Mo Dewji aeleza mkasa mzima wa kutekwa kwake


Mfanyabiashara Bilionea, Mohammed Dewji amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu sakata lake la kutekwa nyara mwaka jana na namna alivyotishiwa maisha yake.

Katika mahojiano na BBC Swahili, Mo ameeleza kuwa kwa kipindi kizima, alihisi kwamba kuna uwezekano mkubwa hatoweza kutoka salama na kuwa mwisho wake wa maisha unakaribia.

"Saa 24 za kwanza baada ya kutekwa zilikuwa kama mwezi, imani ndio kitu kikubwa kilichonisaidia katika kipindi kizima. Walinifunga macho, miguu na mikono kwa siku tisa. Tulikuwa hatuongei sana, walikuwa sio watu wa hapa," ameeleza Mo.

"Asubuhi walikuwa wananifungua mikono wananifunga mbele, lakini usiku ndio kulikuwa na mitihani walikuwa wananifunga nyuma. Na wakikufunga nyuma maanake huwezi kulala, lazima ulale kulia au kushoto."

Mo anasema alikuwa akitoa ushirikiano kwa kila alichotakiwa kufanya. Kikubwa anasema alikuwa akimuomba Mungu atoke salama ambapo siku ya tisa walimsukuma pale Gymkhana na kuondoka zao.

Mo Dewji alitekwa Oktoba 11 2018 na watu wasiojulikana alfajiri wakati alipokuwa akielekea mazoezini alipofika katika hoteli moja ya kifahari katika eneo la Oysterbay jijini Dar es Salaam kama ilivyo ada yake kila siku alfajiri kwa ajili ya kufanya mazoezi ya viungo.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato