U.N. yasema maisha ya mshindi wa tuzo ya Nobel DR-Congo yako hatarini



Dkt Denis Mukwege, Mashindi wa Tuzo ya Amani ya Noble 2018Image caption: Dkt Denis Mukwege, Mashindi wa Tuzo ya Amani ya Noble 2018

Umoja wa Maitaifa umeonya kuwa maisha ya daktari wa Dr-Congo aliyeshinda Tuzo ya Nobel 2018 yako hatarini baada ya kupokea msururu wa vitisho vya mauaji vinavyotolewa dhidi yake.

Kamishena wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amelaani vitisho hivyo na kutoa wito Dkt. Denis Mukwege na familia yake kupewa ulinzi.

Bachelet pia amezishinikiza mamlaka nchini DRC kuidhinisha rasimu ya sheria ya ulinzi inayodhibiti shughuli za wanaharakati wa kutetea haki za binadamu "kwa kuzingatia viwango vya kimataifa."

Wiki iliyopita Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi aliamuru Bw. Mukwege mwenye umri wa miaka 65 kupewa ulinzi wakati uchunguzi wa tisho la mauaji dhidi yake ukiendelea.wenzakeImage caption: Dkt Denis Mukwege (Aliyevalia miwani) akiwa na madaktari wenzake

Denis Mukwege ni daktari anayeshughulikia afya ya wanawake nchini DRC. Yeye na wenzake walikuwa wamewahudumia waathiriwa 30,000 wa ubakaji kufikia mwaka 2013.

Anasema: "Nilijiuliza - ni nini haswa kilikuwa kinaendelea? Huu ulikuwa tu si uhalifu bali mikakati mahsusi. Kuna wakati ambapo watu wengi wangebakwa kwa mpigo, tena wazi mbele ya watu wengine - kijiji kizima kingebakwa usiku. Basi wanapofanya hivyo hawaumizi tu wanaowabaka bali jamii nzima inayolazimishwa kuwatizama.

Vita Mashariki mwa DRC vimewalazimisha mamia kutoroka makwao hali inayohatarisha maisha yao.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato