Posts

Showing posts from October, 2020

MAGAZETI YA LEO 14.10.2020

Image
 

Belarus yatishia kutumia risasi za moto dhidi ya waandamanaji

Image
  Mamlaka nchini Belarus jana zimetishia kutumia risasi za moto kuvunja maandamano dhidi ya rais Alexander Lukashenko huku mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wakikubaliana kumwekea vikwazo kiongozi huyo. Akizungumza kwa njia ya video naibu waziri wa mambo ya ndani wa Belarus , Gennady Kazakevich amesema serikali haitowaondoa askari mitaani na iwapo maandamano hayatositishwa wanaweza kutumia risasi za moto . Onyo hilo limetolewa baada ya vikosi vya serikali kutawanya kwa nguvu siku ya Jumapili maandamano ya kumpinga rais Lukashenko, hatua iliochochea Umoja wa Ulaya kufikia uamuzi wa kumwekea Lukashenko vikwazo. Matumizi ya risasi za moto itakuwa ni hatua ya karibuni kabisa inayoonesha kuongezeka mvutano tangu raia wa Belarus walipoingia mitaani kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Agosti na mateso wanayopitia mahabusu.

SHULE YA MSINGI CHIPOLE SONGEA INAWATANGAZIA NAFASI ZA MASOMO

Image
Uongozi wa Shule ya msingi Chipole unawatangazia nafasi za kujiunga na masomo kwa Darasa la  awali, i, ii, iii,  v na vi  kwa mwaka 2020 / 2021. Chipole Primary School ni shule  ya bweni kwa wasichana na wavulana. inawalea watoto kimwili na kiroho,  inafanya vizuri kitaaluma katika mitihani ya ndani, kata, wilaya, mkoa na kitaifa, Shule ipo  Wilaya ya Songea   kataya Magagura Mkoani Ruvuma. Shule ina mandhari nzuri ya kuvutia na tulivu  inayo muwezesha mwanafunzi kujifunza na kufanya vizuri katika taaluma shule ina walimu wa kutosha  wenye  sifa thabiti za kitaaluma katika masomo yote. Standard four national assessment (sfna) -2019 results chipole primary  school   -ps1603003 waliosajiliwa : 29. waliofanya mtihani: 29.  wastani wa shule: 287.1379 kundi la shule: watahiniwa pungufu ya 40 nafasi ya shule kwenye kundi lake katika halmashauri / manispaa:  2 kati ya 18 nafasi ya shule kwenye kundi lake kimkoa: 2 kati ya 170 nafasi ya shule kwenye kundi lake kitaifa: 57 kati ya 3244

Rais wa TFF aunda kamati ya ushindi ya Taifa Stars

Image
 

Winga wa Yanga kuanza majukumu yake Novemba

Image
  WINGA Saidi Ntibazonkiza anayekipiga timu ya Taifa ya Burundi ambaye amesaini dili la mwaka mmoja na nusu ndani ya Klabu ya Yanga ataanza kutumika rasmi Novemba 15. Kwa mujibu wa Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa sababu kubwa ya kuanza kutumika Novemba 15 ni kutokana na kutimiza majuku ya timu yake ya Taifa ya Burundi. Said alikuwa miongoni mwa wachezaji waliocheza Oktoba 11 Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Injinia Hersi amesema:"Ataanza kuutumikia mkataba wake tarehe 15 Novemba 2020 na ni mkataba wa mwaka mmoja na nusu. "Ataripoti kuitumikia klabu baada ya kumaliza majukumu ya timu ya taifa nchi yake inatarajiwa kucheza mechi ya pili tarehe 15 Novemba. "Hivyo atakuwa ndani ya timu kwa nusu ya msimu huu na msimu ujao atakuwa msimu kamili na atamaliza kabisa kuitumikia timu ya Yanga," amesema.

Poland na Ukraine zatoa wito kwa Urusi kuhusu Crimea

Image
Rais wa Poland Andrzej Duda na Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky, wameitaka Urusi ikomeshe harakati zake za kutaka kujumuisha Crimea kama eneo lake kinyume cha sheria. Kulingana na maelezo yaliyotolewa na ofisi ya rais wa Ukraine,  marais hao wawili walitoa wito kwa Urusi isitishe utekaji wa Crimea. Duda, alibainisha kuunga mkono mipaka ya Poland na Ukraine, na kuweka msisitizo kuwa maeneo ya Donbas na Crimea yanapaswa kurejeshwa kwa Ukraine. Duda pia alifahamisha kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinapaswa kuendelea hadi itakapositisha utekaji wa maeneo kinyume cha sheria, huku Zelensky akitoa shukrani kwa ushirikiano wa Poland katika suala la nchi yake na mwelekeo wa NATO. Wakati huo huo, mazungumzo ya mkutano pia yalisisitiza umuhimu wa kulinda haki za jamii zilizokuwa na uchache katika nchi ya Ukraine na Poland.

Mgombea udiwani kata ya Tandale aahidi Kujenga secondari ya Kata

Image
  Mgombea udiwani kata ya Tandale jimbo la kinondoni halmashauri ya wilaya ya kinondoni mkoani dar-es-salaam Kupitia chama cha ccm ndugu  Abdallah Azizi Saidi (Chief) ameahidi Kujenga shule ya secondary ya Kata.  Aliyasema Hayo Jana wilayani kinondoni alipokuwa Akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo ya Tandale kupitia mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Tandale wilayani kinondoni Mbele ya Mgombea Ubunge Wa jimbo hilo la kinondoni Ndugu Abassi Tarimba. Aidha Mgombea Huyo   amesema kuwa Atahakikisha Anatanua kituo cha Afya cha tandale,Atatoa Mikopo Isiyo na riba kubwa kwa kina mama,Atatoa Bima Za afya kwa watoto na kina mama,Atatoa msaada Wa kisheria pamoja na kusimamia ulinzi na usalama Wa Kata hiyo ya Tandale.

