Marufuku kushikana mikono na kukumbatiana

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito kwa wananchi kuacha kupeana salamu ya kupeana mikono na kukumbatiana hasa kipindi hiki cha tishio la virusi vya cororna.

“Katika kipindi hiki cha tishio la virusi vya corona nawataka Wananchi wajizuie kabisa kupeana mikono, kukumbatiana na kupeana mabusu, najua ni ngumu hii kwa Watanzania lakini tujitahidi ili kujiepusha na kuwaepusha wenzetu na maambukizi”- WAZIRI UMMY @ummymwalimu •

“Njia kuu za kuambukizana corona zinatoka kwenye majimaji, kwahiyo unavyombusu, kumkumbatia au kumshika mkono mwenzio unamuweka kwenye hatari, na kama utampa mkono haraka kanawe maji, kwa kipindi hiki tusalimiane hata kwa ishara na usipopewa mkono usinune” -WAZIRI UMMY MWALIMU

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato