Dirisha la usajili linafungwa leo
LEO Agosti 31 ni siku ya mwisho kwa timu kukamilisha masuala ya usajili kwa wachezaji wao itakapofika saa 5:59 ukurasa wa usajili unafungwa rasmi.
Sokoni kila timu inapambana kwa masuala ya usajili na tunaona kwamba bado zipo timu ambazo hazijatambulisha wachezaji wao ina maana kwamba bado wapo sokoni kusaka aina ya wachezaji wanaowahitaji.
Pia zipo ambazo zimeshamaliza masuala ya usajili baada ya kuwatambulisha wachezaji pamoja na benchi la ufundi wanastahili pongezi kwa kuwa wameonyesha walijipanga na wapo tayari kwa ajili ya msimu mpya.
Msimu mpya unatarajiwa kuanza Septemba 6, siku zinakwenda kasi hivyo kwa wale ambao wanadhani ni muda mrefu umebeki wanapaswa washtuke mapema.
Azam, Simba na Namungo hizi hapa tayari zimekamilisha masuala ya usajili na wachezaji wanaendelea na kambi kwa pamoja wakiwa wameshamaliza majukumu yao ya usajili.
Kagera Sugar nao pia wamekamilisha usajili wao kwa kuboresha kikosi chao na kuwapa taarifa mapema wachezaji ambao hawatakuwa ndani ya kikosi hicho.
Ruvu Shooting nao waliwaacha wachezaji kadhaa na taarifa zao ilikuwa ni mapema kama ilivyokuwa kwa Yanga hili pia nalo linastahili pongezi kwani kuwapa wachezaji taarifa mapema inawapa nafasi ya kutambua kwamba wanapaswa wafanye jambo gani.
Comments
Post a Comment