Baada ya kukamatwa mbowe aachiwa kwa dhamana


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ameachiwa kwa dhamana baada ya kuhojiwa katika kituo cha Polisi Bomang'ombe Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kwa zaidi ya saa mbili.

Mbunge huyo wa Hai alikamatwa leo Ijumaa Februari 28, 2020 saa 12 jioni baada ya kumaliza kuhutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Nkoromu kata ya Masama Kati wilayani Hai.

Amehojiwa kuanzia saa 12:35 jioni hadi saa 3:20 usiku na alipotoka katika kituo hicho amewaeleza waandishi wa habari kuwa hawezi kuzungumza chochote.

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamdun alilieleza Mwananchi kuwa Mbowe amekamatwa baada ya kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano huo.

Amebainisha kuwa maneno aliyoyatoa yanaashiria  uchochezi  na kuamsha hisia za wananchi, chuki dhidi ya Serikali ya Tanzania na polisi.

"Mbowe amekamatwa baada ya kutuhumiwa kusema au kutoa maneno yanayoashiria uchochezi, kuamsha hisia na chuki dhidi ya Serikali na polisi. Anahojiwa lakini baada ya mahojiano atapewa haki ya dhamana,” amesema kamanda Hamdun

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato