TDL Yajizatiti kukuza sekta ya kilimo cha zabibu nchini
Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), imeeleza dhamira yake ya kuendeleza kilimo cha zabibu mkoani Dodoma pamoja na matarajio yake ya kuingia mikataba ya kununua zabibu moja kwa moja kutoka kwa wakulima wadogo.
Mchango wa TDL wa sera yake ya kununua malighafi nchini na dhamira ya kukuza sekta ya kilimo cha zabibu inaenda sambamba na jitihada za serikali za kuboresha maisha ya wakulima wadogo na kukuza uchumi wa Tanzania.
TDL inaamini jitihada za Serikali za kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda zinaweza kufanikiwa ikiwa wakulima wadogo wanawezeshwa kuzalisha malighafi inayohitajiwa na viwanda.
Meneja Mkuu wa TDL, Devis Deogratius, alisema kampuni hiyo kwa sasa inanunua takribani lita milioni 1.2 za mchuzi wa zabibu kwa mwaka kutoka kampuni za CETAWICO na UWAZAMAM, ambazo zinanunua zabibu za wakulima wa ndani ambapo inatumia bilioni 3.3 kwa mwaka.
Deogratius aliongeza kusema kuwa imedhamiria kununua malighafi ya ndani katika kipindi chote cha miaka ijayo ambapo kwa sasa inatumia malighafi na huduma za kufanikisha uzalishaji kwa asilimia 80% ambayo ni sasa na shilingi bilioni 46.
TDL imewekeza katika uundaji wa chapa za Kitanzania ambazo ni pamoja na: Imagi, Valeur, Wines Dodoma, Dodoma Rose, Konyagi na Zanzi Cream liqueur ambazo zimetengenezwa kwa viwango vya ubora kwa kimataifa kwa kulenga mahitaji ya makundi mbalimbali katika soko.
Comments
Post a Comment