Klabu ya Simba yapata ugeni kutoka Ujerumani
Wageni wa klabu ya soka ya wanawake Simba Queens, timu ya St Pauli ya Ujerumani wamewasili nchini leo Februari 29, 2020 majira ya Saa 9:30 Alfajiri kwa ajili ya kuitembelea klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Simba, ujio huo wa St Pauli ni muendelezo wa ushirikiano baina ya timu hizo.
'St Pauli wamefika nchini wakiwa na jumla ya wachezaji 15 na watakuwa hapa kwa muda wa siku 15 ambapo pia watatembelea Zanzibar na Morogoro ikiwa ni sehemu ya wao kuufurahia sehemu za kitalii katika Miji hiyo mbali na kucheza michezo kadhaa ya kirafiki', imeeleza taarifa hiyo.
Mbali na kucheza mechi pia wataelimisha jamii kuhusu usawa wa kijinsia, katika kufanikisha azma ya kufuta unyanyasaji wa kijinsia katika jamii kwa kutumia michezo
Comments
Post a Comment