Deni la Serikali laongezeka kwa asilimia 11
Serikali imesema Deni la Serikali limeongezeka kwa asilimia 11 kutoka kiasi cha shilingi Trillion 49.84 katika miezi 6 ya mwazo ya utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2018/19 hadi kufika trillion 54.84 kwa kipindi cha miezi sita ya utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2019/20.
Akitoa tathimini ya utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2019/20 kwa kipindi cha miezi sita ya mwazo jijini Dodoma Waziri wa Fedha na Mipago, Dkt. Philip Mpango amesema deni hilo bado ni himilivu kulingana na viwango vya kimataifa ikiwamo kulingana na pato la Taifa.
Amesema ukuaji wa Deni hilo ni kutokana na mikataba ya mikopo iliyoingiwa kipindi cha nyuma pamoja na mikopo ya riba nafuu kwa ajili ya ujenzi wa miradi mikubwa inayojengwa nchini.
Katika ukuaji wa pato la Taifa Waziri Mpango amesema pato la taifa limekuwa kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka uliopita ukuaji huo ukichangiwa na ongezeko la michango ya ukuaji shughuli za kiuchumi na kuwanufaisha wale wanaoshiriki.
Comments
Post a Comment