Mwanadiplomasia mkuu wa China apuuzilia mbali wasiwasi wa Ulaya kuhusu haki

 


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa China Wang Yi amezitetea kambi za kuwazuia watu katika jimbo la Xhinjiang na sheria mpya ya usalama ya Hong Kong akipuuzilia mbali wasiwasi wa nchi za Ulaya kuhusu haki za binaadamu na kuonya kuhusu uingiliaji wa masuala ya China.

 Akizungumza mjini Paris jana, Wang alisisitiza madai kuwa wale wote waliotumwa katika vituo hivyo vya kutoa mafunzo jimboni Xhinjiang wameachiwa huru na kupewa ajira - hata wakati makundi ya haki za binaadamu na familia wakiripoti kuhusu kuendelea kuzuiliwa kwa Waislamu wa jamii ya Waighur na kupotea kwa mawasiliano na wapendwa wao. 

Kuhusu sheria ya usalama Hong Kong alisema ilibidi wachukue jukumu la kusitisha vurugu kisiwani humo kwa kuweka sheria ya kudumisha usalama wa taifa. 

Waziri huyo yupo kwenye ziara yake ya kwanza ya Ulaya tangu janga la virusi vya corona lilipozuka akitafuta kufufua biashara na mahusiano yaliyoharibiwa na mgogoro wa kiafya na kiuchumi ulimwenguni.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato