Serikali yaombwa kutatua tatizo la magunia Masasi
Na Hamisi Abdulrahmani, Masasi. Serikali imeombwa kuingilia kati suala la tatizo la ukosefu wa magunia ya kuhifadhia korosho za wakulima wilayani Masasi mkoani Mtwara ambapo bado korosho nyingi za wakulima zipo majumbani mwao na zinashindwa kupelekwa katika minada kutokana na tatizo hilo. Hayo yalisemwa jana wilayani Masasi na madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi kwenye kikao chao cha kawaida cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika kijiji cha Mbuyuni makao makuu mapya ya Halmashauri hiyo. Walisema kuwa korosho nyingi bado zipo majumbani kwa wakulima zimehifadhiwa sakafuni na kwamba zinashindwa kukusanywa na kupelekwa katika minada inayofanyika kutokana na uhaba wa magunia. Walisema hata idadi ya korosho zilizouzwa kwenye minada na zilizopo kwa wakulima kwa kukosa magunia idadi kubwa zile ambazo zimekwama kwa kukosa magunia ya kuhifadhia. Musa Msanga diwani kata ya Lulindi alisema wanaiomba serikali kuingilia kati suala la uhaba wa magunia kwa wakulima. Alisem...