Bunge la Macedonia Kaskazini lamuidhinisha Zoran Zaev kuwa waziri mkuu



Wabunge wa Macedonia Kaskazini wamemuidhinisha Zoran Zaev kuwa waziri mkuu baada ya kumpigia kura 62 dhidi ya 51 kuchukua wadhifa huo. Zaev anatarajiwa kurejea ofisini baada ya kuondoka Januari, kufuatia mpango uliofikiwa mwezi huu kati ya chama chake cha Social Democratic - SDSM na Democratic Union for Integrations - DUI, chama kikubwa kinachoiwakilisha jamii ya Waalbania. 

Ratiba ya Zaev ni pamoja na kumteuwa waziri mkuu mwenye asili ya Kialbania mwishoni mwa muhula wa serikali.

 Kura hiyo imepigwa baada ya saa nyingi za mdahalo jana. Itakuwa mara ya kwanza tangu nchi hiyo iliyojitenga kutoka Yugoslavia ya zamani mwaka wa 1991 kuwa na waziri mkuu mwenye asili ya Kialbania. Waalbania wamekuwa wakishinikiza kupewa haki zaidi tangu nchi hiyo ilipopata uhuru.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato