanawake katika sekta muhimu kama Teknolojia na sayansi haionekani lakini historia inaonesha jinsi gani wanawake walivyotoa mchango mkubwa hasa katika karne ya mapinduzi ya viwanda. Leo nimeona nikuletee hii listi ya wanawake waliotoa mchango mkubwa katika kufanya vumbuzi mbalimbali za kisayansi duniani. 1:Florence Parpart. Mwaka 1914 Florence Parpart alivumbua friji la kisasa linalotumia umeme ambapo uvumbuzi huo uliweka rekodi ya dunia baada ya kuvumbuliwa na mwanamke. 2:Marie Van Brittan. Anajulikana zaidi kwa mchango wake mkubwa katika uvumbuzi wa kamera ya cctv mwaka 1969,,ambapo ugunduzi huu aliufanya baada ya kukithiri kwa uhalifu katika jiji la Newyork. 3: Stephanie Kwolek . Stephanie Kwolek atakumbukwa kwa uvumbuzi wake wa material iliyotumika kutengeneza bullet proof. 4:Hedy Lamarr’s . Ni mwafizikia aliyebobea katika maswala ya mawasiliano ambapo aligundua teknolojia ya wireless iliyo saidia kuanzishwa kwa wiFi na mfumo wa GPS. 5:Jose

Mtazamo chanya bila kuwa na kitu hiki ni sawa na bure

Image
Inasemekana ya kwamba mtazamo chanya ni rasilimali tosha dhidi ya kuuaga umaskini, aidha watalamu wa masuala haya ya elimu ya mafanikio wanazidi kusisitiza ya kwamba ili mtu aweze kufanikiwa anatakiwa kuibeba mitazamo  hiyo chanya kila wakati. Lakini licha ya watu wengi kuibeba mitazamo hiyo chanya wamekuwa wakisahau kitu kimoja, kitu  hicho  ni muhimu sana kwani huenda sambamba na mitazamo hiyo chanya. Na leo nataka nikwambie kitu hicho, kwani kuwa na mtazamo chanya bila ya kuwa na kitu hicho ni sawa na bure. Kitu chenye ni hiki, mtazamo chanya huenda sambamba na " kuwajibika" watu wengi kama ujuzi  na maarifa wanayo ya kutosha, ila tatizo ni kule kunakowafanya watu hao kuwa mtazamo chanya zaidi ila wamesahau kuwajibika juu ya kitu walichonacho. Tangu umeanza kujifunza mambo mbalimbali ya mafanikio naamini mpaka sasa kwa sehemu fulani una mtazamo chanya juu ya jambo fulani, ila kinachokoseana kutoka kwako ni kule kunakoitwa kuwajibika juu ya mtazamo huo. Hivyo mimi

NBS na Sheria mpya ya utoaji Takwimu

Image
Ofisi ya Taifa ya Takwimu –NBS imetoa maelezo ya marekebisho ya Sheria ya Takwimu Namba 9 ya mwaka 2015 katika ofisi za takwimu zilizopo barabara ya Sokoine jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano, Mkurugenzi Mtendaji wa NBS, Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa sheria ya takwimu ya Mwaka 2015 imerekebishwa kupitia Sheria Namba 8 ya mwaka 2018. Dkt Chuwa amesema “Lengo la marekebisho hayo, ni kuimarisha utaratibu wa usambazaji takwimu nchini, kwa nia ya kuepusha kutoa takwimu zinazokinzana kwa jamii, pia, marekebisho hayo yanalenga kuimarisha mijadala ya kisera pamoja na matokeo yake’. Aidha, marekebisho ya sheria hiyo ambayo yamejikita zaidi katika kuweka utaratibu wa uchambuzi wa kina kutumia mfumo wa kuweka takwimu ‘Dataset’ zinazotokana na tafiti  kadhaa ambazo nyingi zimewekwa kupitia kwenye tovuti  ya NBS na baadhi zipo kwenye hifadhi zetu, amesema Dkt. Chuwa. Akieleza utaratibu wa utoaji wa takwimu ambazo zitatofautiana na zilizotolewa awali n

Mrisho Mpoto amtolea maneno mazito Diamond 'Ruge amefariki njoo umzike'

