Daraja kubwa zaidi laanza kutumia China
Daraja la Pingtang Kusini mwa Jimbo la Guizhou nchini China lenye mnara mkubwa wa semiti duniani ilianza kutumika hapo jana.
Daraja hilo liko katika eneo la Bouyei-Miao Jimbo la Qiannan, limeunganishwa na waya yenye urefu wa mita 2,135 kwenye korongo na itatumika kuunganisha barabara kuu ya Pingtang-Luodian .
Jumla ya Yuan bilioni 1.5 (karibu dola milioni 215 za Kimarekani) ziliwekezwa katika ujenzi wa daraja hilo.
Kufunguliwa kwa daraja hilo kutapunguza wakati wa kusafiri kati ya Pingtang na Luodian kutoka kwa zaidi ya saa mawili na nusu hadi karibu saa moja, na kuwezesha kuondoa umasikini katika maeneo yenye mwamba wa Gu.
Comments
Post a Comment