Watumishi wa Mahakama ya Tanzania wapewa darasa


Watumishi wa Mahakama ya Tanzania watakaofanya kazi katika Mahakama Inayootembea ‘Mobile Court’ katika jijini la Dar es Salaam, wametakiwa kuwa tayari kufanya kazi katika  mazingira mapya ya Mahakama hiyo, ili kutoa huduma bora za  kimahakama.

Akizungumza katika ukumbi wa kufanyia mikutano Kitengo cha Maboresho ya Huduma  za Mahakama ya Tanzania (JDU) , Mtaalam kutoka Benki ya Dunia (WB),Waleed Malik amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano bila  kujali nyadhifa za utumishi wao,

 Aidha  ameongeza kwa kusema kuwa si mtu mmoja atakaye husika katika utendaji kazi wa Mahakama hiyo , bali jopo la watumishi , ambapo aliwataja baadhi yao akiwemo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Karani, Afisa Habari, Katibu Mahususi, Mtaalam wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dereva.

“Mnatakiwa kuwa tayari kupata taarifa za ghafla ambazo zitawataka kufanya maboresho katika utendaji kazi wenu, na namna ya kutatua matatizo ya ghafla yanayotokea katika vifaa vinavyotumika kufanyia kazi ndani ya Mahakama hii kutoa taarifa na kupokea taarifa kwa umma juu ya ufanisi wa utendaji kazi,” alisema Waleed.

Waleed alifafanua kwamba wanatakiwa kufanya kazi kwa ufanisi ili kuweza kuleta matokeo chanya juu ya Mahakama hiyo na faida kwao katika  utendaji kazi.

Aliongeza wanatakiwa kuendelea kutoa elimu na kutoa vipeperushi kuhusu Mahakama hiyo, ili wananchi wapate kuilewa na kupata huduma mbalimbali.

Comments

Popular posts from this blog

Mwenyekiti aishauri Serikali kuhalalisha uchangudoa ili kujipatia mapato