Tembo 12 wafa katika mazingira ya kutatanisha Zimbabwe
Mamalaka ya hifadhi ya wanyama nchini Zimbabwe zinachunguza jinsi tembo 12 walivyokufa katika mbuga ya kitaifa ya Hwange.
Tembo hao walipatikana wakiwa wamekufa wakiwa na pembe zao.
Mamlaka zinasema hazina hofu kwamba huenda wametiliwa sumu ya cyanide - ambayo pia hutumiwa na wawindaji haramu badala ya silaha- kwani hakuna wanyama wengine walioathirika
Sampuli ya damu imechukuliwa kutoka kwa tembo hao kuchunguza kilichosababisha vifo vyao.
Mbuga ya kitaifa ya Hwange National inakaribia mpaka wa Botswana ambako mamia ya mizoga ya tembo ilipatikana mwaka huu.
Comments
Post a Comment