Mkuu wa ujasusi wa jeshi la DRC afariki dunia
Mkuu wa idara ya ujasusi wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Delphin Kahimbi amefariki jana Ijumaa baada ya kupata mshituko wa moyo, hii ikiwa ni kulingana na mke wake, kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba kumefunguliwa uchunguzi kuhusu madai kwamba alijaribu kulivuruga amani ya taifa hilo.
Kahimbi pia alikuwa akikabiliwa na vikwazo vya Umoja wa Ulaya kufuatia madai ya kukiuka haki za binadamu wakati aliporuhusu operesheni za kijeshi dhidi ya waasi mashariki mwa Congo katika miaka ya 2000.
Mkewe Brenda Kahimbi ameiambia Reuters kwamba, mumewe alipata mshituko wa moyo akiwa nyumbani na kufariki muda mfupi baada ya kufika hospitalini.
Vyanzo viwili vya usalama wa taifa vimesema Kahimbi hivi karibuni alisimamishwa kwa tuhuma za kujaribu kuficha silaha na kuivuruga amani ya nchi.
Comments
Post a Comment