Tetesi za soka kimataia
Manchester City wanajianda kulipa kiasi cha pauni Milioni 450, ili kuweza kusajili Lionel Messi ikiwa ni mpango wa kumsajili kwa miaka mitano na sehemu ya mkataba huo kujiunga na timu New York City, (Sport, via Daily Star)
Tottenham ilijaribu kutaka kuingilia kati na kuvurugwa uhamisho wa kiungo wa Ajax Donny van de Beek, anayekwenda kujiunga na Man United.
Manchester United imefanya mazungumzo na Aston Villa wakati inajitahidi kufikia makubaliano ya mchezaji Muingereza Jack Grealish, 24. (Mail)
Manchester United imejiunga na Liverpool katika kinyang'anyiro cha kumsaka kiungo wa kati ya Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 29. (Dagbladet TV, via Sun)
Leeds United imeonesha nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Udinese raia wa Argentina Rodrigo de Paul,26, lakini imearifiwa kwamba hatua yoyote ya kumsajili mchezaji huyo itawagharimu pauni milioni 31. (Guardian)
Tottenham na Newcastle zimeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na Norway Josh King, 28. (Chronicle)
Valencia imemuulizia kiungo wa kati wa Arsenal Matteo Guendouzi, 21, raia wa Ufaransa. (Super Deporte - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Chile Arturo Vidal, 33, atakuwa huru kurejea klabu yake ya zamani ya Juventus. (Goal
Kocha wa Inter Milan Antonio Conte anataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 29, kutoka Chelsea. (Football Italia)
Wakala wa Emerson Palmieri amesema Inter inapania kumsajili beki wa kushoto wa Italia, 26, kutoka Chelsea msimu huu. (Goal)
Mshambuliaji wa Ufaransa wa West Ham Sebastien Haller, 26, amekataa fursa ya kujiunga na Hertha BSC. (90 mins)
Barcelona italazimika kulipa pauni milioni 12 ikiwa inataka kukatiza mkataba wa mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 33. (Goal)
Wakala wa kiungo wa kati wa Roma Amadou Diawara amesema Arsenal inamwinda mchezaji huyo wa Guinea, 23. (Tuttomercato, via Standard)
Comments
Post a Comment