Bashe asema Serikali haina mpango wa kufuta kilimo cha tumbaku


Serikali haina mpango wa kufuta kilimo cha tumbaku nchini wala kuwapangia wakulima viwango vya uzalishaji kwa kuwa zao hilo ni miongoni mwa mazao yanayoliingizia taifa mapato makubwa.

Naibu waziri wa Kilimo Hussein Bashe ameyasema hayo wakati akizungumza na wakulima wa tumbaku  wilayani Kahama na kudai kuwa changamoto ya wakulima kubaki na tumbaku imemalizika  baada ya serikali kutafuta wanunuzi kutoka katika maeneo mbalimbali duniani.

Naye Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Kahama Bw. Emmanuel Charahani amesema ujio wa wadau na wanunuzi wapya umesaidia kuondosha hasara ya tumbaku iliyokuwa imekwama katika maghala na majumbani mwa wakulima.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato