Aliyemuua Mwanamuziki Radio ahukumiwa miaka 14 Jela
Mahakama Kuu nchini Uganda imemuhukumu kifungo cha miaka 14 jela Godfrey Wamala maarufu Troy kwa kosa kumuua mwanamuziki Moses Ssekibogo maarufu Mowzey Radio. Troy alipatikana na hatia siku ya Jumatatu
Radio alifariki Februari 1, 2019 baada ya kupigana na Troy wakiwa baa mwaka jana.
Godfrey Wamala amekutwa na hatia ya kumuua Moses Sekibogo (Mowzey Radio) bila ya kukusudia. Hukumu hiyo imesomwa licha ya Mwanamuziki huyo kufariki katika ghasia zilizotokea sehemu ya starehe
Kesi ilikuwa ikiendeshwa na Jaji Jane Abodo katika Mahakama Kuu Entebbe, Jaji amesema kuwa Godfrey Wamala atatumikia miaka 13, miezi 3 na siku 4 baada ya kukaa mahabusu kwa mwaka mmoja.
Comments
Post a Comment