Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dkt, Eliezer Feleshi, amefanya mazungumzo na wadau kutoka Benki ya Dunia(WB) juu ya tathmini ya Mradi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania yanayofanywa chini, ambapo umeleta matokeo chanya katika shughuli za Mahakama. Akizungumza na ujumbe wa benki hiyo, katika ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania, Jaji Kiongozi alisema mradi huo, umeweza kusaidia kuboresha shughuli za utendaji kazi wa Mahakama na kusogeza huduma karibu na wananchi. “Tumeweza kusikiliza kesi kwa kutumia Mahakama Inayotembea (Mobile Court) jijini Mwanza, hivyo ni moja ya maboresho ya huduma za Mahakama, yaliyotokana na mradi huu,” alisema Jaji Kiongozi. Aliongeza kuwa mradi huo unaofadhiliwa kwa fedha za mkopo kutoka benki hiyo, umewezesha Mahakama ya Tanzania,kusikiliza kesi kwa njia ya Mtandao ‘Video coference’, ambapo, ugeni huo, ulitaka kufahamu tathimini ya eneo hilo, alisema umeweza kutumika ...