Uturuki imekemea vikali kuchomwa kwa Quran nchini Uswidi
Uturuki kupitia wizara yake ya mambo ya nje imekemea vikali kiitendo cha kuchomwa moto Quran nchini Uswidi.
Uturuki imekemea vikali kitendo cha kuchomwa moto Quran kilichotokea nchini Uswidi.
Uturuki imefahamisha kuwa imeshangazwa na kitendo hicho ambacho kimetajwa kuwa kitendo cha uchokozi na uchochezi.
Uturuki imesema kuwa kitendo hicho ni pigo kubwa dhidi ya utamaduni ya kuishi pamoja na kuheshimu thamani za utofauti wa tamaduni za Ulaya.
Kitendo hicho, Uturuki imefahamisha kuwa ni kitendo cha uchokozi dhidi ya jamii ya waislamu.
Taarifa ya maandishi iliotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Uturuki zimelaani kiitendo hicho kilichotekelezwa na mwanasiasa mwenye sera za kibaguzi na chuki dhidi ya uislamu kutoka nchini Danmark .
Comments
Post a Comment