Mikutano ya kampeni za mgombea Ubunge -Ludewa yatoa majibu ya kero ya Barabara iliyodumu kwa muda mrefu

Image
  Na Amiri Kikagalila, Njombe. Mbunge wa Jimbo la Ludewa  aliyepita bila kupingwa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) wakili Msomi Joseph Kamonga ameendelea na mikutano ya kampeni za Kumuombea kura Rais Dkt John Pombe Magufuli na madiwani wa CCM ikiwa zimebaki Siku 16 kuelekea Kufanyika kwa Uchaguzi mkuu nchini Tanzania hapo Oktoba 28, 2020. Kamonga akiwa katika kata ya Madilu wilayani Ludewa amewashukuru Wananchi wa eneo hilo kwa kukiamini Chama cha Mapinduzi na kumpitisha yeye  bila kupingwa kuwa mbunge wa jimbo la Ludewa na amewaahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabiri ikiwemo swala la Barabara. ''Ndugu zangu nimekuja kusema Asante sana,Jambo la pili nimekuja kuwaombea kura viongozi wa CCM, Tumekuja kumuombea kura Rais wetu Mpendwa Dkt,John Pombe Magufuli,tunamuombea kura Magufuli kwa ujasiri kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwenye taifa letu ni Rais wa kipekee mfano pekee mwaka jana aliweka utaratibu wa Kusikiliza Changamoto za wafanyabishara mbalimbali n

Naibu kamishna wa uhifdhi utalii na huduma za biashara atembelea vituo vinavyosimamiwa na TAWA Mkoani Tabora

Image
NA FARIDA SAIDY. Naibu Kamishna Bw.Imani Nkuwi amefanya ziara ya kikazi katika vituo vilivyo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) vilivyopo Mkoani Tabora na kuzungumza na watumishi wa vituo vya Kanda Dhidi ya Ujangili ya Magharibi (KDU), Pori la Akiba la Ugalla, Pori la Akiba Luganzo Tongwe, na  Pori la Akiba Wembere Ziara  hiyo iliyofanyika tarehe 12.10.2020 pamoja na mambo mengine Naibu Kamishna Nkuwi alitoa ufafanuzi kwa watumishi hao kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika Shirika pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakibili watumishi kwenye vituo vyao. Aidha, alitumia vikao hivyo kuwahimiza watumishi kufanya kazi kwa uzalendo, ueledi na kudumisha upendo miongoni mwao ili kuiwezesha TAWA kufikia malengo yake,huku akisisitiza kuzingatia Tunu za TAWA zilizoanishwa katika mpango kazi wao. Naibu Kamishna Nkuwi alitoa ufafanuzi kwa watumishi kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na Serikali katika Taasisi za Uhifadhi zilizopo chini

Trump arejea kwenye kampeni baada ya kupona COVID-19

Image
Rais Donald Trump wa Marekani amerejea tena kwenye kampeni za uchaguzi mkuu kwa kufanya mkutano wa kwanza jimboni Florida siku kadhaa tangu alipogundulika na maambukizi ya virusi vya corona. Rais Trump aliwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la wazi huko Sanford; Florida bila ya kuvaa barakoa. Mkutano wa kampeni mjini Florida,  jimbo ambalo ni muhimu kwa Trump kushinda, unafungua njia ya mikutano zaidi iliyopangwa kufanyika wiki hii kwenye majimbo ya Pennsylvania, Iowa na North Carolina.  Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliosimama bega kwa bega wengi wakiwa bila barakoa, Trump amesema afya yake imeimarika na yuko huru kukutana tena na wapiga kura bila ya kuwa na wasiwasi wowote.  "Nimetiwa nguvu kwa maombi yenu na nimefarijika kwa uungaji wenu mkono. Tunaungwa mkono vya kutosha. Na tuko hapa lakini tunaenda kukamilisha, tutalifanya taifa hili kuwa kubwa kuliko ilivyokuwa hapo kabla." alisema rais Trump. Trump anayewania muhula wa pili katika uchaguzi w

Tetesi za soka kimataifa

Image
Manchester United imeweka mipango ya kumsainisha kiungo wa Rennes na Ufaransa Eduardo Camavinga, 17, iwapo mfaransa mwenzie Paul Pogba, 27, ataamua kuondoka Old Trafford. (Sport Witness) Uhamisho wa mshambuliaji wa Algeria Said Benrahma wa £25m kutoka Brentford kwenda West Ham uko hatarini kuvunjika, ambapo wapiga nyundo hao wamejielekeza zaidi kwa mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28. Crystal Palace huenda ikapeleka ofa ya lala salama kumnasa Benrahma, 25. (Mirror) Manchester City itajaribu tena kumsajili mlinzi wa kushoto wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico, 28, mwezi January. (Sun) Tottenham huenda ikarejesha nia yake ya kumsajili mlinzi wa kati wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 25, mwezi January. (Team Talk) Fulham wako katika hatua nzuri ya mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Huddersfield na Uholanzi Terence Kongolo, 26. (Football Insider) Wachezaji kadhaa wa Manchester United wameeleza masikitiko yao ya namna hali inavyomwendea mlinda mlango w

MAGAZETI YA LEO 13/10/2020

Image