Posts

Showing posts from May, 2020

DC Morogoro atoa siku 14 wenye vibanda vya nyasi kuondoka Msamvu

Image
Mji wa Morogoro umekumbwa na taharuki usiku wa kuamkia juzi baada ya moto kuzuka katika stendi kuu ya mabasi Msamvu na kuteketeza vibanda vya wafanyabiashara wanaoendesha shughuli zao katika stendi hiyo, ambapo Mkuu wa wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, ametoa agizo la siku 14 kubomolewa kwa vibanda vyote vilivyopo kituoni hapo. Mkuu wa wilaya ya Morogoro ameeleza hayo baada ya tukio la moto uliosababishwa na uunguwaji holela wa umeme katika vibanda hivyo na kusababisha kuteketeza mali zao. Zaidi ya vibanda viwili huku Mkuu wa Wilaya akimuagiza meneja wa tanesco morogoro kukata umeme unaongia katika vibanda hivyo.

Ofisi ya DC Lindi yaipa kongole halmashauri ya manispaa ya Lindi

Image
Na Ahmad Mmow, Lindi. Kufuatia jitahada kubwa zilizofanywa na watendaji na madiwani wa halmashauri ya manispb ya Lindi. Serikali wilayani Lindi imepongeza halmashauri hiyo.  Pongezi hizo zilitolewa juzi na katibu tawala wa wilaya(DAS) ya Lindi, Thomas Safari wakati wa kikao cha mwisho cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kilichofanyika juzi katika ukumbi wa mtakatifu Andrea Kagwa uliopo manispaa ya Lindi. Safari alisema licha ya changamoto ndogondogo ambazo baadhi yake zimesababishwa na raslimali chache lakini inastahili kupongezwa.  Alisema ushirikiano wa madiwani na watendaji wanaongozwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Joomary Satura umesababisha mabadiliko makubwa ya maendeleo.  Alisema ushirikiano huo licha ya kubadilisha mandhari ya manispaa, hasa kwenye miundombinu ya barabara, lakini pia umeiletea sifa na heshima manispaa hiyo.  Alisema barabara nyingi katika mitaa ya katikati ya manispaa hiyo zimejengwa barabara za kiwango cha lami. Hali amba

Ngasa: Tupo tayari kurejea kwenye ligi

Image
MRISHO Ngasa, kiungo mkongwe ndani ya Klabu ya Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kurejea kwenye mechi za ushindani baada ya kuanza mazoezi Mei 27. Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia.Serikali imeruhusu masuala yamichezo kuanza Juni Mosi na tayari bodi ya ligi imetangaza kuwa Juni 13 ligi itaanza. Ngassa amesema kuwa wanaendelea vizuri na mazoezi jambo linalowafanya wazidi kujiamini pale ligi itakapoanza. “Kila kitu kinakwenda vizuri kwenye mazoezi na kila mchezaji anafurahi kwani tulikuwa nje kwa muda mrefu, kwa sasa tupo tayari kurejea uwanjani ili kuendelea pale ambapo tuliishia,” amesema. Yanga ikiwa imefunga mabao 31, Ngasa amehusika kwenye mabao matatu, akifunga mawili na kutoa pasi moja ya bao.

Jafo atoa siku 17 ujenzi wa soko Morogoro kukamilika

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo ameagiza kukamilishwa kwa ujenzi wa soko la Manispaa ya Morogoro ifikapo Juni 17 mwaka huu. Agizo hilo amelitoa leo mjini Morogoro katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Ofisi hiyo yake baada ya kuona kuwa limechelewa kukamilika ndani ya muda uliopangwa awali. ”Hili ni Soko  kubwa la bidhaa kupitia fedha za miradi ya kimkakati hapa nchini lilioanza kujengwa mwanzoni mwa mwaka wa jana ambalo litawezesha wafanya biashara kupata mazingira rafiki ya kufanyia biashara”amesema Jafo Aidha Jafo ametembelea na kujionea  ujenzi wa stendi ya daladala ya Mafiga inayojengwa chini ya usimamizi wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini(Tarura)  kwa ajili matumizi ya Manispaa hiyo ya Morogoro huku akifurahishwa na kazi ya ujenzi wa stendi hiyo ambayo imefikia  wastani wa asilimia 98 ya ujenzi. Jafo ameitaka Manispaa hiyo kuendelea kusimamia ukusanyaji wa mapato kutoka kat

Yanga yaweka historia ya aina yake, yasaini mkataba na La Liga

Image
Kutokana na janga la Corona viongozi wa La Liga na wale wa Sevilla wameshindwa kuhudhuria tukio la kusaini mkataba wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji la kihistoria iliyofanyika pale Serena Hotel. Hata hivyo viongozi hao wametuma video clip wakielezea uzuru wao na kueleza mpango kazi wao nini watakifanya kuhakikisha Yanga SC inafanikiwa kisha mkurugenzi wa La Liga akasaini mkataba na kuutuma kisha Yanga SC kuupokea, Mshindo Msolla na Eng Hersi Said wameusaini na kukamilisha zoezi! Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo amepongeza jitihada hizo zinazofanywa na viongozi hao hivyo amewataka kuendelea na uimarishaji katika sekta ya michezo. “Niwapongeze kwa hili la leo, matamanio ya uendeshaji kwa Yanga ni ya muda mrefu toka kwa Castro Mponela. .alipokuja na Yanga kampuni , la pili alipokuwa Yusuf Manji alipokuja na dhana ya kukodisha hili litakuwa la tatu mengine yalikuwa kubadilisha katiba”. Amesema Dkt.Kikwete.

Wakili asema kifo cha George Floyd kilipangwa

Image
Wakili wa familia ya George Floyd, ambaye kifo chake kiliibua maandamano ya hasira kote nchini Marekani , amemshutumu afisa wa polisi kwa "kupanga mauaji". Polisi wa Minneapolis Derek Chauvin ameshitakiwa kwa mauaji , lakini wakili Benjamin Crump amekiambia kituo cha habari cha CBS news kuwa yalikuwa ni mauaji ya kiwango cha kwanza. "Tunadhani kwamba alikua na nia … takriban dakika tisa aliendelea kushindilia goti lake kwenye shingo ya mwanaume ambaye alikua anamuomba amsamehe na kumwambia kuwa hawezi kupumua," alisema matukio ya uporaji yameripotiwa katika jimbo la Philadelphia. Video kutoka katika vituo viwili vya televisheni vya Philadelphia Jumapili zilionesha vijana wakivunja magari kadhaa ya polisi na kuiba katika duka moja . Rais Donald Trump alituma ujumbe wake wa twitter uliosema: Sheria na amri vifuatwe Philadelphia, SASA! Wanapora maduka. Walete wanajeshi wetu waingilie kati ". Tukio la Floyd limeibua ghadhabu miongoni mwa Wamarekani ju

MAGAZETI YA LEO 1/6/2020

Image

Wema Awashukuru Wanaomtakia Ndoa Njema

Image
Staa mkubwa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu amemshukuru Mungu kwa kuona watu ambao ni mashabiki wake wakimtakia ndoa njema. Wema amefunguka juu ya ishu iliyosambaa mitandaoni kama moto wa kifuu juzikati kuwa ameolewa ambapo amesema amejisikia furaha mno kuona watu wakimuombea apate mume, jambo ambalo anaamini Mungu atapokea maombi yao. Wema ameliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, aliona watu ni jinsi gani walivyokuwa na shauku ya kumjua muoaji na hiyo kwake ni baraka tosha na Mungu akipenda, kitu hicho kitafanyika muda si mrefu na siyo kwa uwezo wake, bali wa Mwenyezi Mungu. “Nimeona kwa kweli ni jinsi gani watu walivyo na upendo na mimi kwa kusema tu naolewa, hivyo naomba Mungu azipokee dua zao. “Mimi ninachokiamini, jambo hilo litafanyika tu siku za usoni, lakini ni kwa uwezo wa aliye juu na si mwingine,” amesema Wema ambaye aliweka picha kwenye ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram zikimuonesha akiwa amechorwa ina kama bibi harusi, jambo ambalo amesema bado, lakini linakuja

