Posts

Showing posts from October, 2019

VIDEO: Takukuru watoa tahadhari Mkoani Dodoma

Image
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, amewatahadharisha wananchi na viongozi wa ngazi mbalimbali katika Mkoa wa Dodoma kuwa makini na vitendo vya utapeli vilivyoibuka vya kutumia jina la Mkuu huyu kutapeli watu TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

Spika Ndugai awasihi Wakenya kujifunza zaidi Kiswahili

Image
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewasihi Wakenya kuongeza juhudi katika kujifunza lugha ya Kiswahili kwani kwa sasa ni moja ya lugha rasmi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kwamba itawasaidia kufanikiwa katika mambo mbalimbali. Ndugai ametoa kauli hiyo nchini Kenya wakati akizindua Kanuni za Kudumu za Bunge la Kenya kwa lugha ya Kiswahili na matangazo ya moja kwa moja ya bunge. “Ukitaka kujifunza lugha fulani ni lazima utumie kamusi ya lugha yenywe, kwahiyo ninawatia moyo muendelee kujifunza Kiswahili kwasababu sasa hivi kinatumika kama alugha mojawapo muhimu na rasmi katika Jumuiya ya SADC, Umoja wa Afrika, Bunge la Afrika lakini pia kwenye Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki kiswahili ni moja ya lugha rasmi inayotumika. “Ili uweze kupata mafanikio ni vizuri ukajua lugha ya kiswahili hata kama ni kile cha kuombea maji, sio vibaya kuzungumza kiingereza lakini ili uweze kufanikiwa katika mambo yako unayoyafanya ni vyema ukajifunza Kiswahili pia,” amese

RC Singida akabidhi Gari kikosi cha Zimamoto na Uokoaji

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wananchi kujiepusha na majanga ya moto yanayotokana na uzembe au makusudi kwa kigezo cha kutegemea uwepo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Dkt. Nchimbi aliyasema hayo wakati akikabidhi gari aina ya‘Land Lover Defender’kwa Jeshi la Zima moto na Uokoji mkoani hapa litakalotumika kwa shughuli mbalimbali za utawala. “Natarajia gari hili liitasaidia kurahisisha majukumu ya kijeshi kwa Jeshi hili, hususan kwenye eneo la utoaji elimu na kujenga maarifa kwa jamii katika kuhakikisha suala la kinga linapewa kipaumbele ili kuepusha maafa na ajali zozote huko mbeleni,” alisema Nchimbi. Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF), Ivo Ombella, alisema gari hilo litatumika kwa shughuli zote za dharula ndani ya jeshi hilo chini ya uratibu wa idaraya utawala. “Ifahamike kuwa Jeshi la Zima moto na Uokoaji linahusika nadharula zote ikiwemo majanga ya moto, tetemeko la ardhi, mafuriko na uzazi isip

Tanzania kuanzisha kituo cha Kimahakama na usuluhishi wa migogoro ya Kimataifa

Image
Tanzania na Taasisi ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) iliyoko chini ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimekubaliana kuandaa mkakati maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo maalum na ya haraka ya msaada wa kisheria kwa Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali (DPP) hususani katika kusimamia mashauri katika mahakama na mabaraza ya usuluhishi ya Tanzania na ya Kimataifa katika maeneo ya madini, biashara na usuluhishi na makampuni ya Kimataifa pamoja na mafuta na gesi. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo mara baada ya majadiliano na Afisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya ushauri wa kisheria ya Afrika (ALSF) Bwana Stephen Karangizi mazungumzo yaliyofanyika katika makao makuu ya Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) Abidjan Nchini Ivory Coast. Prof. Kabudi amesema kuwa lengo la majadiliano hayo ni kuisaidia Tanzania kuweka mikakati kuimarisha sekta ya Sheria ikiwa ni pamoja na kuiongezea uwezo ofisi ya

TANECU yauza tani 13,181 za Korosho

Image
Na. Ahmad Mmow, Newala Chama kikuu cha ushirika cha Tandahimba and Newala Co-operative Union( TANECU) mkoani Mtwara, jana kiliuza korosho za wakulima zenye uzito wa tani 13,181 katika mnada wa kwanza kwa msimu wa 2019\2020 uliofanyika mjini Newala.  Katika mnada huo ambao ulihudhuriwa na kushuhudiwa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa bei ya juu ilikuwa shilingi 2,526 kwa kilo moja huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,468. Taarifa ya makusanyo ya Korosho na kiasi kilichoingizwa katika mnada iliyosomwa na meneja mkuu wa TANECU Ltd ,Mohammed Nassoro  ilibainisha kuwa Korosho zilizouzwa zilikuwa kwenye maghala makuu ya TANECU yaliyopo Newala na Tandahimba na Agrofocus Newala.  Ilieleza kwamba katika ghala la Agrofocus ziliuzwa tani 194, ghala la TANECU Newala ziliuzwa tani 6,303 na ghala la TANECU Tandahimba ziliuzwa tani 6,682. Baada ya kaimu mkurugenzi wa bodi ya korosho Tanzania, Frances Alfred  kutoa taarifa ya bei ya korosho katika soko la Dunia hadi kufikia jana  k

Serikali imeweka mkazo katika sekta ya Michezo - Naibu Waziri Ole Nasha

Image
Na. Ezekiel Mtonyole Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika kuimarisha michezo kama eneo muhimu la mtaala wa mafunzo ya ualimu kutokana na ukweli kwamba michezo inaimarisha stadi za kujifunza, nidhamu na ni ajira pia. Hayo yamesemwa Mkoani Mtwara na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha wakati wa kufunga Mashindano ya Kitaifa ya Michezo na Sanaa kwa Vyuo vya Ualimu Tanzania Bara (UMISAVUTA). Amesema pamoja na kuwepo kwa mchepuo wa michezo katika baadhi ya vyuo vya Ualimu ni vizuri Vyuo hivyo kupitia Ofisi ya Kamishna wa Elimu wakaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ufundishaji na ujifunzaji wa michezo na sanaa unalenga kuwawezesha vijana kufanya vizuri katika eneo hilo kwa maendeleo yao na Taifa. Ametaja Vyuo ambavyo kwa sasa vinatoa mchepuo wa michezo kuwa ni Chuo cha Ualimu Tarime, Butiama, Butiama Mtwara Kawaida na Ilonga na kwamba Wizara itahakikisha kuwa michezo inaimarishwa katika vyuo vyote vya ualimu nchini. Naibu Waziri Ole Nas

VIDEO: Aggrey Mwanri auwasha moto viongozi wa Hospitali hali tete

Image
\ Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri ameutaka uongozi wa hospitali ya wilaya ya ya Uyui ifikapo tarehe kumi November mwaka huu iwe imekamilika ili iweze kutoa huduma ka wananchi. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

MAGAZETI YA LEO 1/11/2019

Image

RC Mtwara atoa neno kwa sekta binafsi kuhusu Miradi ya REA

Image
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa ametoa wito kwa sekta binafsi nchini kujitathmini na kufanya kazi kwa uadilifu ili kuonesha mchango wao katika kujenga nchi, hususan kupitia utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini. Byakanwa alitoa wito huo, wakati akizungumza na Ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Nishati Vijijini (REB), uliomtembelea ofisini kwake, ukiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini mkoani humo. Mkuu huyo wa Mkoa amelazimika kutoa wito huo kutokana na kutoridhishwa kwake na kasi ya mkandarasi anayetekeleza mradi husika mkoani Mtwara, ambaye ni muunganiko (JV) wa kampuni za Radi Services Ltd, Njarita Contractors Ltd & Aguila Contractors Ltd. “Nchi hii haijengwi na watumishi wa umma peke yao; Sekta binafsi nao wana hisa kwenye nchi hii, kwahiyo wasilenge kupata faida tu bali pia waoneshe mchango wao katika kujenga nchi yetu kwa kukamilisha miradi hii kwa wakati na kiwango kinachoendana na thamani ya pesa iliyotolewa,” a

Mo Dewji aeleza mkasa mzima wa kutekwa kwake

Image
Mfanyabiashara Bilionea, Mohammed Dewji amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu sakata lake la kutekwa nyara mwaka jana na namna alivyotishiwa maisha yake. Katika mahojiano na BBC Swahili, Mo ameeleza kuwa kwa kipindi kizima, alihisi kwamba kuna uwezekano mkubwa hatoweza kutoka salama na kuwa mwisho wake wa maisha unakaribia. "Saa 24 za kwanza baada ya kutekwa zilikuwa kama mwezi, imani ndio kitu kikubwa kilichonisaidia katika kipindi kizima. Walinifunga macho, miguu na mikono kwa siku tisa. Tulikuwa hatuongei sana, walikuwa sio watu wa hapa," ameeleza Mo. "Asubuhi walikuwa wananifungua mikono wananifunga mbele, lakini usiku ndio kulikuwa na mitihani walikuwa wananifunga nyuma. Na wakikufunga nyuma maanake huwezi kulala, lazima ulale kulia au kushoto." Mo anasema alikuwa akitoa ushirikiano kwa kila alichotakiwa kufanya. Kikubwa anasema alikuwa akimuomba Mungu atoke salama ambapo siku ya tisa walimsukuma pale Gymkhana na kuondoka zao. Mo Dewji alitekwa Okto

10 wadakwa na Polisi kwa tuhuma mbalimbali jijini Mbeya

Image
Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 10:00 asubuhi huko Kijiji cha Kibisi, Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi waliwakamata 1. Ambokile Mwaisabila (38), 2. Isaya Christopher (28) na 3. Zaina Kasim (26) wote wakazi wa Kibisi wakiwa na Pombe Moshi @ Gongo ujazo wa lita kumi na mbili (12). Watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa Pombe hiyo. Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 11:50 asubuhi huko katika Kitongoji na Kijiji cha Itete – Ndembo, Kata ya Kabula, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Askari Polisi walimkamata Tunu Kijumile (21) mkazi wa Ndembo akiwa anauza pombe haramu [gongo] ujazo wa lita tatu (03) Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa gongo. Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Igawa, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika operesheni maalum walimkamata Damin Mpinga (71), mbena, mkulima, mkazi wa igawa akiwa na gongo ujazo wa lita 10 katika chupa 20 

Ratiba ya robo fainali Carabao Cup hii hapa

Image
Droo ya robo fainali Carabao Cup tayari imefanyika leo Alhamisi Saa 5:45 Asubuhi kwa saa Afrika Mashariki baada ya michezo ya hapo jana. Sasa ni rasmi kuwa Oxford itacheza na Man City, Man United watacheza na Colchester United, Aston Villa watavaana na Liverpool, huku Everton wakipepetana na Leicester. Oxford vs Man City. Man United vs Colchester United. Aston Villa vs Liverpool. Everton vs Leicester.

Taasisi za serikali zatakiwa kuwasilisha taarifa za kesi za madai

Image
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imetoa maelekezo kwa Taasisi zote za Serikali kuhakikisha kwamba, zinawasilisha taarifa zote zinazohusu mashauri ya madai zinazohusiana na taasisi hizo. Mwanasheria Mkuu wa Serikali Profesa Adelardus Kilangi, ameyasema hayo leo jumatano, wakati akifungua mkutano baina yake na Wakurugenzi wa Sheria na Wakuu wa Vitengo vya Huduma za Kisheria kutoka katika Wizara, Mamlaka za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Idara zinazojitegemea, Wakala na Taasisi mbalimbali za Serikali. Zaidi wa wajumbe 300 kutoka taasisi hizo wamehudhuria Mkutano huu ambao ni wa siku mbili, unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango Jijini Dodoma,akiwamo pia Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt.Clement Mashimba (SG). Kwa mujibu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali,taarifa hizo zinatakiwa kuwasilishwa katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali. Profesa Kilangi, amewaeleza washiriki wa mkutano huo kwamba, Ofisi yake imeamua kutoa m

Aliyemuua Mwanamuziki Radio ahukumiwa miaka 14 Jela

Image
Mahakama Kuu nchini Uganda imemuhukumu kifungo cha miaka 14 jela Godfrey Wamala maarufu Troy kwa kosa kumuua mwanamuziki Moses Ssekibogo maarufu Mowzey Radio. Troy alipatikana na hatia siku ya Jumatatu Radio alifariki Februari 1, 2019 baada ya kupigana na Troy wakiwa baa mwaka jana. Godfrey Wamala amekutwa na hatia ya kumuua Moses Sekibogo (Mowzey Radio) bila ya kukusudia. Hukumu hiyo imesomwa licha ya Mwanamuziki huyo kufariki katika ghasia zilizotokea sehemu ya starehe Kesi ilikuwa ikiendeshwa na Jaji Jane Abodo katika Mahakama Kuu Entebbe, Jaji amesema kuwa Godfrey Wamala atatumikia miaka 13, miezi 3 na siku 4 baada ya kukaa mahabusu kwa mwaka mmoja.

Afungwa minyororo chumbani baada ya kupatwa na tatizo la akili

Image
Mkazi wa Old Shinyanga, Manispaa ya Shinyanga, Shadrack Johanes (26) amefungiwa chumbani kwa miezi miwili akiwa amefungwa minyororo miguu na mikono. Shangazi wa kijana huyo, Devota Emmanuel, alieleza kuwa baada ya kuanza kupatwa na tatizo hilo la akili, mpwa wake alianza kupiga watu, kuvunja vioo vya magari na nyumba za watu. Kijana huyo alikutwa kwenye chumba hicho akiwa uchi, hivyo ndugu walilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuwa amepata tatizo la akili. Devotha alisema waliamua kumfungia ndani ili asiendelee kuwatia hasara kwasababu ya kutumia fedha nyingi kuwalipa watu waliokuwa wanaharibiwa nyumba na magari yao na kijana huyo. Alidai kuwa walimpeleka Hospitali ya Rufani ya Bugando jijini Mwanza kupatiwa matibabu, lakini madaktari hawakubaini ugonjwa unaomsumbua, hivyo kuwapa rufani kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili. "Kutokana na hali ngumu ya kimaisha na ukosefu wa fedha, tukaamua kurudi naye hapa nyumbani na kumfungia ndani ili asifanye fujo tena mitaani,&q

VIDEO:Bashe awashushia rungu viongozi wa ushirika

Image
Naibu Waziri wa kilimo Husain Bashe ameagiza viongozi wote wa vyama vya ushirika ambao sio wakulima kuondolewa kwenye nafasi zao, na  kutaka viongozi wa vyama hivyo lazima wawe miongoni mwa wakulima,  aeleza mipango ya Wizara yake walivyopanga kuimarisha vyama vya ushirika hapa nchini na kuhakikisha wakulima wananufaika na jasho lao. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAHU KU SUBSCRIBE

Msemaji wa serikali, Bosi PSSSF watatua kero ya Walimu papo kwa papo

Image
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan Abbasi, jana jioni alilazimika  kumpigia simu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bw. Hoseah Kashimba ili kutatua kero za walimu waliodai kuna wenzao wamestaafu hawajalipwa mafao yao. Tukio hilo lilijitokeza wakati Dkt. Abbasi akijibu hoja za walimu mara baaya ya kuwasilisha mada wakati wa Mkutano ulioandaliwa  na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) mkoani Simiyu na kuhudhuriwa na walimu kutoka mikoa ya Kigoma, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Geita, Mara, Tabora na Kagera Katika mkutano huo walimu walitaka kujua ni lini Serikali italipa pesheni kwa wastaafu ambao hawajalipwa kwa muda mrefu.  Dkt. Abbasi alionesha kushangazwa na hali hiyo kwani aliwaeleza wanasemina hao kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, imeachana na utamaduni wa zamani wa kulimbikiza madeni yasiyo na sababu. Alitoa mfano kuwa licha ya TZS Bilioni zaidi ya 40 zilozotolew

Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga - Mwinyi Zahera

Image
Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa hawezi kuwasikiliza mashabiki wanachokisema kwa sasa baada ya kufungwa na Pyramids FC bali anawasiliana na uongozi ambao ulimpa mkataba. Hayo yamekuja kufuatia mashabiki wa klabu hiyo kutoa malalamiko yao wakimtaka Zahera kuondoka kutokana na matatizo wanayosema yamekithiri kwenye kikosi ikiwemo kushindwa kupanga vizuri kikosi cha kwanza pamoja na mbinu. “Mimi sikuajiriwa na mashabiki wa Yanga bali nilisaini mkataba na viongozi, kwahiyo siku viongozi wakinitaka kiwaachie timu nitafanya hivyo, sitokwenda mazoezini”, amesema Zahera. “Nina uzoefu mkubwa ila hapa Afrika, mashabiki wanakasirika. Hakuna mchezaji yoyote wa Yanga anayeweza kucheza Pyramids FC na lingine ni kwamba wakati tunasajili wachezaji, hatukusajili kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika ila tulisajili kwa ajili ya ligi”, ameongeza. Aidha, Zahera amesema kuwa mashabiki hawapaswi kumlaumu yeye kwa matokeo ya Klabu Bingwa kwani kikosi chake kiliandaliwa kwa ajili ya ligi kuu, a

Pakistani: Treni yawaka moto ikiwa safarini

Image
Habari za hivi punde zinasema kuwa zaidi ya watu 60 wamepoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa vibaya baada ya treni ya abiria kuwaka moto. Afisa wa dharura wa Uokoaji nchini Pakistani, Baqir Hussain amesema moto huo umetokana na mlipuko wa mtungi wa gesi ndani ya treni hiyo hivi leo.

Samuel Eto'o atolea macho kazi ya ukocha

Image
Mwanasoka mashuhuri wa Cameroon Samuel Eto'o amesema yeye ni mwanasoka bora wa muda wote wa Afrika na sasa analenga kupata mafanikio zaidi kama kocha. Eto'o mwenye miaka 38 anafikiria hatua yake inayofuata baada ya kutundika viatu vyake mapema Septemba, na kustaafu soka akiwa na Qatar Sports Club.  Amesema inafika wakati unalazimika kuangalia changamoto nyingine, na ndio alilopanga kufanya. Amecheza mpira wa kulipwa kwa zaidi ya miaka 20 ambapo ameshinda makombe makubwa 18, yakiwemo ya Champions Leagues mawili akiwa na Barcelona na jingine akiwa na Inter Milan. Pia ameshinda Kombe la mataifa ya Afika mara mbili akiwa na Cameroon pamoja na medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 2000. Hata hivyo tuzo ambayo anaitamani na hajaitia mikononi ni ya Ballon d'Or. George Weah wa Liberia anabakia kuwa Mwafrika pekee aliyepata tuzo hiyo mwaka 1995, lakini hilo halijamfanya Eto'o aondoe imani yake kwamba yeye ni mchezaji bora kutoka bara hilo.

Niliowaamini walinikimbia, niliuza gari kumuuguza mwanangu - Munalove

Image
Mwanadada aliyejipatia umaarufu kupitia mitandao wa kijamii wa Instagram, Munalove ambaye mwaka jana alifiwa na mtoto wake wa pekee Patrick baada ya kuugua kwa muda mrefu ameweka wazi story yake tangu kumuuguza hadi mtoto huyo anafariki. Akizungumza, Muna amesema hakuna mtu yeyote aliyemsaidia katika kipindi alichokuwa anamuuguza mtoto wake, hali iliyosababisha kuuza gari ili kupata fedha za kumuuguza. Amesema alipitia wakati mgumu alipokuwa akimuuguza lakini watu wote aliowaamini wamlimkimbia katika kipindi alichowahitaji zaidi. “Watu hawajui nilihangaika kwa kiasi gani kwasababu hawajui hata Patrick alifika vipi hapa gharama gani nililipia lakini wao walikuwa wana kazi ya kunichafua tu kwenye mitandao bila kujua nilichokuwa ninapitia. “Kuna wakati nilitamani hata kujiua au mwanangu aamke awaambie kuwa wanamsingizia mama yangu, wale wote niliokuwa ninawaamini walinikimbia nikabaki peke yangu na nilikataa kuwapa mwili hadi tulipoandikishana wakubali kwamba nilihangaika mwenye

RC Kagera ateketeza zana za uvuvi haramu

Image
Na. Clavery Christian, Kagera Afisa uvuvi Mkoa Kagera, Bw, Gabrieli Mgaene amesema kuwa zana za uvuvi haramu zenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 zimekamatwa katika msako ulifanywa na kikosi cha kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa victoria na kufanikiwa kukamata Mitego ya kuvulia samaki aina ya makokoro 197 na nyavu zenye macho madogo ambayo hayafiki inchi 6 zinazo ruhusiwa kisheria 19,620 na nyavu za dabo ambazo zina macho zaidi ya ishirini na sita 1.200 na monofilamenti neti 1,880 na nyavu za dagaa zenye macho madogo chini ya milimita 8/40 zimeteketezwa kwa moto baada ya mahakama kudhibitisha kuwa ni zana haramu na ziteketezwe kwa mujibu wa sheria. Awali akiongea na wananchi wa kata ya miembeni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen Marco E Gaguti amewataka wananchi katika mwalo wa Nyamkazi wilayani Bukoba katika mkutano wa hadhara na wavuvi  amesema kuwa mkoa Kagera ni miongoni mwa mikoa mitano hapa nchini ambayo iko chini katika kuchangia pato la taifa na wakati mkoa wa Kagera una

DC Ngubiagai kula sahani moja na viongozi wa AMCOS

Image
Na Ahmad Mmow-Lindi Katika kuhakikisha wakulima waliopo wilayani Kilwa hawadhulumiwi. Mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai amesema atafuatilia kwa karibu mchakato wa uuzaji na ununuzi wa mazao ya kilimo ya wakulima katika vyama vya msingi vya ushirika( AMCOS) vilivyopo wilayani humo. Jana akizungumza na Muungwana Blog katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko baada ya kukamilika zoezi la kuwalipa wakulima wa ufuta katika vijiji vya Nanjirinji na Zinga ambao walikuwa hawajalipwa kutokana na fedha zao kuibwa na viongozi na watendaji wa AMCOS, alisema kuanzia sasa atakuwa anafutilia kwakaribu zaidi mchakato wa ununuzi na uuzaji wa mazao ya kilimo kwenye AMCOS zote zilizopo wilayani Kilwa. Ngubiagai ambaye alianza kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa agizo lake kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa( TAKUKURU) kuhusu fedha za wakulima wa ufuta zilizoibwa na viongozi wa AMCOS kutoa matokeo chanya kwa kipindi kifupi alisema hatasubiri kupelekewa taarifa akiwa ofisini.

Mtoto mlemavu atelekezwa na wazazi, walezi waomba msaada

Image
Na George Bahemu Ngara-Kagera Mtoto mlemavu ambaye ana umri wa miaka nane atelekezwa na wazazi wake kutokana na ulemavu wake katika kijiji Cha Mhweza katani Mabawe wilayani Ngara mkoani Kagera. Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema mtoto huyo alizaliwa akiwa mzima muda ulipofika wa kutembea na kutambaa haikuwezekana kutokana na ulemavu wake. Wakizungumza na Muungwana Blog wamesema kuwa mtoto Mama yake baada yakuona nimlemavu alimuacha kwa Bibi yake nakwenda kuolewa wilayani humo. Renatha ambaye ni jirani na Neema amesema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa sawa na muda wakutambaa na kutembea haikuwezekana na hospitali hawakufanikiwa kuona tatizo la mtoto huyo. "Huyu mtoto alizaliwa mwaka 2011 lakini mpaka sasa hatembei wala kusimama yeye ni wakulala tu na Mama yake baada ya kuona ni mlemavu alimkana na matumizi hatoi hata mia." Amesema Renatha Japheth Emily ni mjomba wake Neema amesema kuwa hajafurahishwa na kitendo alichokifanya Mama yake kwenda kuolewa nakuacha m