Ajinyonga kwa msongo wa mawazo
HAROUN Abdalla Faki (30) amekutwa amejinyonga huko Bububu Kijichi Mkoa wa Mjini Magharibi huku ikidaiwa chanzo chake kukabiliwa na msongo wa mawazo. Mmoja wa ndugu wa familia, aliyejitambulisha kwa jina mmoja, Juma alisema Faki alifika Bububu Kijichi kwa mjomba wake kwa ajili ya matembezi ya kawaida. Hata hivyo, kwa muda wa wiki moja alionekana akiwa na wasiwasi na mtu asiye na furaha muda mwingi, sawa na mtu aliyekumbwa na msongo wa mawazo. Akielezea tukio hilo, mtu huyo alikutwa akiwa tayari amejinyonga kwa kutumia shuka. “Haroub alifika Bububu Kijichi kwa mjomba wake kwa ajili ya matembezi ya kawaida ingawa kwa muda wote hakuwa na furaha akiwa sawa na mtu anayeonekana kuwa na msongo wa mawazo,” alisema. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Awadh Juma Haji alithibitisha tukio hilo na kuwataka vijana kuacha kutumia sheria mikononi mwao. Kwamba wanapokumbwa na misukosuko, wapate ushauri kwa watu husika. Alisema katika kipindi cha hivi karibuni, yamejitokeza matukio...