RC Kagera ateketeza zana za uvuvi haramu
Na. Clavery Christian, Kagera
Afisa uvuvi Mkoa Kagera, Bw, Gabrieli Mgaene amesema kuwa zana za uvuvi haramu zenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 zimekamatwa katika msako ulifanywa na kikosi cha kudhibiti uvuvi haramu katika ziwa victoria na kufanikiwa kukamata Mitego ya kuvulia samaki aina ya makokoro 197 na nyavu zenye macho madogo ambayo hayafiki inchi 6 zinazo ruhusiwa kisheria 19,620 na nyavu za dabo ambazo zina macho zaidi ya ishirini na sita 1.200 na monofilamenti neti 1,880 na nyavu za dagaa zenye macho madogo chini ya milimita 8/40 zimeteketezwa kwa moto baada ya mahakama kudhibitisha kuwa ni zana haramu na ziteketezwe kwa mujibu wa sheria.
Awali akiongea na wananchi wa kata ya miembeni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brig. Jen Marco E Gaguti amewataka wananchi katika mwalo wa Nyamkazi wilayani Bukoba katika mkutano wa hadhara na wavuvi amesema kuwa mkoa Kagera ni miongoni mwa mikoa mitano hapa nchini ambayo iko chini katika kuchangia pato la taifa na wakati mkoa wa Kagera una fursa za kutosha kuweza kuchangia vizuri pato la taifa na ukiwa mkoa pekee unaopakana na nchi 4 za afrika.
''Ujumbe wangu wa leo mkubwa nataka kila mtu ajitafakali ni kwa jinsi gani anaweza akaongeza tija kwenye kazi anayoifanya, uwe ni mvuvi uwe ni mfanyabiashara wa samaki. Nataka kuona fikra na vikundi vinavyofikiria kuacha kufanya biashara hapa kwenye mwalo na kwenda kutafta masoko nje ya nchi na ndani ya nchi kule ambako bidhaa zetu hazifiki tunaongelea kufanya kazi yenye tija katika sekta ya uvuvi lakini uvuvi huu lazima uwe uvuvi endelevu ili sisi wenyewe tunufaike na mazao yanayotoka ziwani na vizazi vyetu vijavyo,'' Alisema RC Gaguti.
Aidha amewataka wataka wakazi wa kata miembeni kulinda rasilimali za ziwa victoria walizopewa na mwenyezi Mungu ili ziweze kuwasaidia watoto wao huko mbeleni ambapo amesema kuwa swala la kulinda na kutunza rasilimali za nchi siyo swala la serikali ni swala la kila mmoja na ni wajibu kikatiba hivyo kuwataka kuwa walinzi wa kwanza na kukemea na kuchukua hatua kwa wale wote watakao hujumu rasilimali zilizopo katika ziwa victoria.
Comments
Post a Comment