Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara yashika namba moja Kwa usafi
Na John Walter-Manyara
Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Manyara yanyakua Kikombe na Kitita cha shilingi Milioni Tatu baada kung’ara katika mashindano ya jumla ya Usafi na Mazingira na kuipiga chini Mikoa Mingine.
Akikabidhi zawadi hizo kutoka ofisi ya wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara Missaile Mussa amesema mashindano hayo yalihusisha Mikoa Mitatu Ya Manyara, Arusha na Katavi.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti amesema mkoa huo hausifiki kwa usafi tu bali katika Usalama na kila idara wapo vizuri.
"Sisi sio watu wa maneno tunapiga kazi, ingekuwa ni mikoa mingine angezungumzia ushindi huu mwaka mzima' alisema Mnyeti.
Naye Katibu wa Afya mkoa wa Manyara Thomas Malle anasema mafanikio hayo wameyapata kwa sababu wanazingatia kanuni zote za Usafi ambazo zinafanywa na kampuni walizozipa kazi.
Comments
Post a Comment