Mtoto mlemavu atelekezwa na wazazi, walezi waomba msaada


Na George Bahemu Ngara-Kagera

Mtoto mlemavu ambaye ana umri wa miaka nane atelekezwa na wazazi wake kutokana na ulemavu wake katika kijiji Cha Mhweza katani Mabawe wilayani Ngara mkoani Kagera.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema mtoto huyo alizaliwa akiwa mzima muda ulipofika wa kutembea na kutambaa haikuwezekana kutokana na ulemavu wake.

Wakizungumza na Muungwana Blog wamesema kuwa mtoto Mama yake baada yakuona nimlemavu alimuacha kwa Bibi yake nakwenda kuolewa wilayani humo.

Renatha ambaye ni jirani na Neema amesema kuwa mtoto huyo alizaliwa akiwa sawa na muda wakutambaa na kutembea haikuwezekana na hospitali hawakufanikiwa kuona tatizo la mtoto huyo.

"Huyu mtoto alizaliwa mwaka 2011 lakini mpaka sasa hatembei wala kusimama yeye ni wakulala tu na Mama yake baada ya kuona ni mlemavu alimkana na matumizi hatoi hata mia." Amesema Renatha

Japheth Emily ni mjomba wake Neema amesema kuwa hajafurahishwa na kitendo alichokifanya Mama yake kwenda kuolewa nakuacha mtoto anahangaika nakuiomba serikali na jamii kwa ujumla iweze kumsaidia mtoto huyo.

Selina ambaye ni Bibi yake na mtoto huyo lakini pia ni mlezi wa mtoto huyo amesema anashindwa kufanya shughuli zake za nyumbani kwani muda mwingi huutumia kulea mtoto huyo.

"Huyu mtoto haongei, hatembei wala kusimama napata shida wakati wa kuaandaa mashamba yangu ili tuwe tunapata chakula na Baba yake alimkana hata sukari yakumsaidia mtoto hatuletei." Amesema Selina

Pamoja na hayo viongozi ambao ni wakazi wa eneo hilo wamesema hawafurahishwi na wazazi ambao wanatelekeza watoto wao kisa ni walemavu nakuiomba serikali na wananchi waweze kumsaidia mtoto huyo ili apate mahitaji yake ya kila siku.

KWA MCHANGO ZAIDI WA MTOTO HUYO NEEMA AMBAYE ANAOMBEWA MSAADA NA MLEZI WAKE 0754990242.



Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato