Posts

Showing posts from April, 2019

VIDEO: Taharuki yatanda Jiji la Arusha

Image
Mamia ya Wananchi wa jiji la Arusha usiku wa kuamkia Leo wameshindwa kulala vyema usingizi wao kutokana na kukumbwa na Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha kwa zadi ya saa nane. TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USIKOSE KU-SUBSCRIBE

Wizara mbili zaagizwa kusimamia mradi wa Tsh. Bilioni 9 na Rais Magufuli

Image
Rais John Pombe Magufuli ameziagiza Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kushirikiana kukamilisha ujenzi wa majengo mapya ya Chuo cha Ualimu cha Mpuguso Wilayani Rungwe. Rais ametaka ujenzi huo uendane na thamani ya fedha zaidi ya Tsh. Bilioni 9 ambazo zimeshatolewa na serikali kwa ajili ya mradi huo. Ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na Jumuiya ya wanachuo cha Ualimu Mpuguzo, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo mapya ya chuo hicho ambayo yatagharimu Tsh. Bilioni 9. Kwa upande wake Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Mary Mwanjelwa amesema serikali itatoa kibali cha kuajiri watumishi wapya zaidi ya 50,000 katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.

Prof. Kabudi afanya mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.),(kulia) akiwa katika mazungumzo na Naibu  Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika  Mashariki na Sudan, Balozi Makila James, katika Ofisi ndogo za Wizara Dar es salaam jana. 

Shirika la ndege la Kenya latangaza hasara

Image
Shirika la taifa la safari za ndege nchini Kenya, Kenya Airways(KQ) limetangaza kupata hasara ya kifedha mwaka uliopita kwa takribani dola za kimarekani milioni 75 ambayo ni sawa na Bilioni 7.55 ya Kenya. KQ inasema kuwa hasara imetokana na ongezeko kubwa bei ya mafuta, mishahara ya juu, migomo na viwango vya juu vya gharama za usafiri wa ndege.

Taarifa muhimu kutoka kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Image
Taarifa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu muongozo wa ubandikaji stempu za kodi za kielektroniki katika bidhaa zenye stempu za zamani na zisizo na stempu.

Almasi kubwa kuliko zote Tanzania yapatikana Shinyanga

Image
Mchimbaji mdogo wa Madini ya Almasi wilaya ya Kishapu aibuka na Almasi Kubwa kuliko zote Tanzania. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ametoa wito kwa wanunuzi wa Almasi kufika mkoani humo. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainabu Telack ndiye ameitangaza Almasi hiyo mbele ya waandishi wa habari kuwa inauzito wa karati 521 kuliko zote zilizochimbwa Mkoa wa Shinyanga au Tanzania kwa kuwa hadi sasa  Almasi zenye uzito wa karati 300-421ambazo zimekuwa zikipatikana mgodi wa wiliamson- Mwadui uliopo wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga. Picha na StarTV 

Tuzo za MO Dewji kufanyika mara pili ndani ya Simba SC

Image
Tuzo za Mo Simba zilizoasisiwa na Mohammend Dewji mwaka 2018 zinatarajiwa kutolewa kwa awamu ya pili baada ya kumalizika kwa msimu wa 2018/2019.

MAGAZETI YA LEO 1/5/2019

Image

Makosa yanayofanywa na wanaume katika mahusiano

Image
Kuna mambo ambayo mtu anaweza kufanya pasi na kujua kuwa anafanya makosa. Ikija katika masuala ya mahusiano, wanaume wengine huchukulia kama mzaha. Wakishafaulu kutongoza na kumteka hisia mwanamke, wao hujisahau na kuanza kuishi nao kama mtu wa kawaida. Leo tumekuja na ujuzi wa kukuonyesha makosa ambayo unaweza kuwa unayafanya bila kujua kuwa yana athari. Kiufupi ni makosa ya kijinga ambayo yanaweza kuepukika kirahisi iwapo utayafuatilia. Hii ni muhimu kwa kuwa ukiachana na makosa haya basi unaweza kudumu katika mahusiano marefu na mpenzi wako zaidi. Yafutayo ndiyo makosa yanayofanywa na wanaume katika mahusiano; Unasahau kujijenga kibinafsi Kosa lengine ambalo wanaume hujipata katika uhusiano ni pale ambapo wanatelekeza majukumu yao ya kujiendeleza kimaisha. Wanasahau mambo ambayo walikuwa wakifanya ama walikuwa wakitarajia kufanya kabla kuingia katika uhusiano wa kimapenzi. Kusahau marafiki zako Ni kawaida kupunguza mawasiliano na marafiki zako pindi ambapo utaingia kati

Kuondoa mikunjo ya ngozi

Image
MIKUNJO  katika ngozi ni miongoni mwa matatizo yanayowakabili wanawake wengi. Tofauti na mikunjo ya uzee, mikunjo hii hutokana na kuchoka kwa ngozi kunakosababishwa na mambo mablimbali. Katika kupambana na tatizo hilo, wadau wa urembo wa asili wamegundua njia mbalimbali zinazoweza kutumika kutatua tatizo hili. Wadau hao wanashauri kumwona mtaalamu wa afya kwa ushauri zaidi wa matumizi ya njia hizo za asili kabla ya kuanza kutumia njia za asili kwani hata kama ni vipodozi asilia, haina maana kama ni salama kwa watu wote. Kwa mujibu wa wadau hao, unaweza kutumia viungo vinavyopatikana jikoni kwako kupambana na mikunjo katika ngozi. Baadhi ya viungo hivyo ni pamoja na: Karoti Tumia juisi ya karoti kwa kupaka katika ngozi yako, hasa katika maeneo yaliyoathirika. Karoti ina virutubisho muhimu kwa ngozi yako. Pia ina uwezo mkubwa wa kuondoa sumu ndani ya ngozi. Si hivyo tu, karoti inaweza kuondoa kabisa tatizo la mikunjo ya ngozi hasa sehemu za pembeni ya macho, shingo na maen

Biashara ya nafaka ya mtaji mdogo

Image
Iwapo wewe ni muajiriwa na muda haukutoshi kujiingiza katika biashara kubwa zinazohitaji muda, basi amua kufanya biashara hii ya nafaka. Wapo ambao wanaishi katika nyumba zenye nafasi ya kutosha, pia wapo ambao wana chumba kimoja na sebule na hawana mahali pa kuhifadhi magunia kadhaa ya nafaka. Ila iwapo una vyumba viwili basi angalia namna ya kugawa nafasi hiyo uweze kuweka hata angalau gunia 20 za kilo hamsini hamsini kwa kuanzia ili utapopata faida ya msimu huu uweze kujiwekea malengo ya kupangisha chumba kimoja cha ziada. Kwa kawaida nafaka zote huwa bei ndogo wakati zinapovunwa na bei hupanda pole pole kadri muda unavyoenda. Hivyo hakuna siku utapata hasara kwa kuhifadhi nafaka zilizovunwa endapo utafuata taratibu za uhifadhi ili nafaka zisiharibiwe na wadudu ama panya. Hebu tuchukulie kwa mfano, mwezi mmoja baada ya watu kuvuna mahindi na maharage ukaamua kununua kilo 500 za mahindi na kilo 500 za maharage. Ukazihifadhi katika magunia ya kilo hamsini hamsini. Utakuwa n

Huu ndiyo Ugonjwa utokanao na Msongo wa Mawazo

Image
Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi. Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi. Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe  na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo. Ufuatayo ni ugonjwa unaosabishwa na msongo: Magonjwa ya moyo Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo. Magonjw

Jambo hili ni muhimu sana katika kupata mafanikio

Image
Inasemekana ya kwamba mtazamo chanya n rasilimali tosha dhidi ya kuuaga umaskini, aidha watalamu wa masuala haya ya elimu ya mafanikio wanazidi kusisitiza ya kwamba ili mtu aweze kufanikiwa anakiwa kuibeba mitazamo  hiyo chanya kila wakati. Lakini licha ya watu wengi kuibeba mitazamo hiyo chanya wamekuwa wakisahau kitu kimoja, kitu  hicho  ni muhimu sana kwani huenda sambamba na mitazamo hiyo chanya. Na leo nataka nikwambie kitu hicho, kwani kuwa na mtazamo chanya bila ya kuwa na kitu hicho ni sawa na bure. Kitu chenye ni hiki, mtazamo chanya huenda sambamba na " kuwajibika" watu wengi kama ujuzi  na maarifa wanayo ya kutosha, ila tatizo ni kule kunakowafanya watu hao kuwa mtazamo chanya zaidi ila wamesahau kuwajibika juu ya kitu walichonacho. Tangu umeanza kujifunza mambo mbalimbali ya mafanikio naamini mpaka sasa kwa sehemu fulani una mtazamo chanya juu ya jambo fulani, ila kinachokoseana kutoka kwako ni kule kunakoitwa kuwajibika juu ya mtazamo huo. Hivyo mimi naa