WHO: Uongozi imara chanzo cha Afrika kupata maambukizi madogo ya corona

Image
Shirika la Afya Duniani (WHO), limesema kuwa uongozi imara wa nchi ni moja kati ya sababu za Afrika kupata kiwango kidogo cha maambukizi ya virusi vipya vya corona (covid-19), tofauti na ilivyotarajiwa. Afrika ina 1.5% ya visa vyote vya corona vilivyoripotiwa duniai kote, na ina 0.1% ya vifo vya corona duniani kote, kwa mujibu wa WHO. Mkurugenzi wa WHO Ukanda wa Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti alitoa kauli hiyo alipozungumza na vyombo vya habari mwishoni mwa wiki, kuhusu hali ya maambukizi barani Afrika. “Kwa kuwa na uongozi imara wa nchi zake na kutekeleza maelekezo ya wataalam wa afya kujikinga na virusi vya corona, visa vya corona barani Afrika vimebaki katika kiwango cha chini zaidi ya maeneo mengine duniani,” alisema Dkt. Moeti kwenye mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari ulioandaliwa na WHO na Jukwaa la Uchumi la Dunia (World Economic Forum). Dkt. Moeti amesema kuwa WHO imewapa mafunzo wataalam 10,000 wa afya Afrika kwa ajili ya kusaidia kukinga na kudhibiti usambaaji

Mahabusu kuanza kufanya kazi kama wafungwa

Image
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuhakikisha mahabusu waliopo katika magereza nchini wanaanza kufanya kazi kama ilivyokuwa kwa wafungwa. Amesema mchakato huo ambao tayari umeanza, utakapokamilika utaleta mapendekezo ya jinsi gani ya kuwatumia mahabusu hao na wafungwa kufanya kazi za uzalishaji mali na kuhakikisha Jeshi la Magereza linajitegemea kikamilifu. Aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na maofisa na askari magereza katika magereza ya Segerea, Ukonga na Keko Dar es Salaam, alipofanya ziara ya kusisitiza magereza kujitegemea. Alisema ili binadamu ale ni lazima afanye kazi na pia vitabu vitakatifu vinasisitiza hilo, hivyo mahabusu wanapaswa kufanya kazi kwa kuwa nao wanakula vyakula magerezani. “Kuna mjadala mkubwa tunaendelea kuchakata kuhusu mahabusu waweze kufanya kazi, lengo letu si kuwafanyisha kazi za sulubu, au kazi zinazotweza utu wao, hapana, wao pamoja na wafungwa wana adhabu wan

Trump amekatisha uhusiano wa Marekani na WHO

Image
Bwana Trump amekosolewa nyumbani na nje ya nchi baada ya Maekani kujiondoaa kama mshirika wa Shirika la Afya Duniani - WHO. Umoja wa Ulaya umemsihi kufikiria tena uamuzi wake huku waziri wa afya wa Ujerumani akiitaja hatua hiyo kuwa ni wenye kukatisha tamaa kwa afya kimataifa. Mkuu wa kamati ya afya ya bunge la seneti Marekani, ambaye ni wa Republican kama Trump amesema kuwa huu sio wakati wa kujiondoa kwenye shirika hilo. Bwana Trump amesema WHO imeshindwa kuwajibisha China juu ya mlipuko wa virusi vya corona. The WHO, shirika linalosaidia kuimarisha masuala ya afya na kukabiliana na milipuko ya magonjwa imekuwa ikikosolewa kila wakati na Rais huyo wa Marekani kutokana na jinsi ilivyo shughulikia janga la corona. Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa wahudumu wa afya na wanasiasa, wengi wakiwa wanahofia kuwa maamuzi ya Trump yanaweza kuharibu jitihada ambazo tayari dunia imezifanya kukabiliana na mlipuko huu. Tayari, Umoja wa Ulaya umeandika maelezo ya pamoja ikimtaka rais U

Jengo la halmashauri lililotumia Sh milioni 200 ladaiwa kutekelezwa

Image
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, amemtaka Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani humo kuchunguza matumizi ya Sh milioni 202  zilizotumika katika ujenzi wa nyumba ya Mkurungezi wa Manispaa ya Songea. Agizo hilo alilitoa jana  alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye jengo hilo ambalo linadaiwa kutelekezwa kwa miaka minne bila kukaliwa na mtumishi yeyote huku fedha za Serikali zikiwa zimetumika.  Mndeme alisema kwa taarifa alizonazo jengo hilo limejengwa tangu mwaka  2016, lakini hadi sasa halikaliwi na mtumishi yeyote jambo ambalo ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali.  Alisema kibaya zaidi uongozi wote wa halmashauri na wilaya upo na wanaangalia fedha za Serikali zilivyotumika katika jengo hilo bila kuchukua hatua stahiki.  Kufuatia hali hiyo, alimwagiza Kamanda wa Takukuru kuhakikisha anachunguza kwa umakini fedha zilizotumika katika ujenzi huo, huku akimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhamia kwenye nyumba hiyo ndani ya siku tatu.

Wanaodaiwa kuwa wapenzi wakutwa wamejinyonga

Image
WATU wawili; Jackson Hamis (24) na Lenista Mligo (24) wakazi wa Making’inda Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao wanadaiwa kuwa ni wapenzi, wamekutwa wamefariki dunia kwa kujinyonga katika maeneo mawili tofauti, huku mazingira ya vifo vyao yakiwa ni ya kutatanisha.  Akizungumza juzi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maingwa, alisema tukio hilo lilitokea Mei 29, mwaka huu saa 1.30 asubuhi katika maeneo  tofauti yaliyopo Kata ya Msamala, Mtaa wa Making’inda, Manispaa ya Songea. Kamanda Maigwa alilitaja tukio la kwanza kuwa ni la Lenista ambaye alikutwa kwenye mti akiwa amejinyonga kwa mtandio, huku miguu ikiwa imegusa chini ya ardhi jambo ambalo alisema linatiliwa shaka kama amejinyonga mwenyewe au kauawa na kuwekwa kichakani hapo.  Alisema tukio la pili ni la Hamis aliyekutwa chumbani alimokuwa akiishi akiwa amejinyonga kwa kutumia shuka ambalo alifunga juu ya kenji ya nyumba hiyo.  Kamanda Maigwa alisema kabla ya tukio hilo, wapenzi hao walionekana wakinywa pombe za

CAG awaweka matatani maofisa halmashauri

Image
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini, ameutaka uongozi wa Halmashuari ya Wilaya ya Itilima mkoani humo kuwachukulia hatua za kisheria watu wote waliosababisha uwepo wa hoja 36 katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Sagini alisema katika hoja hizo, wapo watumishi wa halmashuari hiyo ambao walishindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo, ambao ametaka watafutwe na wachukuliwe hatua kila mmoja kulingana na hoja yake. Alitoa maagizo hayo jana wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la halmashuari hiyo kilichokuwa maalumu kujadili taarifa ya CAG ya mwaka 2018/19. Sagini alisema maelekezo ya Serikali kutoka Ofisi ya Tamisemi yanawataka viongozi wa halmashuari kuchukua hatua za kisheria kwa wale wote ambao wamesababisha uwepo wa hoja kwenye ripoti hiyo. Alisema kumekuwepo na tabia ya kuchukuliwa hatua kwa watumishi wa ngazi za chini huku wakuu wao wa idara wakiachwa, jambo ambalo alisema halitakiwi kuonekana katika hatua hizo zitakazochukuliwa.

China yalaani kitendo cha Marekani kukataa kutoa vibali vya kuingia nchi hiyo wanafunzi wa China

Image
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amelaani kitendo cha Marekani kukataa kutoa vibali vya kuingia wanafunzi wa China katika nchi hiyo. Zhao Lijian amesema kuwa vitisho vya serikali ya Marekani dhidi ya wanafunzi wa China sambamba na kukataa kuwapatia viza, ni kinyume na uwazi na uhuru ambao Washington imekuwa ikidai kuutekeleza. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China ameitahadharisha Marekani isijaribu kukiuka kwa namna yoyote haki za wanafunzi wa China, kwa kuwa kitendo hicho kitakuwa ni ubaguzi wa rangi. Malalamiko ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China yametolewa katika hali ambayo Beijing imekuwa ikilalamikia uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya eneo la Hong Kong na Taiwan, na kuitaka isimamishe uingiliaji wake huo mara moja. Uhusiano wa Washington na Beijing umezidi kuvurugika na kufikia kiwango cha chini kabisa hasa baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump.

Wolper avishwa pete ya uchumba na kijana huyu

Image
Msanii wa filamu hapa nchini Jacqueline Wolper ameonekana kuvalishwa pete ya uchumba siku ya jana maeneo ya dukani kwake Sinza makaburini na mfanyabiashara wa mavazi bwana Chidy Designs. Hilo limedhibitishwa kupitia picha na video zinazosambaa mitandaoni zikiwaonyesha wawili hao wakichumbiana, na wakati Chidy Designs akimvalisha pete hiyo alisikika akisema maneno yafuatayo  "Nakupenda, nakuhitaji wewe ndiyo furaha yangu nipo tayari kutulia kwa asilimia mia moja na nipo tayari kuwaona wanawake wote wa pembeni kama frame za baiskeli nakupenda sana" Aidha kwa upande wa Jacqueline Wolper amesema  "Kiukweli nashindwa kuelewa hii hali imekuaje, sina cha kuongea ila nimefurahi na nimefarijika kwa kijana kama huyu kuwa tayari na kuamua kufanya hivi na naomba iwe kheri, nimempokea na nampenda sana" Chidy Designs amesema mahusiano yao yalianza muda mrefu na Wolper ni mwanamke ambaye anamjua kwa muda mrefu.

Waziri Jafo -"shule hii iitwe Jokate Mwegelo"

Image
Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Kisarawe Selemani Jafo amekagua ujenzi wa shule ya kwanza ya kihistoria ya wasichana ambayo inajengwa kwa usimamizi wa DC wa Kisarawe Jokate Mwegelo ambaye alisimamia harambee ya ukusanyaji wa fedha za ujenzi ili kumaliza tatizo la wanafunzi wengi hasa wa kike kupata sifuri katika matokeo yao ya kidato cha nne na sita. Fedha zilizopatikana katika harambee kupitia kampeni ya 'Tokomeza Zero' zimewezesha kukamilishwa kwa majengo 15 yakiwemo madarasa nane, nyumba ya walimu, mabweni, maabara, maktaba na vyoo”tumeweka hadi vimbweta” Waziri Jafo ametaka shule hiyo iitwe 'Jokate Mwegelo Girls Secondary School' kwasababu ya jitihada zilizofanywa na DC huyo katika kusimamia upatikanaji wa fedha mpaka kufikia hapo ambapo Serikali itamalizia madarasa na mabweni yaliyobaki "mwezi July mwaka huu, shule ianze kuchukua kidato cha tano"

Kikwete mgeni rasmi utiaji saini wa mabadiliko Yanga leo Mei 31

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete  leo Mei 31, 2020 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa utiaji saini wa mchakato wa mabadiliko ya Uendeshaji wa timu ya Yanga.

Rwanda yaripoti kifo cha kwanza cha mgonjwa wa corona

Image
Wizara ya Afya nchini Rwanda imeripoti kifo cha kwanza cha mgonjwa wa corona aliyetajwa kuwa ni dereva wa malori mwenye umri wa miaka 65. Taarifa ya Wizara hiyo iliyotolewa jana imeeleza kuwa mgonjwa huyo alipata maambukizi akiwa nchi jirani alikoenda kikazi, lakini alipozidiwa aliamua kurejea nchini humo kwa ajili ya matibabu. Mgonjwa huyo alipatiwa matibabu kutoka kwa wataalam wa afya lakini alifariki kutokana na matatizo ya kupumua. Hadi jana, Mei 30, 2020, visa vya corona vilifikia 359 nchini Rwanda, lakini wagonjwa 250 kati ya hao walishapona na wameruhusiwa kutoka hospitalini. Wagonjwa wanaendelea kupatiwa matibabu hadi sasa ni 108, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Afya. Rwanda imelegeza masharti ya kubaki nyumbani (lockdown), na imeruhusu baadhi ya biashara kufunguliwa baada ya kufungwa kwa muda kama hatua za awali za kuchukua tahadhari. Inatarajiwa kuwa kesho, Juni 1, 2020 waendesha pikipiki (bodaboda) wataanza kuruhusiwa kubeba abiria pamoja na kuruhusu mizunguko

Polisi wanasa pikipiki 825 zilizoibiwa, waanika mbinu zilizotumiwa na wezi

Image
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata jumla ya pikipiki 825 na vifaa vingine, zilizokuwa zimeibwa katika mikoa nane nchini. Pikipiki hizo zimekamatwa kufuatia amri iliyotolewa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro kufuatia kuongozeka kwa visa vya wizi wa pikipiki katika mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Mara (Tarime-Rorya) na Kagera. Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa jana, Mei 30, 2020 na Kamanda wa Oparesheni Maalum za Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Mihayo Msikhela, oparesheni hiyo ilifanyika kuanzia Mei 4 hadi Mei 29, 2020, katika mikoa nane. Alisema kuwa wakati wa oparesheni hiyo, walibaini kuwa wamiliki wengi wa pikipiki hawana mikataba ya maandishi na watu wanaoendesha pikipiki zao maarufu kama bodaboda. Pia, walibaini kuwa wapo ambao hawakuandikishana wakati wa kuuziana pikipiki; na wengine hawakubadili namba za usajili baada ya kununua kutoka kwenye makampuni husika. Aidha, Kamanda Msikhela alisema kuwa walibaini kuwa baadhi

ATCL yasafirisha abiria 200 waliokwama nchini

Image
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imewasafirisha abiria 200 kwenda chini India, waliokuwa wamekwama nchini kutokana na marufuku ya kufanya safari za anga za nje ya nchi, iliyowekwa Machi 25, 2020. Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kuwa wakati ndege hiyo inarejea, itawarudisha abiria 180 wa Tanzania waliokuwa wamekwama nchini India. Alisema kuwa kutokana na marufuku ya safari za anga kutoka na kuingia nchini kama hatua ya kupambana na mlipuko wa virusi vipya vya corona (covid-19), abiria wengi waliokuwa wanatarajia kusafiri kati ya India na Tanzania walikwama. “Tunaishukuru Serikali ya India kupitia ubalozi wake kwa ushirikiano wao hasa katika kipindi hiki ambacho wamesitisha usafiri wa anga ndani ya nchi yao,” alisema Mhandisi Matindi. Aliongeza kuwa katika kipindi hiki cha corona, ATCL iliendelea kutoa huduma ya usafiri ndani ya nchi kupitia viwanja 11, huku ikichukua tahadhari zote dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo. Kwa upande wake Balozi wa

Maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi nchini Marekani, sababu na hatari zake

Image
Marekani imetumbukia tena katika machafuko makubwa kutokana na malalamiko ya wananchi wanaopinga mauaji yaliyofanywa na polisi wa nchi hiyo dhidi ya raia mweusi. Katika kipindi cha siku nne zilizopita miji mbalimbali ya Marekani kuanzia Minneapolis hadi New York, Atlanta mpaka Houston na Milwaukee hadi Los Angeles imekumbwa na maandamano na ghasia kubwa baina ya raia wanaoandamana, na polisi. Watu kadhaa wamejeruhiwa katika baadhi ya machafuko hayo na kunashuhudiwa ghasia na hata oporaji wa maduka katika miji mingine. Inatupasa kusema hapa kuwa, kinachoshuhudiwa sasa nchini Marekani si hasira na vuguvugu la kupita tu la kulalamikia mauaji yaliyofanywa na polisi dhidi ya raia mweusi, George Floyd, aliyegandamizwa na kubinywa shingo na afisa wa polisi hadi kufa katika mji wa Minneapolis, bali ni mlipuko wa hasira za mamia ya miaka ya ukandamiza, dhulma na ubaguzi uliokita mizizi katika jamii ya Marekani dhidi ya watu weusi na jamii za waliowachache.   Meya wa New York, Andrew Cu

Lulu Diva Afunguka Kumwagiwa Maji ya Moto

Image
Mwanamuziki wa kike wa Bongo Fleva, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ amesema anawashangaa watu wanaosema amemwagiwa maji ya moto, kisa mume watu, jambo ambalo siyo kweli.Lulu Diva amesema kuwa, mwanaume huyo anayehusishwa naye ni kama ndugu yake. Akizungumza  Lulu Diva amesema siku zote vitu vya uongo vinavuma kuliko kitu chochote. Amesema Baraka anayetajwa ni mtu ambaye anafanya naye kazi na amekuwa kama ndugu yake.“Hivi kama nimemwagiwa maji ya moto jamani si ningeonekana basi hata na makovu mwilini? “Unajua siku zote kitu cha uongo kinasambaa kuliko kitu chochote maana Baraka ni kama kaka yangu kabisa, waache kupakaza uongo kama huo,” amesema Lulu Diva akipangua skendo ya kutembea na mume huyo wa mtu.

Madhara ya moto uliowaka Stendi ya Msamvu Morogoro

Image
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro SSP Michael Stephen, amesema moto uliotokea usiku wa kuamkia leo Mei 31, 2020nje ya stendi ya Msamvu, haujaleta madhara kwenye usafiri Akiongea asubuhi ya leo, SSP Michael Stephen amesema moto huo haujaleta madhara kwasababu umetokea kwenye vibanda vya nje ya stendi. ''Madhara makubwa kwenye usafiri hakuna kwasababu moto umetokea nje ya stendi ambapo umeunguza vibanda kadhaa pale lakini shughuli za usafirishaji ziliendelea kama kawaida'', amesema. Aidha SSP Michael Stephen amewataka wananchi wenye vibanda eneo hilo kuwa na tahadhari ya matumizi ya moto.

EU: Marekani inatukwamisha

Image
umeihimiza Marekani kutafakari upya uamuzi wake wa kukata ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa madai kwamba Shirika hilo halikushughulikia vizuri janga la corona. • Katika taarifa iliyotolewa kwa pamoja na, Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula Von der Leyen na Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja huo Josep Borell, wamesema wakati ambapo Ulimwengu unakabiliwa na kitisho cha janga la maambukizi ya virusi vya corona, Dunia inapaswa kuimarisha ushirikiano na kutafuta suluhuhisho kwa pamoja. Viongozi hao wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza kwamba vitendo vinavyodhoofisha na kukwamisha juhudi za Kimataifa za kutafuta matokeo mazuri vinapaswa kuepukwa na kila upande.

Shilingi 103.8 bilioni kugharamia usambazaji umeme wa gharama nafuu mitaa ya mijini

Image
. Na Ahmad Mmow, Lindi.  Katika kuhakikisha wananchi wanaoishi mitaa ya mijini ambayo inafanana na vijiji wanapata umeme wa gharama nafuu. Serikali imetenga shilingi 103,800,000,000(103.8 bilioni) kwa ajili ya kusambaza nishati hiyo katika mitaa ya mijini. Hayo yameelezwa na waziri wa nishati, Dkt Menrad Kalemani wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa gesi asilia kwa wateja wa nishati ya kupikia majumbani. Hafla ambayo ilifanyika jana katika mtaa wa Mnazi Mmoja, manispaa ya Lindi Dkt Kalemani alisema serikali imetenga kiasi hicho cha fedha ili wananchi wengi wanaoishi katika mitaa ya mijini ambayo mazingira yake yanafanana na vijiji wapate umeme wa gharama nafuu. Ambapo gharama za kuunganishiwa umeme huo itakuwa sawa na vijijini ambayo ni shilingi 27,000. Kutokana na azima hiyo ya serikali, waziri Kalemani amemuagiza meneja wa shirika la umeme(TANESCO) wa kanda ya Kusini ahakikishe utekelezaji wa azima huyo unaanza Julai, Mosi, mwaka huu w

Mpasuko mkubwa waibuka ndani ya kundi la kigaidi la Daesh (ISIS)

Image
Msemaji wa Jeshi la Iraq ameeleza kuwepo mpasuko mkubwa ndani ya safu ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) hasa baada ya kuuawa kiongozi wa genge hilo, Abubakar Al-Baghdad. Yahya Rasul, Msemaji wa Jeshi la Iraq aliyasema hayo jana Jumamosi ambapo akiashiria juu ya kuangamizwa Haji Taisir, mmoja wa viongozi muhimu wa kundi hilo la kigaidi, amesema kuwa licha ya kwamba kiongozi huyo wa (ISIS) alikuwa hatulii eneo moja na alikuwa hatumii simu wala mawasiliano yoyote, lakini mwishowe aliangamizwa katika operesheni kali iliyofanywa katika jimbo la Deir Ez-Zor, mashariki mwa Syria. Sambamba na kusisitiza kwamba hivi sasa kundi la Daesh linakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kukosa kiongozi, Yahya Rasul ameongeza kwamba kuna mabaki ya wanachama wa kundi hilo ambao juhudi zaidi zinapaswa kufanyika ili kuwaangamiza kabisa. Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS), limezidisha harakati zake nchini Iraq katika miezi ya hivi karibuni ambapo makumi ya wanamuqawama wa Harak

VIDEO: DC Jokate ''nilipoteuliwa maneno yalikuwa mengi''

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Jokate Mwegelo amesema wakati anateuliwa na Rais John Magufuli maneno yalikuwa mengi sana na watu walidhani Rais ameteua msanii msanii tu. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

VIDEO: Waziri Jafo amwagia sifa DC Jokate ''we ni mzuri kweli na unapiga kazi''

Image
Waziri wa Tamisemi Sulemani Jafo ameagiza kuanza kwa ujenzi mpya wa shule ya Sekondari Kisarawe pamoja na kuanza kufanya kazi kwa Zahanati ya Mhaga iliyopo Wilayani Kisarawe ili kupunguza changamoto za elimu na afya katika wilaya hiyo. Waziri Jafo ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua shule iliyojengwa kupitia kampeni ya tokomeza zero chini ya mkuu wa wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ambapo amesema pa moja na kujengwa kwa shule ya Kisarawe na Zahanati pia anatarajia kuongeza madarasa, maabara na majengo mengine ili kukamilisha shule hiyo iliofikia asilimia 70. Kwa upande wake DC Jokat amesema shule hiyo inakuwa ya 17 katika wilaya ya kisarawe ambapo mchakato wa waalimu pa moja na usajili umeshaanza hasa baada ya waziri kumpendekeza mwalimu mkuu wa shule hiyo ambayo imepewa jina Jokate Sekondari Mariam Mpunga ambaye awali alikuwa Mwl Wa shule ya Msingi Kibuta  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

MAGAZETI YA LEO 31/5/2020

Image