Hizi ndio mechi ambazo hutakiwi kuzikosa leo, Samatta ataendelea kutupia?


Jumamosi ya leo ligi mbali mbali barani ulaya zinaendelea kutimua vumbi huku Mbwana Samatta na klabu yake ya KRC Genk wakiwa miongoni mwao.

Genk ambao watakuwa katika uwanja wa nyumbani wanatarajiwa kushuka dimbani usiku wa leo majira ya saa 4.30 kucheza dhidi ya Sint-Truidense VV.

Michezo mingine ambayo inapigwa leo na hutakiwi kuikosa ni Newcastle United ambao watacheza na Manchester City, Chelsea na West Ham United, Liverpool na Brighton.

Pia Totenham Hotspur watacheza na Bournemouth, Bayern Munich dhidi ya Bayer Leverkusen, wakati Alaves dhidi ya Real Madrid.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato