Samuel Eto'o atolea macho kazi ya ukocha


Mwanasoka mashuhuri wa Cameroon Samuel Eto'o amesema yeye ni mwanasoka bora wa muda wote wa Afrika na sasa analenga kupata mafanikio zaidi kama kocha.

Eto'o mwenye miaka 38 anafikiria hatua yake inayofuata baada ya kutundika viatu vyake mapema Septemba, na kustaafu soka akiwa na Qatar Sports Club.

 Amesema inafika wakati unalazimika kuangalia changamoto nyingine, na ndio alilopanga kufanya. Amecheza mpira wa kulipwa kwa zaidi ya miaka 20 ambapo ameshinda makombe makubwa 18, yakiwemo ya Champions Leagues mawili akiwa na Barcelona na jingine akiwa na Inter Milan.

Pia ameshinda Kombe la mataifa ya Afika mara mbili akiwa na Cameroon pamoja na medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 2000.

Hata hivyo tuzo ambayo anaitamani na hajaitia mikononi ni ya Ballon d'Or. George Weah wa Liberia anabakia kuwa Mwafrika pekee aliyepata tuzo hiyo mwaka 1995, lakini hilo halijamfanya Eto'o aondoe imani yake kwamba yeye ni mchezaji bora kutoka bara hilo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato