Kesi ya anayetuhumiwa kumuua na kumchoma moto mkewe upelelezi wakamilika
Upelelezi wa kesi ya mfanyabishara Khamis Saidy, anayekabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya kumuua na kisha kumchoma moto mke wake Naomi Marijani, tayari umekwishakamilika.
Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon ambapo ameileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.
Wakili Wankyo ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Salum Ally, wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa, ambapo imepigwa kalenda hadi siku ya Januari 7, 2020, itakapotajwa tena.
Ikumbukwe Mfanyabishara Khamis Saidy, anadaiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni, baada ya kumuua na kisha kumchoma moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake na kisha kuyabeba mabaki ya mwili huo na kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga.
Comments
Post a Comment