Niliowaamini walinikimbia, niliuza gari kumuuguza mwanangu - Munalove
Mwanadada aliyejipatia umaarufu kupitia mitandao wa kijamii wa Instagram, Munalove ambaye mwaka jana alifiwa na mtoto wake wa pekee Patrick baada ya kuugua kwa muda mrefu ameweka wazi story yake tangu kumuuguza hadi mtoto huyo anafariki.
Akizungumza, Muna amesema hakuna mtu yeyote aliyemsaidia katika kipindi alichokuwa anamuuguza mtoto wake, hali iliyosababisha kuuza gari ili kupata fedha za kumuuguza.
Amesema alipitia wakati mgumu alipokuwa akimuuguza lakini watu wote aliowaamini wamlimkimbia katika kipindi alichowahitaji zaidi.
“Watu hawajui nilihangaika kwa kiasi gani kwasababu hawajui hata Patrick alifika vipi hapa gharama gani nililipia lakini wao walikuwa wana kazi ya kunichafua tu kwenye mitandao bila kujua nilichokuwa ninapitia.
“Kuna wakati nilitamani hata kujiua au mwanangu aamke awaambie kuwa wanamsingizia mama yangu, wale wote niliokuwa ninawaamini walinikimbia nikabaki peke yangu na nilikataa kuwapa mwili hadi tulipoandikishana wakubali kwamba nilihangaika mwenyewe bila kupata msaada wa mtu yeyote.
“Hata yule aliyekuwa anadai mtoto ni wake hakukanyaga mochwari badala yake alimtuma rafiki yake, nakumbuka Casto alinitumia meseji akaniambia anaumia anaposikia maneno yaliyokuwa yanaendelea na hivyo akanitaka nikubali tu ili tumpumzishe Patrick kwa heshima,” amesema Munalove
Comments
Post a Comment