Antonio Nugaz awatuliza mashabiki Yanga kuhusu Niyonzima


Baada ya ushindi wa bao 1-0 wa Yanga dhidi ya Biashara United, afisa muhamasishaji mkuu wa Yanga Antonio Nugaz ameweka wazi kuwa Yanga bado inafanya usajili mkubwa mmoja kabla ya dirisha la usajili kufungwa.

Pia ametangaza kuwa Niyonzima ataingia jijini Dar es Salaam Jumatano hii akitokea kwao Rwanda.

“Mungua akijalia Jumatano chuma kinatua (Niyonzima) akishatua tutaambiana namna gani ya kumpokea, halafu kwamba kwa uzuri tumebakiwa na usajili mmoja mkubwa imebakia moja lazima aje mtu wa kuwalaza saa 12 na robo” amesema.

Niyonzima anarejea Tanzania tena baada ya kuondoka mwanzo wa msimu 2019/20 kutokana na kuachwa na Simba SC aliyoitumikia kwa misimu miwili akitokea Yanga SC alikodumu kwa miaka sita mfululizo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato