Manchester United yaanza kubisha hodi nafasi za nne juu EPL


Manchester United imeanza kubishia hodi nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Uingereza baada ya kukamilisha mwaka 2019 kwa kishindo Jumamosi.

Ilizamisha wenyeji Burnley 2-0 kupitia mabao ya Anthony Martial na Marcus Rashford uwanjani Turf Moor.

Vijana wa kocha Ole Gunnar Solskjaer walijinyanyua kwa haraka baada ya kuchapwa 2-0 na Watford katika mechi iliopita na sasa wataingia mwaka 2020 na matumaini mapya wanaweza kufuzu kushiriki Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao.

Ili kutimiza ndoto ya kumaliza ndani ya mduara wa nne-bora, Martial na Rashford wataendelea kutegemewa na walidhihirisha umuhimu huo wao walipofungia United mabao katika mechi iliokuwa na nafasi chache sana nzuri za kufunga.

Moja wapo ya vitu vizuri Solskjaer alishuhudia katika mechi hiyo ni kuwa kwa mara ya kwanza United haikufungwa bao baada ya kushindwa kufanya hivyo katika mechi 14 zilizopita.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato