SOLEO yachangia bidhaa za thamani ya Sh. milioni 52.9 kwa Halmashauri ya Mkuranga
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga yapokea pakiti 264,600 kutoka SOLEO zenye thamani ya shilingi milioni 52.9 kwa ajili ya msaada kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambazo ni virubisho vilivyo na mchanganyiko wa Vitamini na madini.
Akitoa ufafanuzi katika kampeni ya uzinduzi wa Mpango wa kupunguza utapia mlo Wilaya ya Mkuranga iliyoandaliwa na kamati ya Lishe Wilayani humo, iliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mikere jana, Makamu Mkurugenzi wa shirika hilo Grace Mghamba amesema virutubisho hivyo ambavyo ninaweza kutumiwa na watoto 5880 wamegawa bure wakiwa na lengo la kumsaidia mtoto kwa ajili ya kuondoa utapia mlo na udumavu.
Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Kaimu katibu Tawala wa Mkoa Abdulrahman Mdimu, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Mkuranga kwa kuanzisha Mpango huu ambao katika Mkoa wa Pwani ni Mkuranga Pekee ndiyo imejipanga na kuhakikisha inaondoa tatizo hilo baada ya kuona Katika baadhi ya Kata zake 10 zinaongoza kwa watoto waliokosa Lishe bora.
Awali Mdimu akikagua Bustani ambayo imeandaliwa shuleni hapo kama shamba darasa la kulima mbogamboga na mahindi kwa ajili ya chakula, amepongeza kwa hatua hiyo na kuitaka kamati ya Lishe Wilaya ya Mkuranga kuongeza juhudi katika kuboresha Afya na kueneza elimu hiyo katika jamii.
Katika kuhakikisha hii kampeni inakuwa na tija katika jamii, Diwani wa kata ya njia nne, Sultani Cheche “Dr Cheche”, ameahidi kujitolea trekta kwa ajili ya kulima bure katika shul zote ndani ya Kata yake ambazo zitajihusisha katika kulima na kuzalisha mazao ya Lishe na kusema zoezi hili litakuwa endelevu.
Katika uzinduzi huo viongozi na wawakili wa taasisi na NGO’s mbalimbali walipata fursa ya kutoa taarifa zao za namna gani wamejipanga kuhakikisha tatizo hilo la utapia umlo na udumavu kwa wototo chini ya miaka mitano linaisha ndani ya Wilaya ya Mkuranga.
Comments
Post a Comment