Killy na Cheed waangukia kwa Harmonize
Wasanii waliotoka kwenye lebo ya Kings Music Records ambayo inamilikiwa na msanii Alikiba, Official Killy Tz na Official Cheed wameonekana kuwa upande wa msanii Harmonize baada kuonyesha kumpa sapoti msanii huyo.
Hali hiyo imekuja baada ya Killy na Cheed kupost matukio ambayo anayafanya Harmonize kwenye kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram, huku watu wakiwatarajia huenda wao ndiyo wakawa wasanii wapya wa lebo ya Konde Gang.
Ukifuatilia tukio la Harmonize kwenye kilele cha siku ya Wananchi Uwanja wa Benjamin William Mkapa, msanii Killy alimpost Harmonize akiwa amevaa mavazi ya kijeshi kisha kuandika "Mmakonde mmoja".
Pia ukifuatilia post yao ya mwisho kabla ya hiyo ya jana, Cheed na Killy wote walishea post ya video mpya ya Harmonize iitwayo Jeshi kwenye kurasa zao za Instagram.
Comments
Post a Comment