Kiongozi wa upinzani Congo arejea Brazzaville baada ya kutibiwa Uturuki
Kiongozi wa upinzani wa Congo - Brazzaville Jean-Marie Michel Mokoko amerejea Brazzaville jana baada ya kutibiwa nchini Uturuki kwa mwezi mmoja uliopita.
Jenerali huyo mwenye umri wa miaka 73, aliyepambana na Rais mwenye msimamo mkali Denis Sassou Nguesso katika uchaguzi wa 2016, alifungwa miaka 20 jela mwaka wa 2019 kwa mashitaka ya kuhujumu usalama wa taifa na kumiliki silaha kinyume cha sheria.
Wakili wake Yvon Ibouanga amesema Jenerali Mokoko amerudi akitokea Uturuki na kupelekwa katika hospitali ya kijeshi mjini Brazzaville ambako alifanikiwa kuonana naye.
Amesema kiongozi huyo yupo katika hali nzuri na kuwa ombi rasmi la kutaka aachiwe huru litawasilishwa katika siku chache zijazo.
Duru ya idara ya magereza imesema atarudishwa katika chumba chake gerezani baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari.
Comments
Post a Comment