RC Ndikilo azindua mnada wa Korosho Pwani

Na: Said Likacha - Pwani

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amezindua mnada wa Korosho kwa Mkoa wa Pwani kwenye ghala la kuhifadhia mazao ya nafaka Wilaya ya Mkuranga juzi, huku akiwataka wahusika kuhakikisha ndani ya siku kumi wakulima wanapata malipo yao.
Katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa na Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti  wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmshauri sambamba na Bodi ya korosho Tanzania (CBT), Ndikilo ambaye alishuhudia mnada huo wa wazi aliwapongeza washindi wa Kampuni ya Alpha  Choss ambayo itanunua Korosho zote daraja la kwanza kwa Shilingi 2,571 kwa kilo nao (CDJKL) wataonunua daraja lapili kwa Shilingi 2,300 kwa kilo.
Ndikilo pamoja na kutangaza mnda wa pili kufanyika Desemba 4 mwaka huu alitumia fursa hiyo kumwagiza Meneja wa Bodi ya Korosho (CBT) Kanda ya Dar es salaam na Pwani Matata afikishe ombi kwa Waziri mwenye dhamana ili Korosho zisizokidhi madaraja hayo mawili ziuzwe kwa mnada kwenye Vyama vya Msingi (AMCOS).
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa aliwaagiza wakuu wa Wilaya kuwahamasisha wakulima kupalilia mashamba yao mapema na ikibidi watumie sheria kuwabana wakulima watakaokiuka taratibu hizo.
Awali Ndikilo aliongoza kikao cha wadau wa Korosho Mkoa na kuwahakikishia wakulima wanaodai malipo yao watapata malipo hayo baada ya oezi la kurudisha fedha Viongozi wa (AMCOS) wabadhilifu na uhakiki.
Ufunguzi wa mnada huo ni dalili tosha kuwa zoezi hilo la ukusanyaji na ununuzi wa Korosho kupitia mfumo wa Stakabadhi ghalani utakuwa umefungua njia kwa wilaya nyingine zilizo ndani ya mkoa wa pwani kuanza kufanya Minada kwa ajili kuuza Korosho.


Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato