Posts

Showing posts from November, 2019

Serikali yaombwa kutatua tatizo la magunia Masasi

Image
Na Hamisi Abdulrahmani, Masasi. Serikali imeombwa kuingilia kati suala la tatizo la ukosefu wa magunia ya kuhifadhia korosho za wakulima wilayani Masasi mkoani Mtwara ambapo bado korosho nyingi za wakulima zipo majumbani mwao na zinashindwa kupelekwa katika minada kutokana na tatizo hilo. Hayo yalisemwa jana wilayani Masasi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi kwenye kikao chao cha kawaida cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika kijiji cha Mbuyuni makao makuu mapya ya Halmashauri hiyo. Walisema kuwa korosho nyingi bado zipo majumbani kwa wakulima zimehifadhiwa sakafuni na kwamba zinashindwa kukusanywa na kupelekwa katika minada inayofanyika kutokana na uhaba wa magunia. Walisema hata idadi ya korosho zilizouzwa kwenye minada na zilizopo kwa wakulima kwa kukosa magunia idadi kubwa zile ambazo zimekwama kwa kukosa magunia ya kuhifadhia. Musa Msanga diwani kata ya Lulindi alisema wanaiomba serikali kuingilia kati suala la uhaba wa magunia kwa wakulima. Alisem

Serikali yatakiwa kuishirikisha Sekta ya Ardhi katika Mipangomiji nchini

Image
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stellah Manyanya ametaka kushirikishwa kwa sekta ya ardhi hasa idara ya Mipango Miji katika miradi mbalimbali inayoibuniwa na serikali ili kuondokana na miradi isiyokuwa na tija kwa jamii. Mhandisi Stellah Manyanya aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mkutano mkuu wa sita wa Mwaka wa Wataalaamu wa Mipangomiji uliofanyika jijini Dodoma. Alisema, kumekuwepo na miradi mingi nchini inayoanzishwa na Serikali na kutumia gharama kubwa lakini  matokeo yake imekuwa haitumiki ipasavyo na wakati mwingine inaingiliana na shughuli nyingine za kijamii hali inayosababisha kuzuka kwa migogoro kwenye jamii. Alitolea mfano Jengo la Machinga Complex  lililopo Ilala Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Manyanya alisema, kutokuwepo kwa mipango kina ya muda mrefu na utafiti duni ndio chanzo kikubwa hadi leo jengo hilo limeshindwa kufikia lengo walilojiwekea la kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo katika shughuli zao. “ Kuna wale wenzetu waliojenga

Mamluki katika Mashindano ya Michezo ya Wafanyakazi kuchukuliwa hatua

Image
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe ametangaza kuwachukulia hatua Wanamichezo wasiokuwa Wafanyakazi  maarufu kwa jina la “Mamluki” wanaoshiriki Mashindano ya Michezo kwa  Wafanyakazi inayojulikana kama SHIMUTA na SHIMIWI endapo watabainika. Dkt.Mwakyembe amesema hayo  leo Jijini Mwanza wakati akifungua michezo ya Mashirika ya Umma  na Binafsi maarufu kwa jina la SHIMMUTA kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluh Hassan ambaye pia ndiye  mlezi wa mashindano hayo ambapo amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuimarisha afya za wafanyakazi,kubadilishana uzoefu pamoja na kutangaza Taasisi zao. “Kuna hili suala la Wachezaji ambao sio wafanyakazi maarufu kwa jina la MAMLUKI kushiriki karika michezo hii,tena nakumbuka kuna kiongozi aliwahi kuwaita “viongeza nguvu bambikizi”,Hapa sio mahala pao nawataka wajiondoe mapema maana tukiwabaini wao pamoja na Taasisi zao tutawachukila hatua”alisema Waziri Mwakyembe Mhe

Real Madrid yarejea kileleni La Liga

Image
Real Madrid leo wamerejea kileleni mwa La Liga baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Deportivo Alaves Uwanja wa Mendizorroza mjini Vitoria-Gasteiz, mabao yake yakifungwa na Sergio Ramos dakika ya 52 na Dani Carvajal dakika ya 69. Bao pekee la Alaves limefungwa na Lucas Perez kwa penalti dakika ya 65 na sasa Real inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 14, ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Barcelona ambao kesho watamenyana na Atletico Madrid.

Liverpool yashindikana Uingereza

Image
Beki Virgil van Dijk akishangilia baada ya kuifungia Liverpool mabao mawili dakika za 18 na 24 mara zote akiimalizia kazi nzuri za Trent Alexander-Arnold katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Brighton & Hove Albion leo Uwanja wa Anfield kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England. Bao la Brighton limefungwa na Lewis Dunk dakika ya 79 katika mchezo ambao kipa wa Liverpool, Alisson alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 76 kwa kudakia mpira nje ya eneo lake

KRC Genk yachapwa, Samatta aendelea kutupia

Image
Klabu ya KRC Genk imeendelea kusuasua katika kutetea Ubingwa wake wa Ligi Kuu Ubelgiji kwa kuendelea kupoteza michezo. Genk wakiwa wenyeji wa Sint-Truiden na wamepoteza nyumbani kwao kwa kufungwa magoli 2-1, Genk ndio walikua wa kwanza kupata goli kupitia kwa Mbwana Samatta dakik ya 9. Mambo yalianza kubadilika dakika ya 18 Yoli alipofunga goli la kusawazisha kwa Saint Truiden, ushindi wa Truiden ukathibitishwa na Suzuki dakika ya 41 baada ya kufunga goli la ushindi, huu ni mchezo wa 7 kwa Genk kupoteza, Samatta akifunga goli lake la saba msimu huu katika Ligi Kuu.

MAGAZETI YA LEO 1/12/2019

Image

Korea Kaskazini yamuonya Waziri Mkuu wa Japan

Image
Korea Kaskazini leo imemuonya waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kuwa hivi karibuni anaweza kushuhudia kile Pyongyang imekiita "Kombora Halisi la Masafa Marefu" baada ya Abe kukosoa majaribio ya mifumo ya ufyetuaji silaha yaliyofanywa na Korea kaskazini. Matamshi hayo yamekuja siku mbili tangu Korea Kaskazini ilipofanya majaribio ya kile ilichokiita " mfumo mkubwa wa kufyetua makombora" huku Korea Kusini ikiripoti kuwa makombora mawili yalianguka kwenye eneo la bahari ya Japan inayofahamika pia kuwa bahari ya mashariki. Wakati wa majaribio hayo yaliyosimamiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Waziri Mkuu Abe alisema Korea Kaskazini ilifyetua makombora ya masafa marefu yanayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa. Korea Kaskazini imesema ni fedheha kuwa Abe ameshindwa kutofautisha kati ya makombora ya masafa marefu na mfumo mpya wa kufyetua makombora ambao nchi hiyo inadai uliuzindua siku mbili zlizopita.

Watakao ajiri watoto chini ya miaka 18 kwenye Tumbaku kukiona cha moto – Waziri Hasunga

Image
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dar es salaam Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesisitiza marufuku yake aliyoitoa hivi karibuni kuhusu ajira kwa watoto ambao wapo chini ya miaka 18. Mhe Hasunga amepiga marufuku hiyo leo tarehe 30 Novemba 2019 wakati akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Kilimo Jijini Dar es salaam. Alisema kuwa suala la ajira kwa watoto ni miongoni mwa mambo yanazuiliwa kwenye Sheria za kimataifa kupitia Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organization) na Sheria za Ajira hapa nchini hivyo mdau yeyote atakayebainika kukiukwa maelekezo hayo atashtakiwa. “Nawasihi wadau wote hususani wakulima wa Tumbaku tuendelee kupiga vita ajira kwa watoto kwa kuwa ni eneo ambalo limeendelea kulalamikiwa na wadau wengi” Alikaririwa Mhe Hasunga Kadhalika, Mhe Hasunga alisema kuwa katika kuhakikisha zao la tumbaku linaendelea kutoa mchango mkubwa katika pato la mkulima na Taifa, Wizara imejiwekea maleng

SOLEO yachangia bidhaa za thamani ya Sh. milioni 52.9 kwa Halmashauri ya Mkuranga

Image
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga yapokea pakiti 264,600 kutoka SOLEO zenye thamani ya shilingi milioni 52.9 kwa ajili ya msaada kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambazo ni virubisho vilivyo na mchanganyiko wa Vitamini na madini. Akitoa ufafanuzi katika kampeni ya uzinduzi wa Mpango wa kupunguza utapia mlo Wilaya ya Mkuranga iliyoandaliwa na kamati ya Lishe Wilayani humo, iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mikere jana, Makamu Mkurugenzi wa shirika hilo Grace Mghamba amesema virutubisho hivyo ambavyo ninaweza kutumiwa na watoto 5880 wamegawa bure wakiwa na lengo la kumsaidia mtoto kwa ajili ya kuondoa utapia mlo na udumavu. Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kaimu katibu Tawala wa Mkoa Abdulrahman Mdimu, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Mkuranga kwa kuanzisha Mpango huu ambao katika Mkoa wa Pwani ni Mkuranga Pekee ndiyo imejipanga na kuhakikisha inaondoa tatizo hilo baada ya kuona Katika baadhi ya Kata zake 10 zinaongoza kwa watoto waliokosa Lishe bora.

Alikiba na RC Mwanri washiriki mbio za Tabora Green Marathon

Image
Msanii wa bongo fleva Ally Salehe Kiba Maarufu kama Alikiba ameshiriki mbio za Tabora green marathon kwa kukimbia km 2.5 zilizoanzia ofisi ya mkuu wa mkoa wa Tabora hadi viwanja vya Ali Hassan Mwinyi zilizofanyika hii leo mkoani humo Akizungumza katika mbio hizo msanii alikiba amesema mbio zimemfanya achangamshe mwili na akili kwani michezo zinajenga urafiki pia zinakutanisha watu na zinaimarisha mwili hivyo amefurahi kushiriki pamoja na mkuu wa mkoa huo na amewahimiza wananchi wa mkoa huo kuwa na utamaduni wa kukimbia ma kufanya mazoezi ili waweze kuwa imara kimwili.  Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri naye alikuwa ni miongoni mwa wakimbia mbio hizo ambapo yeye amekimbia mbio umbali wa km2.5 ambapo amesema msanii alikiba ni mfano wa kuigwa kwani tangu afike mkoani humo katika tamasha lake la muziki linalojulikana kama unfogetabletour ameweza kufanya mambo mengi ya kijamii ‘’Msanii.  Msanii Alikiba akipanda mti nje ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi baada ya kukimbia mbio.

VIDEO: Serikali yakanusha kuwafukuza wakimbizi wa Burundi

Image
Serikali ya Tanzania imekanusha tuhuma zinazoelekezwa kwake kwamba imekua ikiwafukuza wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika Makambi na Makazi  mbalimbali mkoani Kigoma,Tabora na Katavi. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Kocha wa Mbeya City ajiuzulu

Image
Kocha wa Mbeya City Juma Mwambusi amejiuzulu kuifundisha timu hiyo kutokana na mwenendo usioridhisha msimu huu.  Mwambusi  aliwasilisha barua ya kujiuzulu Nov. 26, 2019 na leo bodi ya timu hiyo imeridhia ombi hilo. Kwa sasa timu imekabidhiwa kwa Kocha Msaidizi Mohamed Kijuso.

VIDEO: Mbowe aweka wazi ''Tundu Lissu amechukua fomu''

Image
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA taifa Freeman Mbowe amethibitisha kuwa aliyekua mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amejaza na kusaini fomu ya kuwania nafasia ya makamu mwenyekiti wa chama hicho. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...... USISAHAU KUSUBSCRIBE

Simba yathibitisha kuachana na Patrick Aussems

Image
 Klabu ya Simba imethibitisha kuachana na kocha wao mkuu Patrick Aussems hii leo baada  ya bodi ya Simba kumwambia kuwa kwa sasa yeye sio kocha mkuu wa Simba. Aussems alisimamishwa na Simba kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kutokuwa na melewano mazuri na uongozi wa Simba.

Breaking News: Simba yamtema Patrick Aussems

Image
Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa bodi ya Simba imemwambia kuwa kwa sasa yeye sio kocha mkuu wa Simba. Aussems alisimamishwa na Simba kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kutokuwa na melewano mazuri na uongozi wa Simba. “Bodi ya Wakurugenzi kupitia kwa Mtendaji Mkuu (CEO) imenitaarifu kuwa mimi siyo kocha Mkuu wa Simba” - Kauli ya Kocha wa Simba Patrick Aussems.

VIDEO: Wananchi wamkataa Mwenyekiti aliyeapishwa, watoa tuhuma nzito juu yake

Image
Wananchi kijiji cha Ng'ombe kilichopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza wametoa malalamiko yao kwa Mbunge wao Charles Kitwanga kuwa Mwenyekiti waliompigia kura na yule aliyeapishwa siyo yeye kwani huyo aliyeapishwa amekuwa akiwadhulumu wananchi ardhi na kutafuna fedha za miradi ya kijiji pia kutoa lugha chafu kwa wananchi TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

RC Ndikilo azindua mnada wa Korosho Pwani

Image
Na: Said Likacha - Pwani Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amezindua mnada wa Korosho kwa Mkoa wa Pwani kwenye ghala la kuhifadhia mazao ya nafaka Wilaya ya Mkuranga juzi, huku akiwataka wahusika kuhakikisha ndani ya siku kumi wakulima wanapata malipo yao. Katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa na Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti  wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmshauri sambamba na Bodi ya korosho Tanzania (CBT), Ndikilo ambaye alishuhudia mnada huo wa wazi aliwapongeza washindi wa Kampuni ya Alpha  Choss ambayo itanunua Korosho zote daraja la kwanza kwa Shilingi 2,571 kwa kilo nao (CDJKL) wataonunua daraja lapili kwa Shilingi 2,300 kwa kilo. Ndikilo pamoja na kutangaza mnda wa pili kufanyika Desemba 4 mwaka huu alitumia fursa hiyo kumwagiza Meneja wa Bodi ya Korosho (CBT) Kanda ya Dar es salaam na Pwani Matata afikishe ombi kwa Waziri mwenye dhamana ili Korosho zisizokidhi madaraja hayo mawili ziuzwe kwa mnada kwenye Vyama vya Msingi (AMCOS). Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ul

David De Gea aweka wazi sababu ya Man United kufanya vibaya msimu huu

Image
Golikipa wa klabu ya soka ya Manchester United, David De Gea, amefunguka kuhusu matatizo ambayo yanaikumba timu hiyo ya kupata matokeo mabovu. Akiongea na Sky Sports News, inawezekana ni kutokana na ukosefu wa wachezaji wa kiwango cha juu. "inawezekana matatizo ya sasa ya kikosi cha Man United yanasababishwa na ukosefu wa wachezaji wa kiwango cha juu," amesema De Gea. Kwa sasa Man United inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza ikiwa na alama 17.

Watu wawili wafariki dunia kwenye ajali ya gari lililobeba mashabiki wa Mwakinyo

Image
Watu wawili wamefariki na wanane wamejeruhiwa katika ajali ya gari la timu ya Coastal Union iliyokuwa imebeba mashabiki wa ngumi waliokuwa wakitoka kutazama pambano la bondia Hassan Mwakinyo dhidi ya Arnel Tinampay lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam usiku wa jana. Ajali hiyo imetokea eneo la Kerege wilayani Bagamoyo, wakati mashabiki hao walipokuwa safarini kurejea jijini Tanga.    Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Coastal Union Hafidh Kido imewataja waliofariki kuwa ni Ibrahim Omar na Hussen Saleh ambapo uongozi wa Coastal kwa kushirikiana na ndugu zao, wanafanya taratibu za kuwasafirisha kwenda Tanga kwaajili ya maziko. Hadi sasa miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo. "Majeruhi walikuwa wanane, mmoja hali yake ilibadilika amepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na mwingine tumemkuta hapa anaitwa Aziza, ambaye ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kwakaheza mk

VIDEO: Tumesikia Zahera amekuja, Hatuwezi kwenda kwenye vyombo vya habari kumjibu - Bumbuli

Image
Msemaji wa klabu ya soka ya Yanga, Hassan Bumbuli, amefunguka kuhusu ujio wa kocha wao wa zamani Mwinyi zahera ambaye alitangazwa kutimuliwa wiki chache zilizopita. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Hizi ndio mechi ambazo hutakiwi kuzikosa leo, Samatta ataendelea kutupia?

Image
Jumamosi ya leo ligi mbali mbali barani ulaya zinaendelea kutimua vumbi huku Mbwana Samatta na klabu yake ya KRC Genk wakiwa miongoni mwao. Genk ambao watakuwa katika uwanja wa nyumbani wanatarajiwa kushuka dimbani usiku wa leo majira ya saa 4.30 kucheza dhidi ya Sint-Truidense VV. Michezo mingine ambayo inapigwa leo na hutakiwi kuikosa ni Newcastle United ambao watacheza na Manchester City, Chelsea na West Ham United, Liverpool na Brighton. Pia Totenham Hotspur watacheza na Bournemouth, Bayern Munich dhidi ya Bayer Leverkusen, wakati Alaves dhidi ya Real Madrid.

Waziri Hasunga awataka mawaziri Jumuiya ya Afrika Mashariki kudumisha mshikamano

Image
Waziri wa Kilimo nchini Tanzania Mhe. Japhet Hasunga (Mb) amesema kuwa mawaziri wenzake wa sekta ya zote ikiwemo sekta ya Kilimo kutoka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki wanapaswa kuendeleza na kuongeza umoja na mshikamano ili kuakisi matakwa ya jumuiya katika Uzalishaji wa mazao bora ya Kilimo. Waziri Hasunga amesema hayo Alhamisi iliyopita wakati akichangia mada kwenye  mkutano wa 39 wa Baraza la mawaziri la jumuiya ya Afrika Mashariki ulioketi Jijini Arusha tangu tarehe 21-28 Novemba 2019  wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani Kusini. Mhe Hasunga alisema kuwa kadri ushirikiano mwema utakavyoendelezwa ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii itaimarisha tija na mafanikio ya soko la mazao katika jumuiya hiyo na dunia kwa ujumla. Aidha, amewataka watendaji wote katika nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kutekeleza taarifa mbalimbali zinazoandikwa kwa ustadi mkubwa kwani kwa kiasi kikubwa kumekuw

VIDEO: DC amgeukia mwekezaji ''hatufai''

Image
Mkuu wa wilaya ya Hanang  Joseph Mkirikiti, ataka  Mwekezaji wa shamba la ngano Estate anyang’anywe shamba hilo kwa kuwa ameshindwa kulima. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

TUNZA INJINI YA GARI LAKO NA KICHOCHEO CHA NANO

Image
Tunakitambulisha kichocheo madhubuti cha Nano  kilichothibitishwa ubora wake na shirika la viwango la kimataifa (ISO 9001:2015). Hii ni teknolojia ya kipekee na ya kimapinduzi kwenye tasnia ya magari na mitambo. kichocheo cha Nano kimetengenezwa na teknolojia ya kisasa duniani ya Nano (Nano technology) kwa ajili ya kuikarabati na kuipa ulinzi injini ya gari yako bila kuifungua. Kichocheo cha Nano huziba mikwaruzo yote ndani ya injini na kuirudisha nguvu ya injini kama ilivyokuwa mpya. Wasiliana nasi kupitia Namba  0715480174. Kichocheo cha Nano kinaipa injini ganda au tabaka gumu la ceramic na platinum. Tabaka hili linafanya muunganiko wa kudumu na chuma cha injini (cylinder wall) na kina uwezo madhubuti wa kuhimili uchakavu na michubuko itokanayo na msuguano. Inarudisha uwezo wa kusukuma wa injini (compression ratio) kwa kuweka ganda gumu kwenye ukuta wa cylinder. FAIDA ZA KICHOCHEO CHA NANO. Hupunguza matumizi ya mafuta kwa 8% - 21%. Huongeza nguvu ya injini hadi kufikia