Image
Baada ya kuenea kwa taarifa za msiba wa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Clouds Media, Msanii wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto amemtaka Msanii wa Muziki ambaye tangu Mkurugenzi huyo afariki hajaposti chochote hivyo amemuomba msanii huyo kwenda kumzika. Mrisho Mpoto  amemuomba msanii huyo aende akamzike Ruge, kama anamheshimu na kumsikiliza. "Nasib Abdul nimekwita jina lako la kuzaliwa mimi kama kaka yako unaeniheshimu na kunisikiliza nakwambia. RUGE MUTAHABA AMEFARIKI nakuomba NJOO UMZIKE... Nimemaliza," ameandika Mrisho Mpoto kwenye ukurasa wake wa Instagram. Tangu kutokea kwa msiba huo hata Media yake ya Wasafi Tv hawajaandika chochote kuhusiana na msiba huo ila wasanii walio chini ya lebo yake ya WCB wamendika kuhusu msiba huo kupitia kurasa zao za Instagram.

IGP Sirro atoa neno kwa Wafanyakazi na wananchi wanaozunguka Mradi wa SGR

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,  IGP Simon Sirro, amewataka wafanyakazi na wananchi wanaozunguka Mradi wa Reli ya Kisasa SGR kuacha kujihusisha na vitendo vya kihalifu badala yake watoe ushirikiano kwa Kampuni ya Yapi Merkezi inayojenga mradi huo unaotumia fedha za ndani za Watanzania. Akizungumza wakati alipofanya ziara kwenye mradi huo kutoka kituo cha Ilala hadi Kilosa mkoani Morogoro, IGP Sirro amesema kuwa, kila mmoja anayo nafasi ya kufanya ili kuhakikisha mradi huo unamalizika kwa haraka na katika muda uliopangwa bila kuwa na vikwazo. Aidha, IGP Sirro amesema kuwa, Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha usalama unakuwepo wakati wote hata pale mradi huo utakapokamilika na kukabidhiwa kwa serikali. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, amesema kuwa ziara ya Mkuu wa Jeshi la Polisi imewaongezea ari ya kufanyakazi saa 24 bila kuwa na hofu ya kiusalama.

Naibu Waziri, Ikupa awaomba wadau kuwasaidia Walemavu

Image
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ametoa wito kwa wadau kuendelea kutoa msaada wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu kwa kuwa hili ni hitaji endelevu kwa watu hao. Ikupa ameyasema hayo Februari 27, 2019 wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Serikali wilayani Busega mkoani Simiyu wakati akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo. Amewashukuru viongozi wa Wilaya ya Busega kwa namna inavyowasaidia watu wenye ulemavu katika kuwapatia vifaa saidizi huku akibainisha kuwa Serikali inaendelea kufanya jitihada za kuwatafutia na kuwapatia watu wenye ulemavu vifaa hivyo kwa kadri vitakavyopatikana. "Napenda kuwashukuru viongozi wa Busega kwa namna wanavyowasaidia watu wenye ulemavu kupata vifaa saidizi kama fimbo nyeupe kwa wasioona, baiskeli na viungo bandia kwa walemavu wa viungo, mafuta kwa wenye ualbino, lakini niwaombe wadau waendelee kuwasaidia kwa kuwa hili ni hitaji endelevu katika kuishi kwao." alisema Ikupa. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri

Dkt. Kijaju aagiza kuchunguza mkataba wa ukarabati wa shule ya Mzumbe

Image
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amuagiza uongozi wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kuuchunguza mkataba wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya Wavulana-Mzumbe, ulioingiwa kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Shirika la Nyumba la Taifa-NHC ili kujiridhisha kuhusu gharama halisi za mradi baada ya kubaini kiasi kinachodaiwa kutumika kukarabati shule hiyo kinatofautiana na fedha halisi zilizotolewa na Serikali. Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo alipotembelea na kufanya ukaguzi wa ukarabati wa shule kongwe ya Sekondari ya wavulana ya Mzumbe iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro na kuelezwa na viongozi wa wilaya hiyo akiwemoo Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kutokuwa na taarifa zozote kuhusu mradi huo. Dkt. Kijaji alishangazwa na utofauti wa kiwango cha fedha kilichoainishwa katika taarifa ya gharama ya ukarabati wa shule hiyo kwamba ilikuwa shilingi milioni 999.7 wakati kiasi cha fedha kilichotolewa na