Kiongozi Mstaafu wa Nissan akimbilia Lebanon
Kiongozi Mstaafu wa Kampuni ya Nissan, Carlos Ghosn amekimbilia nchini Lebanon kutoka Japan alimokuwa akikabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya fedha.
Hata hivyo amesema hajakimbia ili kuzuia haki isitendeke, bali ameyakimbia mashtaka ya kisiasa ambayo yanamkabili kwa sasa.
Haijajulikana Carlos amewezaje kutoka ndani ya Japan kwa kuwa alikuwa amezuiwa kusafiri kutokana na masharti makali kwenye dhamana yake.
Comments
Post a Comment