Posts

Showing posts from August, 2020

Kikosi cha Simba kuanza safari kuelekea Mbeya kuifuata Ihefu FC

Image
 KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji, leo Septemba Mosi kinatarajiwa kuanza safari kuelekea Mbeya kuifuata Ihefu FC. Simba iliweka ngome mkoani Arusha tangu Agosti 28 ambapo ilitia timu siku ya Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Ngao ya Jamii uliochezwa Agosti 30,Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.  Kwenye mchezo huo ambao ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara,  Simba ilishinda mabao 2-0 yaliyofungwa ba John Bocco dk ya 7 na Bernard Morrison dk ya 60. Wanaanza safari ya kutetea taji la Ligi Kuu Bara kwa kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Ihefu Septemba 6 Uwanja wa Sokoine majira ya saa 10:00 jioni. Huu unakuwa mchezo wa kwanza kwa timu zote ndani ya msimu mpya wa 2020/21 huku Ihefu ikiwa ni msimu wake wa kwanza pia  kushiriki Ligi Kuu Bara baada ya kupanda kutoka Ligi Daraja la Kwanza.

Alichosema Wakazi kutetea wasanii chipukizi

Image
  Wakazi ambaye ni Mgombea Ubunge Jimbo la Ukonga kwa tiketi ya ACT-Wazalendo amesema Serikali ya Tanzania haipo katika kukuza ubunifu kutokana na Sheria ya Maudhui iliyopitishwa. Wakazi amesema kumtaka msanii ambaye amefanya ubunifu kuwa na Laki tano ili kuiweka kazi yake YouTube itafanya wabunifu wadogo kushindwa au kuonekana wahalifu kwa kukiuka sheria. Wakazi ametambua umuhimu wa uwepo wa Sera ya Sanaa na Wasanii ili kuwaweka wasanii katika mazingira mazuri na kukuza ubunifu. Wakazi ameyasema haya leo wakati wa uzinduzi wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha ACT-Wazalendo.

Kocha mpya wa Barcelona aanza mazoezi bila Messi

Image
  RONALD Koeman, Kocha Mkuu wa Klabu ya Barcelona jana Agosti 31 alianza kukinoa kikosi chake kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2020/21 bila ya uwepo wa nyota wao Lionel Messi. Baada ya kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Quique Setien, Koeman alikabidhiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho ambacho kilitoka kupokea kichapo cha udhalilishaji cha mabao 8-2 mbele ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.  Picha ambazo zilipigwa na kuwachukua wachezaji ambao walikuwa wameanza mazoezi zilimuonyesha kocha huyo akiwa na baadhi ya wachezaji ambao wanajiandaa na kuanza kwa La Liga huku Messi akiwa hayupo. Wachezaji wa Barcelona walipigwa picha wakiwa mazoezini ambapo winga Ousmane Demebele alionekana akikimbia huku akitumia vifaa vipya vya mazoezi vya timu hiyo.  Pia, Gerard Pique alionekana akiwa na mpira akichezea kwenye mazoezi hayo ambayo yalifanyika bila ya uwepo wa Messi ambaye inaelezwa kuwa anahitaji kuondoka ndani ya timu hiyo na inatajwa kuwa anahitaji

Sugu afunguka haya baada ya kufikisha mwaka mmoja wa ndoa yake

Image
 Mbunge wa Mbeya Mjini anayemaliza muda wake, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ametimiza mwaka mmoja wa ndoa yake.  Sugu alifungua ndoa Jumamosi ya Agosti 31, 2019 na mpenzi wake Happiness Msonga katika Kanisa Katoliki Ruanda Parokia ya Roho Mtakatifu, Mbeya. “LEO ni mwaka mmoja wa NDOA yetu, NAMSHUKURU sana MUNGU kwa MAISHA yetu. Pia nakushukuru wewe MKE wangu MPENZI kwa kuniongezea FURAHA na KUBADILISHA maisha YANGU, with YOU my LIFE makes more SENSE now…LOVE ALWAYS ,” ameandika Sugu kwenye ukurasa wake wa #Instagram. Sugu na mkewe wamebahatika kupata mtoto wa kiume waliempa jina la 'Shawn' Joseph Mbilinyi.

Trump atetea wafuasi wake kuhusu makabiliano makali yaliyotokea Portland

Image
  Rais wa Marekani Donald Trump ametetea wafuasi wake kwa madai ya mchango wao kwenye makabiliano yaliyotokea hivi karibuni. Amesema kwamba kijana anayeshutumiwa kwa mauaji ya watu wawili huko Wisconsin wiki iliyopita na wafuasi wa Trump walioshiriki makabiliano Oregon Jumamosi, walichukua hatua hiyo kujitetea. Bwana Trump aliongeza kwamba mpinzani mwenzake wa chama cha Democratic Joe Biden hajawapinga wanaharakati wa mrengo wa kushoto wanaoshutumiwa kwa kusababisha vurugu. Bwana Biden anaongoza kwenye kura ya maoni kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Novemba. Jumatatu akiwa Ikulu ya Marekani wakati anafanya mkutano na wanahabari, Bwana Trump alimlaumu Bwana Biden na washirika wake kwa vurugu zilizotokea kwenye jimbo ambalo meya na gavana ni wa chama cha Democratic. Mwanahabari wa CNN alimuuliza rais ambaye anatoka chama cha Republican ikiwa atashutumu wafuasi wake ambao walifyatua risasi wakati wa makabiliano na waandamanaji wengine yaliyotokea mwishoni mwa juma

Tetesi za soka kimataifa

Image
 Lionel Messi ataondoka Barcelona msimu hii na '' inawezekana'' akaelekea Manchester City, kwa mujibu wa mgombea wa urais wa klabu hiyo, Toni Freixa. (Goal) Barcelona inaamini kwamba njia pekee ya mshambuliaji huyo wa Argentina, 33, kuondoka kihalali bure ni ikiwa ataahidi kwamba hatashiriki katika michuano ya msimu ujao.(ESPN) Rais wa Argentina, Alberto Fernandez, amemshauri Messi kurejea katika klabu yake ya ujana ya Newell's Old Boys. (C5N, via Evening Standard) Chelsea imekubali kumsajili kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Kai Havertz, 21, kwa kima cha kwanza cha pauni milioni 72, na kusababisha pesa za matumizi yao kipindi cha uhamisho kuongezeka hadi pauni milioni 200. (Guardian) Manchester United inamlenga mlinzi wa RB Leipzig raia wa Ufaransa Dayot Upamecano, 21. (ESPN) Kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, 24, anasemekana kwamba wiki hii atajiunga na Arsenal kwa mkopo kutoka Real Madrid. (Guardian) Vilabu vya Saudi Arabia na Qatar v

Macron aishinikiza Lebanon kuunda haraka serikali mpya

Image
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amerejea Lebanon, nchi ambayo ipo katikati ya mgogoro usio wa kawaida, kwa ziara ya siku mbili iliyosheheni shughuli nyingi na mazungumzo ya kisiasa yanayolenga kuipa ufumbuzi nchi hiyo Macron alitua jana usiku mjini Beirut lakini mkutano wake wa kwanza haukuwa na waziri mkuu mpya aliyeteuliwa saa chache kabla, wala wanasiasa wanaozozana wa nchi hiyo au wanaharakati wa mashirika ya kijamii. Macron badala yake aliamua kumuona mwanamuziki nambari moja wa kike nchini Lebanon, Fairouz, ambaye ni alama ya kitaifa na mmoja wa vigogo wa nadra sana nchini Lebanon wanaopendwa na kuheshimiwa kote nchini humo. Mwanamuziki huyo maarufu katika ulimwengu wa Kiarabu, sasa ana umri wa miaka 86 na hajaonekana hadharani katika miaka ya karibuni. Mkutano na Fairouz ni ishara ya kibinafsi ya Macron. Kisha akakutana na waziri mkuu wa zamani Saad Hariri katika makazi ya balozi wa Ufaransa. Akizungumza katika uwanja wa ndege wa Beirut, Macron alitoa wito wa kuundwa harak

MAGAZETI YA LEO 1/9/2020

Image

Rwanda yaitaka Ufaransa kumkamata mshukiwa wa mauaji ya kimbari

Image
Rwanda imeitaka Ufaransa kumkamata Aloys Niwiragabo anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994. Mtuhumiwa huyo alikuwa kanali wa jeshi, aliyehusika na upelelezi katika enzi za utawala wa hayati Juvenal Habyarimana. Mwendesha mashitaka mkuu wa Rwanda Aimable Havugiyaremye ametangaza kwamba Rwanda tayari imetoa waranti wa kutaka Kanali Aloys Ntiwiragabo akamatwe. ‘’Kwa sasa tunafanya kazi kwa ushirikiano na kundi la wapelelezi wa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Ufaransa.Wapepelezi hao tayari wameishaanza uchunguzi wao na kazi inaenda kama ilivyopangwa.’’ Kwa mjibu wa mwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda Bw. Ntiwiragabo, anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari japo hakutoa maelezo zaidi. Kanali Aloys Ntiwiragabo mwenye umri wa miaka 72 alikuwa mkuu wa idara ya upelelezi wa jeshi wakati wa utawala wa hayati Juvenal Habyarimana. Kanali huyo alikuwa miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi la hayati Juvenal Habyarimana, lakini hayupo kwenye orodha ya watuhu

U.N. yasema maisha ya mshindi wa tuzo ya Nobel DR-Congo yako hatarini

Image
Dkt Denis Mukwege, Mashindi wa Tuzo ya Amani ya Noble 2018Image caption: Dkt Denis Mukwege, Mashindi wa Tuzo ya Amani ya Noble 2018 Umoja wa Maitaifa umeonya kuwa maisha ya daktari wa Dr-Congo aliyeshinda Tuzo ya Nobel 2018 yako hatarini baada ya kupokea msururu wa vitisho vya mauaji vinavyotolewa dhidi yake. Kamishena wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amelaani vitisho hivyo na kutoa wito Dkt. Denis Mukwege na familia yake kupewa ulinzi. Bachelet pia amezishinikiza mamlaka nchini DRC kuidhinisha rasimu ya sheria ya ulinzi inayodhibiti shughuli za wanaharakati wa kutetea haki za binadamu "kwa kuzingatia viwango vya kimataifa." Wiki iliyopita Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi aliamuru Bw. Mukwege mwenye umri wa miaka 65 kupewa ulinzi wakati uchunguzi wa tisho la mauaji dhidi yake ukiendelea.wenzakeImage caption: Dkt Denis Mukwege (Aliyevalia miwani) akiwa na madaktari wenzake Denis Mukwege ni daktari anayeshughulikia afya ya wanawake nchini D

“Mamba ana nyama tamu anzeni kula” Naibu Waziri

Image
  “Mamba ana nyama tamu sana, anzeni kula nyama yake badala ya kutegemea kitoweo cha samaki pekee” ni kauli ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu Amesema kuwa licha ya nyama hiyo kuwa tamu, lakini kwanza mvunaji wa mamba aombe kibali kutoka kwa maofisa wanyamapori cha kuwavuna kinachotolewa kila Julai Mosi. “Kuacha nyama yake kuwa tamu, lakini pia ngozi yake ni biashara yenye tija ndani na nje ya nchi” Kanyasu ameeleza kuwa Serikali ina mpango wa kufungua mabucha yatakayouza nyama za wanyamapori katika maeneo mbalimbali nchini. “Wizara imeanzisha utaratibu wa uwindaji wa ndani (resident hunting) ambapo nyama zitakazo kuwa zikipatikana zitakuwa zikiuzwa kwenye mabucha hayo,” Kanyasu “Hivyo wawindaji watatakiwa kufuata taratibu za kuomba vibali kwa ajili ya kuwinda ambavyo vitaainisha aina ya wanyama ambao watakwenda kuwawinda” Kanyasu

Poul Makonda apata watoto mapacha "katikati ya machozi umenipatia zawadi tena"

Image
Aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda amebahatika kwa mara nyingine watoto ambao ni mapacha wa kiumbve.  Taarifa hiyo imethibitisha kupitia ukurasa wake wa instagram ambapo ameandika hivi; Heshima na Mamlaka ni zako eee Mungu wa Mbingu na Nchi na kwako wewe tunalia Aba, nitaendelea kutaja ukuu wako siku zote za maisha yangu kwakua hujawahi kuniacha hata dakika moja. Pamoja na mapito magumu na mazito lakini naiona nuru yako huku nikisikia sauti ya ROHO mtakatifu ikisema mwanangu Paul Christian Makonda nalikujua kabla sijakuumba na nikakutenga kwa kusudi langu usikubali TAA iwakayo ndani yako ikazimika. Ona sasa unavyozidi kuniheshimisha katikati ya machozi umenipatia zawadi tena itokayo kwako. Mimi nilieitwa tasa ulinipa mtoto KEAGAN ambaye alishangaza ulimwengu kwa ujio wake:Ukaona haitoshi LEO umenipa DOUBLE PORTION:Leo Mungu wangu umenipa MAPACHA tena wa KIUME na Wa KIKE hii yote ni kutangaza UKUU wako maishani mwangu. Kwa wale ambao bado hawajakuamini na w

TDL Yajizatiti kukuza sekta ya kilimo cha zabibu nchini

Image
Kampuni  ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), imeeleza dhamira yake ya kuendeleza kilimo cha zabibu mkoani Dodoma pamoja na matarajio yake ya kuingia mikataba ya kununua zabibu moja kwa moja kutoka kwa wakulima wadogo. Mchango wa TDL wa sera yake ya kununua malighafi nchini  na dhamira ya kukuza sekta ya kilimo cha zabibu inaenda sambamba na jitihada za  serikali za kuboresha maisha ya wakulima wadogo na kukuza uchumi wa Tanzania. TDL inaamini jitihada za Serikali za kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda zinaweza kufanikiwa  ikiwa wakulima wadogo wanawezeshwa kuzalisha malighafi inayohitajiwa na viwanda. Meneja Mkuu wa TDL, Devis Deogratius, alisema kampuni hiyo kwa sasa inanunua takribani lita milioni 1.2 za mchuzi wa zabibu kwa mwaka kutoka kampuni za CETAWICO na UWAZAMAM, ambazo zinanunua zabibu za wakulima wa ndani  ambapo  inatumia bilioni 3.3 kwa mwaka. Deogratius aliongeza kusema kuwa imedhamiria kununua malighafi ya ndani katika kipindi chote cha miaka ijayo ambapo k

Dirisha la usajili linafungwa leo

Image
 LEO Agosti 31 ni siku ya mwisho kwa timu kukamilisha masuala ya usajili kwa wachezaji wao itakapofika saa 5:59 ukurasa wa usajili unafungwa rasmi. Sokoni kila timu inapambana kwa masuala ya usajili na tunaona kwamba bado zipo timu ambazo hazijatambulisha wachezaji wao ina maana kwamba bado wapo sokoni kusaka aina ya wachezaji wanaowahitaji. Pia zipo ambazo zimeshamaliza masuala ya usajili baada ya kuwatambulisha wachezaji pamoja na benchi la ufundi wanastahili pongezi kwa kuwa wameonyesha  walijipanga na wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya. Msimu mpya unatarajiwa kuanza Septemba 6, siku zinakwenda kasi hivyo kwa wale ambao wanadhani ni muda mrefu umebeki wanapaswa washtuke mapema. Azam, Simba na Namungo hizi hapa tayari zimekamilisha masuala ya usajili na wachezaji wanaendelea na kambi kwa pamoja wakiwa wameshamaliza majukumu yao ya usajili. Kagera Sugar nao pia wamekamilisha usajili wao kwa kuboresha kikosi chao na kuwapa taarifa mapema wachezaji ambao hawatakuwa ndani ya kikos

Mwanadiplomasia mkuu wa China apuuzilia mbali wasiwasi wa Ulaya kuhusu haki

Image
  Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China Wang Yi amezitetea kambi za kuwazuia watu katika jimbo la Xhinjiang na sheria mpya ya usalama ya Hong Kong akipuuzilia mbali wasiwasi wa nchi za Ulaya kuhusu haki za binaadamu na kuonya kuhusu uingiliaji wa masuala ya China.  Akizungumza mjini Paris jana, Wang alisisitiza madai kuwa wale wote waliotumwa katika vituo hivyo vya kutoa mafunzo jimboni Xhinjiang wameachiwa huru na kupewa ajira - hata wakati makundi ya haki za binaadamu na familia wakiripoti kuhusu kuendelea kuzuiliwa kwa Waislamu wa jamii ya Waighur na kupotea kwa mawasiliano na wapendwa wao.  Kuhusu sheria ya usalama Hong Kong alisema ilibidi wachukue jukumu la kusitisha vurugu kisiwani humo kwa kuweka sheria ya kudumisha usalama wa taifa.  Waziri huyo yupo kwenye ziara yake ya kwanza ya Ulaya tangu janga la virusi vya corona lilipozuka akitafuta kufufua biashara na mahusiano yaliyoharibiwa na mgogoro wa kiafya na kiuchumi ulimwenguni.

Mama wa miaka 42 mbaroni kwa tuhuma za kubaka

Image
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 42 anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini Kenya kwa tuhuma za kumbaka mvulana anayesoma darasa la nane na kumrubuni amuoe. Mtuhumiwa huyo alikutwa nyumbani kwake katika eneo la Nyamaraga, Kaunti ya Suna akiwa na mtoto huyo mwenye umri wa miaka 14, Jumamosi iliyopita. Kiongozi Msaidizi wa eneo la Suna, Evance Nyarube alisema kuwa alipata taarifa kutoka kwa majirani wakilalamika kuhusu uhusiano wa kimapenzi yasiyozingatia umri sahihi. Citizen wamemkariri Nyarube akieleza kuwa wazazi wa mvulana huyo wamewahi kuonya kuhusu uhusiano huo lakini maombi yao yalikutana na sikio la kufa. Alieleza kuwa uhusiano huo ni sawa na ubakaji au unyanyasaji wa kingono, hivyo mtuhumiwa atachukuliwa hatua za kisheria. Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama ya Migori, kesho, Agosti 30, 2020. Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Kingono nchini humo, mtu atakayekutwa na hatia ya kufanya ngono na mtoto wa kati miaka 12 hadi 15 anaweza kukabiliwa kifungo kis

Ufungaji wa mafunzo ya ndoa mkupuo wa sita wafanyika Zanzibar

Image
 Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Ndoa waliohudhuria katika hafla ya Ufungaji wa Mafunzo ya Ndoa Mkupuo wa Sita iliofanyika katika Ukumbi wa Masjid Zinjibar Kiembe Samaki Zanzibar. Msomaji wa Kur-ani Afrika Mashariki Rajab Ayoub akisoma   katika hafla ya Ufungaji wa Mafunzo ya Ndoa Mkupuo wa Sita iliofanyika katika Ukumbi wa Masjid Zinjibar Kiembe Samaki Zanzibar.  Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Maalim akimkabidhi Cheti  cha Ushiriki wa Mafunzo ya Ndoa Mwanafunzi Aboud Iddi Mahmoud katika hafla ya Ufungaji wa Mafunzo ya Ndoa Mkupuo wa Sita iliofanyika katika Ukumbi wa Masjid Zinjibar Kiembe Samaki Zanzibar.  -Waziri wa Katiba na Sheria Khamis Juma Maalim akimkabidhi Cheti  cha Ushiriki wa Mafunzo ya Ndoa Mwanafunzi Afia Ali Mohamed  katika hafla ya Ufungaji wa Mafunzo ya Ndoa Mkupuo wa Sita iliofanyika katika Ukumbi wa Masjid Zinjibar Kiembe Samaki Zanzibar.   

Tembo 12 wafa katika mazingira ya kutatanisha Zimbabwe

Image
Mamalaka ya hifadhi ya wanyama nchini Zimbabwe zinachunguza jinsi tembo 12 walivyokufa katika mbuga ya kitaifa ya Hwange. Tembo hao walipatikana wakiwa wamekufa wakiwa na pembe zao. Mamlaka zinasema hazina hofu kwamba huenda wametiliwa sumu ya cyanide - ambayo pia hutumiwa na wawindaji haramu badala ya silaha- kwani hakuna wanyama wengine walioathirika Sampuli ya damu imechukuliwa kutoka kwa tembo hao kuchunguza kilichosababisha vifo vyao. Mbuga ya kitaifa ya Hwange National inakaribia mpaka wa Botswana ambako mamia ya mizoga ya tembo ilipatikana mwaka huu.

Rais wa Afrika Kusini kuchunguzwa kuhusiana na mchango wa kampeini

Image
Rais wa Afrika Kusini Cyril RamaphosaImage caption: Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Maafisa wa chama tawala nchini Afrika Kusini wamesema Rais Cyril Ramaphosa atafika mbele ya Tume ya Uadilifu kujibu maswali kuhusiana na mchago tata wa kampeini. Lakini Jessie Duarte, mwanachama wa ngazi ya juu wa chama cha African National Congress, ANC, hakufafanua ikiwa Bwana Ramaphosa atajiwasilisha mwenyewe mbele ya kamati hiyo ya chama Katika ripoti yake, mamalaka ya kupambana na ufisadi inadai kuwa Bw Ramaphosa alipotosha bunge kuhusumchango aliopokea mwaka 2017, ya thamani ya zaidi ya dola 35,955.

Killy na Cheed waangukia kwa Harmonize

Image
Wasanii waliotoka kwenye lebo ya Kings Music Records ambayo inamilikiwa na msanii Alikiba, Official Killy Tz na Official Cheed wameonekana kuwa upande wa msanii Harmonize baada kuonyesha kumpa sapoti msanii huyo. Hali hiyo imekuja baada ya Killy na Cheed kupost matukio ambayo anayafanya Harmonize kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram, huku watu wakiwatarajia huenda wao ndiyo wakawa wasanii wapya wa lebo ya Konde Gang. Ukifuatilia tukio la Harmonize kwenye kilele cha siku ya Wananchi Uwanja wa Benjamin William Mkapa, msanii Killy alimpost Harmonize akiwa amevaa mavazi ya kijeshi kisha kuandika "Mmakonde mmoja". Pia ukifuatilia post yao ya mwisho kabla ya hiyo ya jana, Cheed na Killy wote walishea post ya video mpya ya Harmonize iitwayo Jeshi kwenye kurasa zao za Instagram.

Shule ya Sekondari ya Mivumoni Islamic yateketea kwa moto Alafajiri ya leo

Image
Shule ya Sekondari ya Mivumoni Islamic, iliyopo katika eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni Dar es Salaam, imeteketea kwa moto Alafajiri ya leo Agosti 31, 2020, na kuelezwa kuwa hii ni mara ya tatu shule hiyo kuungua ndani ya kipindi cha miezi miwili. Akizungumza kwenye kipindi cha SupaBreakfast ya East Africa Radio hii leo Kamishina Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni Salum Mohamed, amesema kuwa taarifa ya chanzo cha moto huo itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge. "Kwa kipindi cha miezi miwili hili ni tukio la tatu katika shule hii, Julai 18 tulipata tukio la moto la muundo huu na tulizima, Julai 23 tukio la moto tena lilitokea hili ni tukio la tatu mfululizo ndani ya eneo moja, ni matukio ambayo yanaendelea kutokea ndani ya hizi Shule za Kiislamu za Jijini Dar es Salaam, uchunguzi umefanyika na Msemaji wa hili ili kujua chanzo ni nini ataitoa Mkuu wa Mkoa " amesema Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto. Aidha Kamis

Kiongozi wa upinzani Congo arejea Brazzaville baada ya kutibiwa Uturuki

Image
Kiongozi wa upinzani wa Congo - Brazzaville Jean-Marie Michel Mokoko amerejea Brazzaville jana baada ya kutibiwa nchini Uturuki kwa mwezi mmoja uliopita.  Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 73, aliyepambana na Rais mwenye msimamo mkali Denis Sassou Nguesso katika uchaguzi wa 2016, alifungwa miaka 20 jela mwaka wa 2019 kwa mashitaka ya kuhujumu usalama wa taifa na kumiliki silaha kinyume cha sheria.  Wakili wake Yvon Ibouanga amesema Jenerali Mokoko amerudi akitokea Uturuki na kupelekwa katika hospitali ya kijeshi mjini Brazzaville ambako alifanikiwa kuonana naye.  Amesema kiongozi huyo yupo katika hali nzuri na kuwa ombi rasmi la kutaka aachiwe huru litawasilishwa katika siku chache zijazo.  Duru ya idara ya magereza imesema atarudishwa katika chumba chake gerezani baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari.

Waandishi wa habari Mkoani Mtwara wapewa pongezi kwa mapambano dhidi ya magonjwa ya Mlipuko

Image
Na Faruku Ngonyani, Mtwara. Katika kuhakikisha jamii inakuwa na uelewa juu ya namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko, waandishi wa wa habari mkoani Mtwara wamejengewa uwezo ili kuweza kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi hususani wakati huu ambao dunia imekumbwa na ugonjwa wa Covid-19. Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo wakati wa kujengewa uwezo, mtaalamu wa magonjwa ya mlipuko kutoka ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, Sasita Shabani amesema mafunzo hayo yatawasadia na kupeleka taarifa sahihi kwa wananchi namna ya kujikinga na magonjwa hayo na kuchukua tahadhari. “Naamini kama wanahabari wataendelea na utaratibu huu wa kujengeana uwezo na kukumbusha namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko nchi yetu itaendelea kuwa salama na kuwa na Taifa la watu wenye afya njema,”amesema Shabani Kwa upande wa wanabari wametoa pongezi kwa saasita Shabani kwa mafunzi huku wakiahidi kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu hiyo kupitia vyombo vya vya habari. Mafunzi hayo yaliandaliwa n

Bunge la Macedonia Kaskazini lamuidhinisha Zoran Zaev kuwa waziri mkuu

Image
Wabunge wa Macedonia Kaskazini wamemuidhinisha Zoran Zaev kuwa waziri mkuu baada ya kumpigia kura 62 dhidi ya 51 kuchukua wadhifa huo. Zaev anatarajiwa kurejea ofisini baada ya kuondoka Januari, kufuatia mpango uliofikiwa mwezi huu kati ya chama chake cha Social Democratic - SDSM na Democratic Union for Integrations - DUI, chama kikubwa kinachoiwakilisha jamii ya Waalbania.  Ratiba ya Zaev ni pamoja na kumteuwa waziri mkuu mwenye asili ya Kialbania mwishoni mwa muhula wa serikali.  Kura hiyo imepigwa baada ya saa nyingi za mdahalo jana. Itakuwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo iliyojitenga kutoka Yugoslavia ya zamani mwaka wa 1991 kuwa na waziri mkuu mwenye asili ya Kialbania. Waalbania wamekuwa wakishinikiza kupewa haki zaidi tangu nchi hiyo ilipopata uhuru.

Rais wa Lebanon akiri haja ya "kuubadili mfumo"

Image
Rais wa Lebanon Michel Aoun amekiri haja ya "kuubadilisha mfumo" wa kisiasa nchini humo na kutoa wito wa kutangazwa taifa lisiloegemea dini katika mkesha wa ziara ya mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron.  Mshirika wa kisiasa wa Aoun, mkuu wa kundi la Hezbollah Hassan Nasrallah pia alisema mapema kuwa anakaribisha pendekezo la Macron la kuwepo mkataba mpya wa kisiasa Lebanon.  Wakati huo huo vigogo wa kisiasa wa madhehebu ya Sunni akiwemo waziri mkuu wa zamani Saad Hariri wamempendekeza Mustapha Adib kuwa waziri mkuu mpya, hatua ambayo vuguvugu la maandamano Lebanon liliipinga mara moja likisema inakwenda kinyume na mabadiliko wanayoyataka.  Adib, mwenye umri wa miaka 48, ni balozi wa Lebanon nchini Ujerumani na hafahamiki sana katika ulingo wa kisiasa.  Ikiwa chini ya wiki nne baada ya kuzuru Beirut kufuatia mlipuko mkubwa katika bandari ya mji huo uliowauwa zaidi ya watu 180, Macron anarejea nchini humo leo kushinikiza masharti yake ya kufanywa mabadiliko.

Mtibwa Sugar yamalizana na majembe kazi yake sita

Image
  JUMA Nyangi, nyota wa zamani wa Klabu ya Alliance FC ya Mwanza anatimiza idadi ya nyota sita waliosajiliwa na Klabu ya Mtibwa Sugar. Nyangi alitambulishwa rasmi jana, Agosti 30 kwa kusaini kandarasi ya miaka miwili ndani ya kikosi cha wakata miwa cha Morogoro. Wachezaji wengine ambao tayari Mtibwa Sugar imemalizana nao ni pamoja na Abal Kassim kutoka Azam FC, Baraka Majogoro kutoka Polisi Tanzania,  George Makanga kutoka Namungo,Hassan Kessy kutoka Nkana FC na Geoffrey Luseke kutoka kutoka Alliance. Mtibwa Sugar ilimtambulisha jana Kessy ambaye ni beki wa kulia kwenda kuziba pengo la Shomari Kibwana aliyeibukia ndani ya Yanga. Nyota hao wataanza kuitumikia Mtibwa Sugar ndani ya msimu wa 2020/21 unaotarajiwa kuanza Septemba 6 kikiwa chini ya Kocha Mkuu,  Zuber Katwila.

Trump, Biden washutumiana kuhusu vurugu zinazotokea nchini humo

Image
Rais wa Marekani Donald Trump na mpinzani wake wa Democratic Joe Biden wameshutumiana kutokana na vurugu zilizotokea huko Portland, Oregon. Bwana Trump amemlaumu meya wa Democrat huko Portland, Ted Wheeler, kwa kuruhusu kutokea kwa kifo na uharibifu mjini humo. Lakini Bwana Biden amesema rais alikuwa anachochea vurugu hizo. Mwanaume mmoja alipigwa risasi huko Portland Jumamosi huku kwingineko mjini humo wanaopendelea Trump walikabiliana na waandamanaji wa Black Lives Matter. Portland imekuwa kitovu cha maandamano dhidi ya ukatili unaotekelezwa na polisi na ubaguzi wa rangi tangu kutokea kwa mauaji ya George Floyd, Mmarekani mweusi huko Minneapolis, Mei 25 na kusababisha ghadhabu nchini na hata kimataifa. Katika msururu wa ujumbe wa Twitter Jumapili, Bwana Trump alisema kwamba "Portland haiwezi kujikwamua kutokana na hali hiyo kwa kuwa na meya mpumbavu", na kupendekeza kwamba atapeleka majeshi ya serikali mjini humo. Pia amemshutumu Bwana Biden kwa "kutokuwa na ari

Kikwete aishauri Yanga "Achaneni na mvutano wa Morrison kwa kuwa mwanapoteza muda"

Image
 ALIYEKUWA Rais wa awamu ya nne wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ameishauri Yanga kuachana na mvutano wa suala la mchezaji, Bernard Morrison kwa kuwa wanapoteza muda na badala yake wawekeze nguvu kuibua vipaji vipya Kikwete ameyasema hayo jana, Agosti 30 kwenye Kilele cha Wiki ya Mwananchi ampabo yeye alikuwa ni mgeni rasmi Uwanja wa Mkapa. Morrison amekuwa kwenye mvutano na Yanga kuhusu suala la mkataba, Yanga inaeleza kuwa ana mkataba wa miaka miwili huku Morrison akisema dili lake la miezi sita lilikwisha. Shauri hilo lilisikilizwa Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji Tanzania kwa muda wa siku tatu mfululizo kuanzia Agosti 10-12 na mwisho Morrison alitangazwa kuwa mshindi kwa kile kilichoelezwa kuwa kulikuwa na mapungufu kwenye mkataba. Kikwete amesema:"Naskika ninyi mwaka huu mmeibiwa mchezaji na majirani zenu,hilo ni jambo la kawaida kwani masuala haya kwa watani wa jadi hayajaanza leo ni ta

Uturuki imekemea vikali kuchomwa kwa Quran nchini Uswidi

Image
Uturuki kupitia wizara yake ya mambo ya nje imekemea vikali kiitendo cha kuchomwa moto Quran nchini Uswidi. Uturuki imekemea  vikali kitendo cha kuchomwa moto Quran kilichotokea nchini Uswidi. Uturuki imefahamisha kuwa imeshangazwa na kitendo hicho ambacho kimetajwa kuwa kitendo cha uchokozi na uchochezi. Uturuki imesema kuwa  kitendo hicho ni  pigo kubwa dhidi ya utamaduni ya kuishi  pamoja na kuheshimu  thamani za utofauti wa tamaduni za Ulaya. Kitendo hicho, Uturuki imefahamisha kuwa ni  kitendo cha uchokozi   dhidi ya jamii ya waislamu. Taarifa ya maandishi iliotolewa na  wizara   ya mambo ya nje ya Uturuki zimelaani kiitendo hicho kilichotekelezwa na  mwanasiasa mwenye sera za kibaguzi na chuki dhidi ya uislamu kutoka nchini Danmark .

Tetesi za soka kimataia

Image
Manchester City wanajianda kulipa kiasi cha pauni Milioni 450, ili kuweza kusajili Lionel Messi ikiwa ni mpango wa kumsajili kwa miaka mitano na sehemu ya mkataba huo kujiunga na timu New York City, (Sport, via Daily Star) Tottenham ilijaribu kutaka kuingilia kati na kuvurugwa uhamisho wa kiungo wa Ajax Donny van de Beek, anayekwenda kujiunga na Man United. Manchester United imefanya mazungumzo na Aston Villa wakati inajitahidi kufikia makubaliano ya mchezaji Muingereza Jack Grealish, 24. (Mail) Manchester United imejiunga na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati ya Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 29. (Dagbladet TV, via Sun) Leeds United imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Udinese raia wa Argentina Rodrigo de Paul,26, lakini imearifiwa kwamba hatua yoyote ya kumsajili mchezaji huyo itawagharimu pauni milioni 31. (Guardian) Tottenham na Newcastle zimeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Josh King, 28. (Chronic

MAGAZETI YA LEO 31/8/2020

Image