Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 10:00 asubuhi huko Kijiji cha Kibisi, Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Askari Polisi waliwakamata 1. Ambokile Mwaisabila (38), 2. Isaya Christopher (28) na 3. Zaina Kasim (26) wote wakazi wa Kibisi wakiwa na Pombe Moshi @ Gongo ujazo wa lita kumi na mbili (12). Watuhumiwa ni wauzaji na wanywaji wa Pombe hiyo. Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 11:50 asubuhi huko katika Kitongoji na Kijiji cha Itete – Ndembo, Kata ya Kabula, Tarafa ya Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya, Askari Polisi walimkamata Tunu Kijumile (21) mkazi wa Ndembo akiwa anauza pombe haramu [gongo] ujazo wa lita tatu (03) Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa gongo. Mnamo tarehe 30.10.2019 majira ya saa 14:30 mchana huko Igawa, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi wakiwa katika operesheni maalum walimkamata Damin Mpinga (71), mbena, mkulima, mkazi wa igawa akiwa na gongo ujazo wa lita 10 katika chupa 20...