Korea Kaskazini yamuonya Waziri Mkuu wa Japan
Korea Kaskazini leo imemuonya waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe kuwa hivi karibuni anaweza kushuhudia kile Pyongyang imekiita "Kombora Halisi la Masafa Marefu" baada ya Abe kukosoa majaribio ya mifumo ya ufyetuaji silaha yaliyofanywa na Korea kaskazini.
Matamshi hayo yamekuja siku mbili tangu Korea Kaskazini ilipofanya majaribio ya kile ilichokiita " mfumo mkubwa wa kufyetua makombora" huku Korea Kusini ikiripoti kuwa makombora mawili yalianguka kwenye eneo la bahari ya Japan inayofahamika pia kuwa bahari ya mashariki.
Wakati wa majaribio hayo yaliyosimamiwa na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, Waziri Mkuu Abe alisema Korea Kaskazini ilifyetua makombora ya masafa marefu yanayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Korea Kaskazini imesema ni fedheha kuwa Abe ameshindwa kutofautisha kati ya makombora ya masafa marefu na mfumo mpya wa kufyetua makombora ambao nchi hiyo inadai uliuzindua siku mbili zlizopita.

Comments
Post a Comment